Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Kwa mantiki yake uhuru wa kutoa maoni mzuri japokuwa una mipaka (Rejea Ibara ya 18 ya Katiba ya Nchi)!
Hata hivyo tumeona matukio kadhaa ambayo, yumkini yamesababishwa na uhuru tulionao, esp kipindi hiki cha JK, ambayo yameidhalilisha Serikali kwa kiasi kikubwa mpaka heshima ya viongozi wetu iko mashakani:
1. Tulishuhudia nyaraka za siri za Serikali zikizagaa mitandaoni na sehemu nyinginezo.
2. Tumeshuhudia pia msafara wa Rais ukipigwa mawe.
3. Tumeshuhudia vile vile viongozi wetu wakizomewa hadharani, jua limewaka kweupe pee!
4. Tumemshuhudia kiongozi mstaafu Ally Hassan Mwinyi akilambwa kofi hadharani!
5. Tumeshuhudia malumbano ya Muungano, Zanzibar kuwa nchi au la, yasiyokuwa ya kawaida.
6. Tumesikia na kushuhudia malumbano ya kidini (Mambo ya Kadhi, OIC, Nyaraka za Kidini Kuelekea Uchaguzi Mkuu, 2010) yakishika kasi kila uchao, hata Bunge Letu Tukufu lilitekwa na jinamizi hili.
.....nk.
Kwa bahati mbaya sana viongozi wetu, esp JK hakemei vitendo vyote vinavyosababisha migawanyiko! He is simply passive!
Hata hivyo kupitia uhuru huo huo wa kutoa maoni tumeshuhudia yafuatayo:
1. Kashfa nzito zikiibuliwa na kuanikwa hadharani, km Wizi wa Deep Green Finance, Kashfa ya EPA, Mwananchi Gold, nk
2. Tumeshuhudia mawaziri wakijiuzulu kwa kashfa zilizoibuliwa.
3. Tumeshuhudia mawaziri wakiwekwa kiti moto Bungeni isivyo kawaida.
4.
.....nk.
Je, Wapendwa wanaJF, kupitia uhuru huo wa kutoa maoni nchi yetu imeimarika na kuwa kitu kimoja zaidi au tumegawanyika na kukosa mshikamano tuliokuwa nao tangu mwanzo? Nchi kama Somalia sasa hivi haikaliki, imegawanyika vibaya sana, sijui kama imesababishwa na uhuru wa kutoa maoni au la, lakini migawanyiko ndiyo iliyoifikisha hapo ilipo!
Kama mshikamano umepungua, Je, uhuru huo uminywe kidogo? Kwa mwendo huu wa nchi yetu tutafika jamani? Mbona inaonekana kupitia ALAMA ZA NYAKATI kwamba ipo siku tutazichapa? (Mungu apishilie mbali) Naomba tujadili!