Uhuru na Kazi, imetimia miaka 48

Jujuman

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
248
33
Wandugu mnakumbuka kauli mbiu hii "Uhuru na Kazi"? Tunatimiza miaka 48. Ndio kwanza viongozi wetu wanacheza kama watoto wa Darasa la nne vile, kila kitu valuvalu, kila mmoja hajui wajibu wake. Sheria hazilindwi wala hazilindiki kila aliye au aliyewahi kuwa Kiongozi basi yuko juu ya sheria. Wizi na uporaji wa Mali ya Taifa, Rushwa na Maonevu kwa walala hoi ndio Wimbo wa Taifa. Kupotea kwa maadili ya Uongozi ni kama Donda ndugu. Raslimali zimekabidhiwa Wageni.
AMA KWELI UHURU NA KAZI!!( AMA UHURU UNA KAZI??).
 
Jujuman,
Mimi nlichipukia wakati wa kauli hiyo, kabla ya hutuba kiongozi alipaswa kuguta: UHURUUUUUUUUUUUU na Wananchi tuliitikia NA KAZIIIIIIIIIII... Naamini ilikuwa na maana nzuri sana ya kukumbushana kuwa Tumedai UHURU tumepata,Hakuna tena Mkoloni wa Kutuibia au wa kumsingizia, sasa Tufanye KAZI KWA JUHUDI NA MAARIFA tujijengee Nchi yetu.Yaelekea tulianza vizuri na sera za mpango wa Maendeleo wa miaka mitano,Tukawa watendaji na watekelezaji wazuri.Mambo yakaanza kubadilika mara AZIMIO LA ARUSHA lilipoibuka na sera nyingi kwa wakati mmoja na ambazo hazikufanyiwa Maandalizi mema.
UTAIFISHAJI
VIJIJI VYA UJAMAA
MASHIRIKA YA UMMA nk
Kufikia hapa UHURU NA KAZI ikapotea na kuibuka WIMBI LA SIASA. Wimbi hili la siasa likaja na kauli yenye utata kwa maoni yangu: Kiongozi akiguta UHURUUUU wananchi tukiitikia KAZI YA CHAMAAAA. Hapa CHAMA kikashika na kung'ang'ania HATAMU. CHAMA kikaanza kuwaosha Wananchi na kuwageuza Watanzania kuwa WANASIASA Kila mahali pakawa na Tawi la Chama na Wanachama Wapya ni lazima wapite Darasani WAKALISHWE FIKRA ZA MWENYEKITI. Kuna mazuri mengi yaliyofanyika ndani ya miaka 48 lakini mengi ya hayo YAMEFAIDISHA WACHACHE KATIKA JAMII. Nafuu iko Mijini, VIJIJINI HALI YA WANANCHI HUKO NI HOI bin TAABANI.
IKIWA MIJI inakosa UMEME inakosa MAJI Leo 48 YEARS ON!! ni vipi itakuwa Vijijini?
MOJA ZURI ni kuwa Watanzania WE CAN TALK tena LOURD AND CLEAR kwa sababu wote tumegeuzwa WANASIASA: USANII na LONGOLONGO Kila MTZ yuko Tayari. JE VIONGOZI WATAKUWAJE Wakati wana Maslahi ya kulinda na kutetea?
 
Back
Top Bottom