Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo"

Kama yeye sio dikteta Babu Seya na mwanae wako wapi???

Babu seya weka hukumu yake hapa na ushahidi uliompelekea kufungwa, yote alikaa akayapika Kikwete? nendeni huko, hamna hoja, tena mahakimu waliotowa hukumu na walioipitia rufaa wasikusikie wanaweza kukuchukulia hatuwa kwani unawabeza wao. Kikwete inamuhusu nini? au na wewe ni mtu wa kusikiliza maneno ya mitaani na si ya mahakamani? halafu unajiita "great thinker"? Unanshangaza sana.
 
.....ni kweli, alienda kuongea na wazee wenzake, wazee waliochoka kimwili na zaidi kifikra, aliendeleza mipasho, jadi ya ccm, kulinda hoja dhaifu wanazotoa;

..alipozikosa zabibu akasema ni mbichi. Huna hoja. Hebu nukuu mpasho mmoja hapa kama wewe ni mkweli wa nafsi yako. Ukishindwa basi ujuwe huna ila "dhanna".
 
Ukweli ni upi?

Ni kuwa katiba ipo na ndiyo inayotuogoza mpaka hapa tulipofikia na ndiyo itayotumika mpaka itaporekebishwa au kufutwa, na si vinginevyo. Huo ndiyo ukweli na ukweli unauma siku zote kwa wale wasioupenda. Katiba mpya itakuwa tayari by 2014, au hilo hamlipendi?
 
Rais amepotosha Watanzania
TUMEMSIKILIZA kwa umakini wote Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa taifa, kupitia kwa wazee walioelezwa kuwa ni wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliowaita katika ukumbi wa PTA Sabasaba juzi, na hatimaye tumejiridhisha pasipo shaka yoyote ile kuwa tukio zima na kauli nyingi zilizotolewa na rais, kama si zote, ziliupotosha umma wa Watanzania, pengine kwa masilahi yake na chama chake (CCM).

Mosi, tukio la rais liliupotosha umma kwa kuelezwa kuwa rais anazungumza na wazee wa Dar es Salaam, wakati ukweli wa mambo ni kuwa rais alikuwa akihutubia wazee wa CCM na ambao u-CCM wao ulionekana waziwazi pale walipokuwa wakimshabikia kichama na kulifanya tukio zima kuchukua sura ya kichama, badala ya kuwa tukio la kitaifa la rais kuzungumza na wananchi bila kujali vyama vyao.

Pili, Rais alipotosha hoja ya vyama vya wapinzani, wasomi, wanaharakati, viongozi wa dini na wananchi wengine, ya kutaka Katiba mpya, ambayo huko nyuma aliwahi kuikubali na kutangaza mchakato wake utafanyika, lakini juzi katika hali ambayo haikutarajiwa, rais alichomeka hoja mpya, ya kuhuisha Katiba (yaani kuifanyia marekebisho Katiba ya sasa), huku akijua fika kuwa hitaji la Watanzania wengi si marekebisho, bali ni Katiba mpya.

Tatu, rais aliupotosha umma pale aliposema yeye ndiye mwenye uhalali na mamlaka ya kipekee ya kuunda tume ya Katiba na kuteua wajumbe wake, akidai kuwa ndiye aliyechaguliwa na wananchi wengi, ukweli ni kwamba mamlaka ya rais yanaishia kwenye Katiba ya sasa iliyomweka madarakani na si kwenye Katiba mpya ijayo, isitoshe ameingia madarakani kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyotokana na Katiba mbovu iliyopo, kwa hali hiyo, hawezi kuwa na uhalali wala mamlaka ya kipekee ya kuwaundia Watanzania tume ya kupata Katiba yao mpya (alichofanya ni kulazimisha tu, kwa kutangaza kuwa atausaini muswada huo uwe sheria).

