UHURU lataja majina ya Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa

MKL

Senior Member
Mar 2, 2012
126
77
Kichwa cha habari kinasema "Wabunge Kamati ya Nishati Wakufuru"

Ndani yake Uhuru Kongwe la CCM linasema wahusika na kamati hii ni matajiri wa kufa mtu
1. Yupo anayemiliki magorofa
2. Wengine magari ya kukodi, Vituo vya Petroli
3. Wapo pia wenye Zabni za Mafuta migodini
4. Wengine wana makampuni ya tours

Nalinauliza wamezipataje mali hizi kwani wengi wao wameingia bungeni Juzi tuu hata awamu moja ya miaka 5 bado hawajamaliza.

Uhuru limekuwa ni gazeti la kwanza TZ wabunge kuwataja kwa majina wabunge wanaounda kamati hiyo kuwa ni:


  1. Selemani Zedi (MWenyekiti)
  2. Diana Chilolo (makamu Mw/kiti)
  3. Haji Khamisi
  4. Catherini Magige
  5. Abia Nyabakari
  6. Charles Mwijage
  7. Yusuph Nassir
  8. Christopher Ole Sendeka
  9. Dr. Festus Limbu
  10. Eng. Athuman Mfutakamba
  11. Lucy Mayenga
  12. Josephine Changula
  13. Mwanamrisho Taratibu
  14. Suleimani Nchambi
  15. Ally Mbarouk Salim
  16. Vicky Kamata
  17. Kisyeri Chambiri
  18. Sarah Msafiri
  19. Munde Tambwe
  20. John Mnyika
  21. Mariam Kisangi

Haya sasa Juzi Tundu Lissu alitaja baadhi ya wabunge wanaoihujumu Tanesco la jana alitakiwa kutoa maelezo kwenye kamati inaofuatilia sakata hili tuone Mbivu na mbichi kati ya hawa nani hasa inaihujumu Tanesco?

Kama Uhuru Kongwe la Chama chama cha CCM limechoka nalo kuwaficha wanaoihujumu Tanesco najiuliza habari hii nayo si ni kama ile tuu ililoliponza MWanahalisi? BAsi nalo Lifungiwe.


Source ni UHURU leo 01/08/2012 page 1-4
 
Mbona limetaja kwa Mafumbo mafumbo tu! Zaidi zaidi limewataja tu Wajumbe waliokuwa kwenye kamati hiyo ambao kila mtu anawafahamu.

Tulitaka kama angemtaja kwa mfano anayemiliki Maghorofa ni Ole Sendeka, Au anayemiliki Vituo vya mafuta vyenye kashfa ni Mh. Nchambi N.K
 
Hamna kitu zaidi ya hizo ngonjera tu za gazeti hilo na uliyeleta huo uzi nawe mtupu.Hiyo ni sawa na ukutapo mtu anapigwa huku wakisema mwizi ukashiriki, ukiuzwa huyo unayempiga kaiba nini?Nyinyiemu dhaifu wote ndo hao hao, ebu tujuze yale mapendekezo ya kamati ya bunge juu ya richmond yametekelezwa kiasi gani na serikali zaidi ya huo ni upepo tu?
 
MKL Hivi ni gazeti tu ndo linalofungiwa, Mbunge hawezi kufukuzwa Ubunge kwa kusema umbea wakaanza na LISSU?
 
Last edited by a moderator:
GAzeti la kwanza kutaja wajumbe wa kamati ya nishati na madini!!!

Aseee!!!
 
hivi gazeti bado lipo na linawateja na wasomaji wengi kweli?isiwe wanauziana wana chama wao kwa wao
 
nalikumbuka mwanahalisi lingeweka wazi kila kitu kwa kila mtu

nalo hili litajiita gazeti la uchunguzi

n.b:
j hando wa wafu radio kashadadia sana oooohhh mbunge kijana mdogo sana anambwembwe hajamaliiza hata kipindi kimoja anautajuri mkubwa......nikajua jungu hili linamuhusu Mnyika

Da nina iman kubwa sana na Mnyika Kuliko Zzk
 
Gazeti la Uhuru hata ukinifungia maandazi sikubali na siwezi kula hayo maandazi, sembuse kubwa zima unatuletea Source kutoka Gazeti la Uhuru? na afadhali hata Magazeti ya Shigongo kuliko Uhuru.
 
Mbona kama vile limetaja majina ya wana kamati? au labda hujaweka habari nzima Mpwa
 
Naomba kujulishwa utajiri wa mwenyekiti wa kamati mstaafu au aliyeachia madaraka J Makamba, kwani huyu mpya kaingia mwezi wa 6 tu !

Uhuru nadhani zaidi ya kununuliwa 'kilazima' serikalini haliuziki zaidi ya hapo.
 
Mtoa mada asitutoe kwenye issue ya ufisadi wa wabunge wa kamati ya nishati na madini ambayo ndiyo mada kwa sasa. Msitu-derail for your own or your party's benefit. Halafu ni ukomavu kuzungumzia masuala, issues siyo watu! How is this poll going to help us in freeing ourselves from these mafisadi waliotuzunguka kona zote jamani! Tukue, tukomae tusiendeshwe na hoja toto.
 
Back
Top Bottom