Uhuru Publications yapata tuzo, ngao ya ubora

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Saturday, 23 July 2011 18:38 administrator
https://www.jamiiforums.com/index.p...mY2F0aWQ9Nzc6cGVyc29uYWwtdGVjaCZJdGVtaWQ9MTc2https://www.jamiiforums.com/index.p...t=default&page=&option=com_content&Itemid=176

KAMPUNI ya Uhuru Publications Limited (UPL), wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, imeshinda tuzo katika shindano la ubora katika mapato na ukuaji, lililoandaliwa na Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na Kampuni ya Ushauri na Ukaguzi (KPMG), ambalo lilianza Desemba mwaka jana na kuzishirikisha kampuni 200 za hapa nchini, ambapo 100 kati ya hizo zilishinda, huku UPL ikishika nafasi ya 70. Pichani, Mhariri Mtendaji wa UPL, Josiah Mufungo, akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwakilishi wa KPMG, Dk. Boniface Abayo, katika hafla iliyofanyika juzi usiku, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Muhasibu Mkuu wa UPL, Alvera Kabwogi. (Na Mpigapicha Wetu).
 
Is this true? Gazeti la UHURU limeshinda tuzo ya Mapato na Ukuaji?
 
Kwenye mapato inawezekana maana idara zote za serikali zitakuwa zinatoa matangazo kwa uhuru (no choice). Lakini ukuaji na ubora? - nadhani hapa kuna utata mkubwa na inaelekea KPGM walitengeza vegezo (judging criteria) sivyo. Wanaweza kuwa wameangalia ukuwaji kwa maana ya ku-print more copies daily lakini wakumbuke ccm ndiyo yenye serikali na baada ya kuona uhuru na dailynews wanapoteza mvuto wamelazimisha idara zote za serikali lazima zipate nakala na pia lazima wotoe matangazo huko. Lakini kama KPMG wangealia readership kw aku-survey ni watu wangapi wanatoa hela yao mfukuno na kununua uhuru wangepata matekeo tofauti kabisa.

Na ubora unaongelewa hapa ni ubora gani? wa habari za zilizokamilika yaani comprehensive news au habari za kiuchunguzi? Uhuru ni propaganda tool na sijui (statistically) ni watu wangapi wanaamini kuwa habari iliyoandikwa kwenye uhuru ni ya kweli. How do you compare news writing ya Mwanahalisi, Raia Mwema na Uhuru?
 
Back
Top Bottom