Nne, rais aliupotosha umma pale aliposema kwamba asipounda tume ya Katiba hakuna mtu mwingine atakayeweza kuiunda, ukweli ni kwamba tume ya Katiba ikiundwa na rais kama anavyotaka, haitatenda haki, itafanya kazi ya kulinda masilahi ya rais na chama chake (CCM), badala yake tume inapaswa kuundwa na wajumbe wa kuchaguliwa kutoka kwenye makundi yote ya uwakilishi wa wananchi, kama vile viongozi wa dini, asasi zisizo za kiserikali, vyama vya siasa, wasomi, walemavu na makundi mengine yote ya kiuwakilishi (hii ingesaidia taifa kupata Katiba mpya ya wananchi badala ya kupata katiba ya rais iliyohuishwa na tume aliyojiundia mwenyewe).

Tano, rais aliupotosha umma kwa kupindisha hoja nyingine ya wapinzani, wasomi, wanaharakati na wananchi wengi, akisema wamemuita dikteta, ukweli wa kilichoelezwa ni kwamba madaraka makubwa aliyonayo rais kupitia Katiba ya sasa hayapaswi kuendelezwa katika mchakato wa kupata Katiba mpya, kwani ni makubwa kupita kiasi na akiamua kuyatumia anaweza kabisa kuwa dikteta, kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Sita, rais aliupotosha umma alipotetea hoja ya muswada wa mabadiliko ya Katiba kusomwa kwa mara ya pili bungeni, ukweli ni kwamba uliposomwa kwa mara ya kwanza ulikataliwa na ulipelekwa kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ili ikusanye maoni nchi nzima na kuishauri serikali kuuboresha, lakini kamati hiyo licha ya kuandaa ratiba yake ya kukusanya maoni ya wananchi kwenye kanda takriban nane za nchi nzima, Spika aliinyima fursa ya kufanya hivyo.

Kwa hiyo, muswada ulioletwa bungeni haukutokana na ushauri wa kamati kama taratibu zinavyotaka, badala yake serikali iliandika muswada mpya kabisa kwa utashi wake na kuuleta kwenye kamati na baadaye bungeni, ambao licha ya kuwa katika lugha ya Kiswahili, bado maudhui yake mengi ni mapya, na kwa hiyo, kwa mujibu wa taratibu, muswada huo mpya ulipaswa kusomwa kwa mara ya kwanza ili wananchi wapate fursa ya kutoa maoni yao.

Tanzania Daima Jumapili, tumesikitishwa sana na kauli nyingi za upotoshaji zilizotolewa na rais, lakini zaidi tunalaani kitendo kilichofanywa na wabunge wa CCM, CUF, TLP, na UDP wakiongozwa na Spika, Anne Makinda, cha kupitisha muswada mpya wa mabadiliko ya Katiba bila kuwapa Watanzania fursa ya kutoa maoni yao ya kuamua mchakato wa kupata katiba yao uweje.
Tunahamasisha Watanzania wote kupinga sheria hiyo mpya inayotarajiwa kusainiwa na Rais Kikwete, kwani kwa namna yoyote ile haitawapatia Katiba mpya waitakayo.

SOURCE: Tanzania Daima


SOURCE: Tanzania Daima

Hiyo source hata Kabwe Zitto hana imani nayo, ni ya nani hiyo?
 
Katiba ndiyo ilimpa nyerere udikteta wa kuweza kumpa na kumuondolea mtu Uhuru, katiba hiyo hiyi ikaonekana ni ya kidikteta na Mzee Ruksa akaibadili toka kufungwa bila sababu kwa muda wowote anaoutaka nyerere mpaka kufikia siku 40 tu mwisho. Au hilo hulijuwi? kama hulijuwi rejea hotuba ya Kikwete, kalielezea. Labda wewe ndiyo huijuwi katiba na usifikiri kuwa katiba ni msahafu kuwa kila mtanzania ataujuwa, hata ufanye vipi. Vitabu vya Mungu leo vina miaka kwa maelfu na watu wengi hawavijui itakuwa katiba? ustake ncheke!
FF tatizo siyo Raisi gani kafanya nini Kama unavyojitahidi kuonyesha kwa kufananisha (comparative analysis) ila ni katiba iliyopo na njia ya kuipata katiba mpya. Kwa ufahamisho wako wananchi waijua katiba yao kupitia maisha Yao ya kila siku yanayolindwa na sheria na taratibu zinazoletwa na katiba. Kusoma katiba Kama novel(from beginning to the end) hakumpi mwananchi uelewa wa hiyo katiba wala kumfanya aijue. Tafadhali tofauti zako na Nyerere (which in most cases I concur with you) zisikufanye upotoshe agenda Kama ilivyoshushwa na Mzee Mwanakijiji.
 
Hivi wewe ni nini unachokijuwa ni wapi alipokosea kwa kushauriwa? ni wapi alipovunja katiba? hamna cha kusema kwani kila mnalolizuwa yeye yuko makini na anwabwaga vibaya sana. Mlitaka Katiba mpya, kaunda tume tena kwa kupeleka mswada bungeni, sasa hamtaki, mbona hamjielewi mnachokitaka ni nini? shortcut? basi hata hiyo shortcut si uwe na hoja ya msingi, nayo pia hakuna. Mliobaki oohhh "dikteta", mnaujuwa udikteta nyinyi? udikteta tumeachana nao alipoondoka nyerere.

Mimi nachojua ni kuwa wananchi ndio msingi wa mamlakaya nchi kama ilivyoainishwa na ibara ya 8 (1) (a) ya Katiba na sio Rais. Rais anapoteka nyara haki hiyo ya wananchi kwa kuatamia madaraka yote katika mchakato wa kupata katiba mpya, bila kuzingatia maoni ya wananchi na kutetea kwa nguvu zote kitendo chake cha kuatamia madaraka, basi ujue kuna tatizo.

Tunadai sheria hiyo ipunguze madaraka makubwa amabayo Rais kajilimbikizia aelewe hilo. Tunadai kwa sababu ni haki yetu Kikatiba na kisheria.
 
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!




Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.

1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.

Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)



Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".

Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).

NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!

Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

Uhuru wa imani
- Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.


Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
Katika hili la Uhuru wa habari mkuu wangu tumpe sifa JK kusema kweli sii Dikteta hata kidogo isipokuwa katiba ndiyo inamruhusu kufanya mengi mabaya aloyafanya lakini sii Dikteta hata kidogo. Tumempa sisi wenyewe nguvu kubwa sana ambayo haitumii na imefikia tunasema JK ni Mzembe, mpuuzi na kadhalika kwa sababu kama kweli angetaka kuibadilisha nchi hii angeweza kabisa na kwa nia nzuri kabisa.... Lakini kashindwa.

Hata hizo katiba za madikteta kina Ghadaffi vifungu kama hivi vilikuwepo lakini havifuatwi, Marekani wana kila kifungu cha haki kama hizi lakini ukiwaletea za kuleta wanakufuata hadi kwenu iwe mafichoni Torabora au Pakistan..Can you believe yule Mlibya aliyetuhumiwa kuangusha ndege ya Pan nam Lockbie ilikuwa sii kweli kababikiwa na Marekani walikua nyuma ya mpango mzima na ndio maana aliachiwa huru sii kama tulivyojuzwa... Source: Report ya Scotland
 
..aipozikosa zabibu akasema ni mbichi. Huna hoja. Hebu nukuu moasho mmoja hapa kama wewe ni mkweli wa nafsi yako. Ukishindwa basi ujuwe huna ila "dhanna".

Duh umerudi una mihasira yako ya kula Ban na kukosa mshiko wa Magamba sasa kila kitu unapinga na kumshambulia Nyerere na kumsifia huyu aliekutuma, ungakua na busara sana ungebaki at least neutral kuliko kuhamishia matatizo kwa Nyerere, hata inflation ya leo ni Nyerere? Kutokua makini kwa JK na ushabiki wa CCM huuoni pia
 
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!

