Uhuru Heights jengo jipya linaloendelea kukua

i411

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
906
290
found this from another forum on the net….
Swali langu watanzania tutaweza kuafford haya maisha ya life style hii. Au mafisadi wa ndani na wa kutoka nchi jingine wanajijengea, mimi nita windowshop hakuna neno,
yangu hoja

DSC03060.jpg
 
Last edited by a moderator:
Watanzania walio wengi hata kama hawewezi lifestyle hii, lakini bado itakua na mchango angalau kidogo kwa watanzania wengine, kwanza kabisa kujenga tuu haya majengo yanachangia uchumi wa tanzania GDP kwa 13% kutokana na data zilizotolewa, pia hata kama ni mafisadi sioni mbaaya wakizitumia hela wanazoiba na kuzizungushia humuhumu ndani ya nchi badala ya kwenda kuzificha kwenya mabenki ya nje ya nchi na kuzineemesha benki hizo, pia kuna biashara nyingi sana zinakua zinasababishwa na hii miradi ambayo biashara hizo zinanufaisha watanzania wengi pia, kuanzia muuza maji mkoroga zege atakayefanya usafi nk, labda kama wafanyakazi hawa watakua wa nchi nyingine hapo inakua noma lakini, bado hata hao wa nje wakija nchini hawaji bure, kuanzia visa, malazi na chakula lazima watanunua vya tanzania tuu, labda kama wachina wanakuja na tambi zao zilizokaushwa du, hapo watakua wametubania, pia katika majengo haya kutakua na shopping malls, sinema, hotel, nk ambavyo vitasaidia kuwachuna watalii, waache hela nyingi nchini, kuliko akija anaenda kuangalia wanyama, akifika dar hakuan eneo lolote la kisasa la kujibududishia, basi hawezi kutumia vizuri, hapo nina wasiwasi kama wamiliki wa hizi hotel na maeneo yote ya biashara yanamilikiwa na wageni halafu wanachukua kila walichokichuma pamoja na msamaha wa kodi na kula kona, hapo tutakua tumeuwawa, ila nina uhakika, yana manufaa kwa tanzania angalau kidogo, tutafika tuu, pia majengo haya yatahitaji maji ya dawasco, umeme wa twiga mzembe(TANESCO) nk, naomba kuishia hapa ntaendelea kutokana na maoni ya wadau wengine,
hiyo picha pia inapatikana hapa, kuanzia jiwe la msingi mpaka lilipo fikia http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=1086599
 
hivi sewage system iliyo dar city centre, minara yote inayojengwa na iliyopo ikapata wapangaji na angalau 70% yao wakaingia chooni kujisaidia haja kubwa baada ya luch, uchafu/m.avi hayatafumukia Ikulu? mfano hai uliopo kwa sasa ni mafuta house; mpaka sasa mfumo wake wa maji taka ni mgogoro mtupu, siku zingine ukipita pale nje unakuta watu wanapakua ma.vi kwa koleo kwenye inspection chambers pale nje barabarani.
 
hapo sasa, wabongo hawapendi kuchukua tahadhari na kufanya vitu kwa malengo, wanasubiri yakifika shingoni ndio wanaanza kutatua, hii inatumia hela nyingi sana, sasa baada ya jiji kujaa harufu, ndio wataamka, na kuanza kuchimba hiyo mifereji itagharimu vitu vingi kwa kuwa vimeshajengwa, mfano barabara, wengine wamechimba nyaya zao chini, hapo foleni bado tatizo, ni vita tupu itakua hapo jijini, kuna majengo kama karibia ishirini yatachipua humo katikati ya jiji ,na hao wanaojiita jiji, sijui mamayor, ni aibu tupu, sijui hata pia wanajitambulishaga kma wao ni viongozi wa jiji? tutafika tuu, kuna jiji llinaitwa a city on flames, maana kila siku ni moto, na moto unaweza kuwa mkubwa kulko jengo, teh teh
 
Tatizo ni badget zipo tight viongozi wanapewa budget tokea wamekabiziwa haitoshi kabisaa na bado kunamishahara ya wafanyakazi wake ya miezi kadhaa haijalipwa. Matokeo yake wanakuwa wanafanya vile vitu vya emergency tuu na mambo mengine unaambiwa kesho tuuu mpaka itokee emergency huo ndo uchumi wetu.
 
hivi sewage system iliyo dar city centre, minara yote inayojengwa na iliyopo ikapata wapangaji na angalau 70% yao wakaingia chooni kujisaidia haja kubwa baada ya luch, uchafu/m.avi hayatafumukia Ikulu? mfano hai uliopo kwa sasa ni mafuta house; mpaka sasa mfumo wake wa maji taka ni mgogoro mtupu, siku zingine ukipita pale nje unakuta watu wanapakua ma.vi kwa koleo kwenye inspection chambers pale nje barabarani.

Wapangaji na wageni wao wawekewe diet ya kula mchana kwenye mkataba wakiwa ofisini kuepuka madhara hayo!!!!!!
 
Swali langu watanzania tutaweza kuafford haya maisha ya life style hii. QUOTE]

Usiseme watanzania sema wewe mtanzania utamudu?

Miye sitamudu nimezoea kwenda gengeni kwa mangi bei ni maelewano sukari,chumvi tunapimiana hela yako too hata vijiko viwili ukitaka mnaelewana bei. Unanunua kadiri ya uwezo wako huko kwingine nasikia unaitaji credit card na sijui nitapata lini hiyo
 
NDINDA, ulichosema sawa kabisa tusiewe na chuki za kijinga , maendeleo huja kutokana na watu, tusiwe na wivu usiokuwa na maana hatutofika!
 
Proto ya ukweli, tatizo tu implementation huwa haziwi up to the standards especially kunapokuwa na mkono wa mbongo.
 
Nadhani umefika muda wa kujifunza, haiwezekani kuimba kila siku utandawazi lakini hatujui nini maana ya utandawazi, ili kufiti katika utandawazi ni lazima tujue tunatakiwa kufanya nini, ni lini na sisi makampuni yetu yataenda nje ya nchi kujenga majengo barabara na vitu vingine kwa kushinda tender kama makampuni mengine yanavyoshinda tender za bongo? ni kweli sisi hatujui kufanya chochote?
halafu maeneo mengine kama utalii, ni muhimu katika nchi yetu, hao custmer care na watu wa uwanja wa ndege, du watu wana nyodo wale, yaani utalii ni hospitality industry, ni lazima mteja awe malkia hata kama anakutukana ni lazima utabasamu, hata kama ni la bandia ili mradi tabasamu na uwe mpole, kwani katika africa kuna nchi kama 10 zote zina bidhaa zinafanana za utalii, wanyama, milima, maji ya bahari na fukwe zake, utamaduni, nk, hapa mtalii ana eneo kubwa la kuchagua, atatafuta wapi akienda anaonekana mtu muhimu na anahudumiwa vizuri, hapo sasa ni ushindani, wobongo kwa nyodo tutawakosa wengi.
kudadadeki pale uwanja wa ndege nilibananishwa pamoja na kusema mi mwanafunzi sina kitu wakasema wanafunzi ndio wenye hela, wakafungua sanduku langu na kuanza kupekua yaaani bahati nzuri mmoja aliniuliza unakaa wapi ndio ikawa bahati yangu, baada ya kusema natokea kipawa basi walianza kunicheka wakisema haujui kama wamebomoa? duh, hapo basi nikapata mwanya wa kutochakachuliwa.
 
Watanzania walio wengi hata kama hawewezi lifestyle hii, lakini bado itakua na mchango angalau kidogo kwa watanzania wengine, kwanza kabisa kujenga tuu haya majengo yanachangia uchumi wa tanzania GDP kwa 13% kutokana na data zilizotolewa, pia hata kama ni mafisadi sioni mbaaya wakizitumia hela wanazoiba na kuzizungushia humuhumu ndani ya nchi badala ya kwenda kuzificha kwenya mabenki ya nje ya nchi na kuzineemesha benki hizo, pia kuna biashara nyingi sana zinakua zinasababishwa na hii miradi ambayo biashara hizo zinanufaisha watanzania wengi pia, kuanzia muuza maji mkoroga zege atakayefanya usafi nk, labda kama wafanyakazi hawa watakua wa nchi nyingine hapo inakua noma lakini, bado hata hao wa nje wakija nchini hawaji bure, kuanzia visa, malazi na chakula lazima watanunua vya tanzania tuu, labda kama wachina wanakuja na tambi zao zilizokaushwa du, hapo watakua wametubania, pia katika majengo haya kutakua na shopping malls, sinema, hotel, nk ambavyo vitasaidia kuwachuna watalii, waache hela nyingi nchini, kuliko akija anaenda kuangalia wanyama, akifika dar hakuan eneo lolote la kisasa la kujibududishia, basi hawezi kutumia vizuri, hapo nina wasiwasi kama wamiliki wa hizi hotel na maeneo yote ya biashara yanamilikiwa na wageni halafu wanachukua kila walichokichuma pamoja na msamaha wa kodi na kula kona, hapo tutakua tumeuwawa, ila nina uhakika, yana manufaa kwa tanzania angalau kidogo, tutafika tuu, pia majengo haya yatahitaji maji ya dawasco, umeme wa twiga mzembe(TANESCO) nk, naomba kuishia hapa ntaendelea kutokana na maoni ya wadau wengine,
hiyo picha pia inapatikana hapa, kuanzia jiwe la msingi mpaka lilipo fikia http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=1086599
Nimeukubali mchango wako
 
Hili jengo lina matatizo makubwa sana katika madirisha.Zege imetumika sana na kuacha nafasi za madirisha ndogo sana badala ya kutumia steel na glass zaidi.Wangejenga jengo dogo lenye mandhari nzuri inside ambalo linaweza kushindana na na majengo mengine ya east africa, kuliko kukimbilia ku break record lakini ndani linakuwa kama warehouse.

Angalia jengo ya kisasa linavyokuwa

construction-site.jpg

http://www.youtube.com/watch?v=r9rXH11y4kE
 
jengo lipo poa tu, hakuna matatizo yoyote, hilo jengo kuanzia gorofa ya kwanza mpaka ya kumi ni paking
 
Hili jengo lina matatizo makubwa sana katika madirisha.Zege imetumika sana na kuacha nafasi za madirisha ndogo sana badala ya kutumia steel na glass zaidi.Wangejenga jengo dogo lenye mandhari nzuri inside ambalo linaweza kushindana na na majengo mengine ya east africa, kuliko kukimbilia ku break record lakini ndani linakuwa kama warehouse.

Angalia jengo ya kisasa linavyokuwa

construction-site.jpg

YouTube - Discovery Videos: Build It Bigger: Trump Tower Animation 3

hili jengo lilikua liwe refu kuliko yote tanzania, na haikua na maana ya kuvunja record, kuna vitu vikali vinakuja virefu kuliko hivi, kimoja kinaitwa RITA tower ghorofa 30 pale karibu na elite tower na nmb house au karibu na club bilcanas, pia kuna majengo pacha ghorof 35 plae karibu na jm mall, pia kule maeneo ya kijitonyama kuna LAPF millenium tower 2 gorofa zaidi ya 28, hii uhuru heights ina 27 na itaongoza kwa muda mfupi, jengo hili halina tatizo lolote, lasivyo lingeshavunjwa, na hao contractor hawaoni aibu kujenga jengo bovu au lisiloendana na mpango uliokubalika , angalia jengo hili na taarifa zake vizuri hapa, utaelewa zaidi http://www.skyscrapercity.com/newreply.php?do=newreply&p=53525351

HABARI - UHURU HEIGHTS KUKWANGUA ANGA ZA DAR ES SALAAM
 
jamani jengo kuwa refuu zaidi ni investment siyo tuu kuvunja record hapo mjini real estate ni ghali sana na kila mwaka nafasi zinaendelea kuwa expensive. so the more gorofa ukijenga ndo unapata good returns of your mtaji.
 
Back
Top Bottom