UHANITHI baada ya Kitovu cha Mtoto kukatika na kudondokea Sehemu zake za Siri

Kwa kuanzia....Imani hii si ya kweli, japo nachelea kuiita potofu (kiSwahili kigumu sometimes). Siiti potofu kwa sababu haina hasara kwa mtoto, bali ina faida!

Dhana hii ilianza zamani za mabibi zetu walipogundua kuwa kama hutunzi vyema kitovu cha mtoto mchanga basi mtoto huyo ataugua na kufariki. Na hilo ni kweli, kwani mtoto atapata 'umbilical infection/sepsis' na kama hatapata matibabu ya haraka na stahiki atafariki kwa 'septicaemia'.

Kwa hiyo imani hiyo ilitungwa ili wamama wawe makini kuchunga kitovu kisiangukie uume mtoto akawa h*nithi, wakati huo huo mama atachunga kitovu kisipate maambukizi. Hivyo japo si kweli kwamba mtoto akiangukiwa kitovu anakuwa h*nithi, lakini uongo huo una faida kwa mtoto kuangaliwa vyema kitovu chake.
nimeamini hili
 
Hivi mpaka tudanganywe ndio tuwe makini na watoto wetu?

Sioni mantiki hata moja ya kumwambia mtu mzima mwenye mtoto uongo ili amtunze mwanawe vyema.
 
Na uzee wangu wote, ndio mara ya kwanza naisikia hii kitu, siikubali wala siiamini.
 
Kwa kuanzia....Imani hii si ya kweli, japo nachelea kuiita potofu (kiSwahili kigumu sometimes). Siiti potofu kwa sababu haina hasara kwa mtoto, bali ina faida!

Dhana hii ilianza zamani za mabibi zetu walipogundua kuwa kama hutunzi vyema kitovu cha mtoto mchanga basi mtoto huyo ataugua na kufariki. Na hilo ni kweli, kwani mtoto atapata 'umbilical infection/sepsis' na kama hatapata matibabu ya haraka na stahiki atafariki kwa 'septicaemia'.

Kwa hiyo imani hiyo ilitungwa ili wamama wawe makini kuchunga kitovu kisiangukie uume mtoto akawa h*nithi, wakati huo huo mama atachunga kitovu kisipate maambukizi. Hivyo japo si kweli kwamba mtoto akiangukiwa kitovu anakuwa h*nithi, lakini uongo huo una faida kwa mtoto kuangaliwa vyema kitovu chake.

Mkuu japo unasema ni potofu lakini ina faida kwa mtoto hapo nashinwa kukubali moja kwa moja. Nimekuta mtu kafunga kitovu cha mtoto wake na kamba halafu Kamba ikazungushiwa kiunoni na wengine pia naskia huzungushia kamba shingoni ili kuhakikisha kwamba hakidondoki. Sasa hii nayo si inaweza leta madhara badala ya faida? Anyway nashukuru kwa kuniambia ni imani potofu japo wengi wetu wanaamini sana hili. Na Kama hujui utasikia akina mama wanamsema mwanamke kwamba hajafundwa!!!
 
sawa na tamthilia za kusadikika. Sawa na kusema ukimruka mtoto atakuwa hawi mrefu.
 
Pamoja kwamba ni imani potofu kwa mujibu wa wataalam nimemshuhudia kijana alieathirika na dhana hii kwenye kuhangaikia tiba alishauriwa aanze kufanya mapenzi na mama yake mzazi.

Na kijana alikuwa akimwazia mama yake kwa matamanio uume ulikuwa unasimama na akifikiria wengine husinyaa kosa alilolifanya hakumshirikisha mama yake .

Alifanya jaribio la kumbaka mama yake akiwa bafuni anaoga aliingia bafuni mama yake akiwa na mapovu usoni na anakiri uume ulikuwa umesimama kisawasawa lakini zoezi lilishindikana baada ya mama kupiga kelele na majirani kujaa. Hivi sasa huyu kijana ni mwendawazimu.
 
Hivi mpaka tudanganywe ndio tuwe makini na watoto wetu?

Sioni mantiki hata moja ya kumwambia mtu mzima mwenye mtoto uongo ili amtunze mwanawe vyema.

zamani si walikuwa wanasema mtoto akiongea wakati wa kula atakufa? Kumbe walijua njia ya hewa na chakula haziko stable ko mtoto anaweza aspirate chakula na kusuffocate.
 
Madokta na wataalam wa haya mambo ya kijamii naomba mnipe mawazo yenu kuhusu hili swala ambalo binafsi haliniingii akilini. Nimepita mikoa mingi hapa Tz na nimekutana na hii dhana ya kuwa kitovu cha mtoto kinapokatika na kudondokea sehem yake ya siri basi automatically huyu mtoto wa kiume anakuwa ******* na Kama ni wa kike basi hatakuwa na hisia za mapenzi na hatazaa. Je wataalam wa JF mnalizungumziaje hili na kitaalam kitovu kinauhusiano gani na sehemu za Siri za mtoto?

ONE LOVE

Umesoma science au arts? Simple biology negates such a contention!!!
 