Hivi hiyo mantiki na falsafa umeitowa wapi? ungekuwa na mantiki na falsafa ungekuwa mshangiliaji? ungekuwa mchezaji, huna kimoja cha manitiki, CCJ i wapi? ilikushinda mantiki au falsafa?

Huo udikteta huujuwi au ni mkali sana kuusikiliza, udikteta tumeachana nao hukoooo kwa Nyerere, ungeongea weye? wapi kwanza, au hukumsikiliza vizuri Kikwete? Daily News? au mzalendo? au Radio Tanzania. Leo unajidai "udikteta" unanchekesha.

Kikwete kafunga kazi kwa kusambaratisha malumbano yasiyo na msingi, Mswaada umepita na unatakiwa usainiwe kabla ya mwaka kwisha na utasainiwa na utafanya kazi na hakuna "shortcut" na hata hiyo "shortcut" si uwe na hoja, unakuja eti mantiki, eti falsafa. Khaaa huna vya kuandika?

Nyuzi ya ngapi hii kuhusu hilohilo moja? mantiki iko wapi? falsafa iko wapi? na hawa moderators wa JF hunishangza pale mmoja wao anapokuwa na "Ruksa" ya kufunguwa nyuzi hata kumi kwa jambo hilohilo moja na haziunganishwi, ni nini kama si kujitafutia "cheap popularity"? wacheni hizo.
 
Babu seya weka hukumu yake hapa na ushahidi uliompelekea kufungwa, yote alikaa akayapika Kikwete? nendeni huko, hamna hoja, tena mahakimu waliotowa hukumu na walioipitia rufaa wasikusikie wanaweza kukuchukulia hatuwa kwani unawabeza wao. Kikwete inamuhusu nini? au na wewe ni mtu wa kusikiliza maneno ya mitaani na si ya mahakamani? halafu unajiita "great thinker"? Unanshangaza sana.
FF in this I agree with you 100%. Having been exposed with facts of the case MNYISANZU was referring I can't stop wondering why people in "vijiwe" are made to believe myths and how lazy they are to find facts. It is a shame. Any one who speak against that judgement might be fitting the profile of a PEDOPHILE
 
..aipozikosa zabibu akasema Siipendi CCM. Hebu nukuu moasho mmoja hapa kama wewe ni mkweli wa nafsi yako Ukishindwa basi ujuwe huna ila "dhanna".

Duh umerudi una mihasira yako ya kula Ban na kukosa EEmshiko wa Magamba sasa kila kitu unapinga na kumshambulia Nyerere na kumsifia huyu aliekutuma, ungakua na busara sana ungebaki at least neutral kuliko kuhamishia matatizo kwa Nyerere, hata inflation ya leo ni Nyerere? Kutokua makini kwa JK na ushabiki wa CCM huuoni pia
 
Mimi nachojua ni kuwa wananchi ndio msingi wa mamlakaya nchi kama ilivyoainishwa na ibara ya 8 (1) (a) ya Katiba na sio Rais. Rais anapoteka nyara haki hiyo ya wananchi kwa kuatamia madaraka yote katika mchakato wa kupata katiba mpya, bila kuzingatia maoni ya wananchi na kutetea kwa nguvu zote kitendo chake cha kuatamia madaraka, basi ujue kuna tatizo.

Tunadai sheria hiyo ipunguze madaraka makubwa amabayo Rais kajilimbikizia aelewe hilo. Tunadai kwa sababu ni haki yetu Kikatiba na kisheria.

Sasa hujuwi kama huo mswaada umepitishwa ili wananchi watoe maoni yao? au hayo maoni utayakusanya vipi? kupitia JF? unanchekesha? piga uwa, huwezi kutetea ujinga. Tume ya kuratibu na kukusanya maoni lazima iwepo, halikwepeki na hiyo hiyo katiba (uliyoonesha kifungu bila kukinukuu) ndiyo inampa Rais uwezo wa kuunda tume, kama walivyounda wa kabla yake. Mlitaka apewe Slaa kuunda tume? basi wangepewa CUF walioanzisha mjadala wa Katiba mpya na wakafikia mpaka kuandika katiba yao wanayoona kuwa ndio sahihi au hilo hulijuwi?
 
Duh umerudi una mihasira yako ya kula Ban na kukosa EEmshiko wa Magamba sasa kila kitu unapinga na kumshambulia Nyerere na kumsifia huyu aliekutuma, ungakua na busara sana ungebaki at least neutral kuliko kuhamishia matatizo kwa Nyerere, hata inflation ya leo ni Nyerere? Kutokua makini kwa JK na ushabiki wa CCM huuoni pia

Rejea hotuba ya Kikwete kwa umakini anauelezea udikteta tulipouwacha, au hata hilo hujalielewa? huna jipya kijana.
 
FF tatizo siyo Raisi gani kafanya nini Kama unavyojitahidi kuonyesha kwa kufananisha (comparative analysis) ila ni katiba iliyopo na njia ya kuipata katiba mpya. Kwa ufahamisho wako wananchi waijua katiba yao kupitia maisha Yao ya kila siku yanayolindwa na sheria na taratibu zinazoletwa na katiba. Kusoma katiba Kama novel(from beginning to the end) hakumpi mwananchi uelewa wa hiyo katiba wala kumfanya aijue. Tafadhali tofauti zako na Nyerere (which in most cases I concur with you) zisikufanye upotoshe agenda Kama ilivyoshushwa na Mzee Mwanakijiji.

Hiyo Katiba imepotoshwa wapi?

Kwani Nyerere hakuwa dikteta? au Kikwete aliposema udikteta tuliuacha huko hukumuelewa kasema nini?

Hiyo katiba ndiyo mambo aliyoyazungumzia KIKWETE inapohusiana na swala liliopo sasa, na kaielezea vilivyo na ni nani mwingine aliyechukuwa jitihada kama hizo kabla yake? ni lini Tanzania Katiba zikachapishwa kwa wingi na kusambazwa kama si wakati wa Kikwete?

Nani asiyejuwa Nyerere alikuwa dikteta? nani asiyejuwa nyerere aliweza na alifanya kuwatia watu ndani bila kuulizwa na mfano mmoja unaojulikana sana ni huo wa Hanga, kwanini tufiche ukweli? hakuna dikteta wa kumuogopa kuwa atakupoteza kwa sasa, lets dare talk openly. Ukweli ubaki kuwa ukweli.
 
Kwa nini linapokuja swala la katiba watu mnazungumzia JK, Slaa, Mbowe, Lipumba, CDM,CUF,NCCR na mnawasahau wananchi wenyewe?

Inaonesha hujamsikiliza Kikwete na wala Bunge lililokuwa linaongelea hayo. Mswaada uliopitishwa ni wa kuwapelekea wananchi huo mjadala wauongelee na tume ni ya kuratibu na kukusanya maoni, mitaka iweje? na hao uliowataja wenye hivyo vyama si wananchi? unanchekesha!
 
Inaonesha hujamsikiliza Kikwete na wala Bunge lililokuwa linaongelea hayo. Mswaada uliopitishwa ni wa kuwapelekea wananchi huo mjadala wauongelee na tume ni ya kuratibu na kukusanya maoni, mitaka iweje? na hao uliowataja wenye hivyo vyama si wananchi? unanchekesha!

Unajua nimegundua kuwa watu wengi humu ni vilaza wa kutupwa na huwa wanafuata mkumbo tu. Inashangaza sana kuona kuwa hadi sasa hivi kuna watu hawaelewi mswada uliopitishwa na bunge unahusu nini. Hali ikiwa hivi humu ndani kwa ma-great thinker je itakuwaje huko nje?
 
1) Hajatowa hadidu za rejea bali kasema wazi kabisa, kuna maadili ambayo tunayo na hayo inapasa yalindwe na kayaelezea ni yepi.

2) Mpaka sasa katiba iliyokuwepo ndiyo inampa mamlaka makubwa, mkitaka Rais apunguziwe madaraka aliyonayo mpeleke maoni na muono wenu kwenye hiyo kamati. Na ndicho kinachofanyika na si kulalama JF. Kikwete hajaandika katiba mpya wala muswada si wa katiba ni wa kusimamia kuandikwa kwa katiba. Hivyo ndiyo ilivyo, mlitaka vipi? asiwepo? mngewashawishi Watanzania wasimpigie kura, hilo mmlishindwa anzeni mbinu nyingine za "shortcut" zimeshtukiwa.

Exactly nilichokieleza ndo unachoendelea kufanya hapa jamvini. Unajitahidi kujadili ambalo si linalozunguka mjadala, (DIVERSIONARY TACTICS) na ndicho alichofanya rais na mnachofanya wewe na watu wengine wa mawazo kama yako.

Haizumngumzwi kama raisi ashiriki kama kiongozi au la. Tunazungumzia namna ya ushiriki wa raisi! Katiba (au niseme Katiba inayotaka kutungwa upya) ni ya wananchi si ya chama wala kundi fulani la watu. Hivyo kumwachia mamlaka makubwa kiasi hicho kwenye huu mchakato rais (kumbuka ye ni binadamu tu kama wengine) sio busara.

Ndio maana watu wanajadili namna bora ya ushirikiswaji wa wananchi kwa upana zaidi!!!!!

Hii mbona inakuwa ngumu sana kueleweka? Ndo kinachonifanya niamini kazi kubwa inafanywa na viongozi wetu ni kuonyesha kinachopiganiwa na makundi mbali mbali(wanaharakati, wasomi, vyama vya siasa na kijamii e.t.c) ni kitu kingine kabisa na uhalisia hence DIVERSIONARY TACTICS kwenye mjadala.
 
Wanabodi, Aliyoyazungumza jana ni ya kwake na ndiyo yanayotoka moyoni mwake, haya ni mambo ya I.Q, kwa waliomsikiliza in between the lines, wanaelewa nazungumzia nini!. Ndio maana kuna wengine wanafanya Ph.D na kui earn na wengine wanasubiri za kupewa, na kupigiwa tarumbeta za shangwe na mapambio, Dr fulani, mpaka kwenye taarifa za habari amepewa title hiyo ya Dr!.Kwa hili la kuitwa Dr silaumu kwa sababu sheria yetu inaruhusu, ndio maana tuna Dr. Kifimbo, Dr. Nguzukululu Jilala (RIP) na , maprofessor kibao, akiwemo Prof. Maji Marefu etc, lakini mtu unapotunukiwa doctorate ya heshima, angalau, ufananie kwa maneno na matendo!.Nimeambiwa UDSM enzi zile, wate wanaongia walikuwa lazima wagraduate, kulikuwa hakuna DISCO, hivyo vilaza wote walikuwa wakipoozwa kwa PASS ya GPA ya 2.0! ili angalauwatoke, na haya ndiyo matokeo!.
Mkuu Pasco naheshimu sana mabandiko yako kama mchambuzi mzuri wa hoja.
Lakini kwa hili hapana, kiongozi mzuri au mbaya hatokani na hayo uliyoyataja hapo juu vinginevyo watu kama akina Mbowe Mnyika, Said Arif nk wasingepewa nafasi kubwa kwa mtazamo wako.
JK kama hafai basi hafai na si kwasababu kapata GPA ndogo au anapewa u dr.
For me this is too lowa bana
 
Back
Top Bottom