Hivi mpaka tudanganywe ndio tuwe makini na watoto wetu?

Sioni mantiki hata moja ya kumwambia mtu mzima mwenye mtoto uongo ili amtunze mwanawe vyema.
Shida ilikuwa ni elimu...watu walielimishwa kwa namna hii.. Nikiwa mtoto mama yangu alinieleza nikijisaidia mtoni yeye atasombwa na maji...au watu wasiende ilipo pump ya maji kuna joka mla watu..kuna faida ktk imani hizi leo tu mashahidi jinsi mali/mazingira yanavyoharibiwa..
 
This is just myth, hazina tofauti na zile zilizokuwa zinawakataza akina mama wajawazito kutokula baadhi ya vyakula japokuwa vina nutrients muhimu sana. Kama ingekuwa kweli basi monitoring yake ingekuwa ya uhakika. Sababu za uhanithi zipo na sijawahi kuiona hii.
 
Hiyo si kweli kisayansi. Hiyo ilifanywa kimila hapo zamani na nia kubwa haswa ilikuwa ya kisaikolojia ili kuwasaidia wamama kukiangalia kitovu kwa uangalizi mkubwa ili kisipate infection kwani zamani kulikuwa hakuna disinfection za kitaalamu kama sasa hivi. Nafikiri ndo ilikuwa nia yao haswa wamama kuhakikisha kitofu kinakauka na wanahakikisha kinaanguka salama na wamekiona kilivyoanguka na kilipoangukia.
 
Mimi japokuwa nimesoma (si daktari lakini) sidharau kabisa imani za kijadi as long as si uchawi na azina madhara.

Kwa logic ndogo tu...kama wazee wanasema kitovu kinamadhara na wataalamu wanasema hakina nani wa kumuamini??? Unless hao wataalamu wanambie sababu za kitaalamu zinazomfanya mwanaume awe 'si ridhiki' ntaendelea kuamini knowledge ya mababu zetu ukizingatia hao wataalamu wenyewe hawana majibu kwa kila matatizo ya jamii.

Hii ina uhusiano na mtoto kutahiriwa akiwa mchanga... niliuliza madaktari zaidi ya mmoja majibu yao yakawa "hakuna madhara" bila maelezo ya kitaalamu...nili conclude kuwa hawana uhakika ila hawataki kunambia kuwa hatujuhi. Kuna mmoja yeye ndio alinifanya nigairi kwani alisema hakuna madhara ila wakwangu nasubirigi wakue.

Sasa kama hakuna jibu la kitaalamu kwa nini tusi opt for jibu la kijadi??

Mfano mwingine nilikuwa naongea na rafiki yangu amekaa sana Zanzibar either Unguja au Pemba sina uhakika. Alinambia watu wa huko wanawachanja watoto wao kwenye mdudu ndio maana wana mitarimbo kama mkono wa mtoto mchanga? Nilibaki nacheka lakini nilizidi kuamini kuwa kuna lots of local knowledges ambazo wadhungu hawazijuhi na sisi tunazidharau kwa kuwa si za mdhungu.
 
nyumba kubwa asante sana kwa kutambua mchango wa wajadi wetu.

Mie mwenyewe sijui maelezo ila siwezi fanyia majaribio kwa mwanangu, naheshimu wajadi.

Umeshasikia kuwa mama mjamzito anakatazwa kukaa mlangoni? Kisa mtoto atakataa kutoka?

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anabisha anasema haoni mantiki na alikuwa mjamzito, weee, siku ya kujifungua imefika mbona mtoto alikataa kutoka bila sababu ya maana akaishia theatre.

Kuanzia siku hiyo sipuuzi wajadi kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hapo umeniongezea ujuzi. Nilikuwa sijasikia ya kukaa mlangoni.

Ila mtoto wangu wa kwanza nilijifungua kawaida wa pili kisu cha kutotarajia.

Doctor mwenyewe alishangaa maana alisema njia iko fresh mtot alishageuka siku nyingi ila dogo kagoma kushuka. Isije kuwa nilikuwa nakaa mlangoni. Sijawahi sikia hili; hata mama yangu alishangaa akasema uzazi wa siku hizi hautabiliki kumbe kuna tusivyovijua. Ntawaelimishe wazazi wajao maana mi nshamaliza. Lol.

nyumba kubwa asante sana kwa kutambua mchango wa wajadi wetu.

Mie mwenyewe sijui maelezo ila siwezi fanyia majaribio kwa mwanangu, naheshimu wajadi.

Umeshasikia kuwa mama mjamzito anakatazwa kukaa mlangoni? Kisa mtoto atakataa kutoka?

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anabisha anasema haoni mantiki na alikuwa mjamzito, weee, siku ya kujifungua imefika mbona mtoto alikataa kutoka bila sababu ya maana akaishia theatre.

Kuanzia siku hiyo sipuuzi wajadi kabisa.
 
Habari wadau,

Leo nikukumbuka usemi kuwa eti kitovu cha mtoto mchanga kikidondokea uke wake basi kama ni KE hatozaa, kama ni ME uume utakuwa hausimami!

1. Je ni kweli?

2. Kama ni kweli naomba kujuzwa kitaalam.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom