Uhamiaji yaomba wananchi kuwataja Wahamiaji haramu nchini

emmanuel1976

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
301
79
Idara ya uhamiaji katika taarifa ya habari ya TBC 1 usiku huu wamekiri kwamba kuna wahamiaji haramu kibao nchini wasio na vibali na wamewaomba wananchi kusaidia kuwataja.

Kilichonishangaza, mie binafsi nilisha m-report mtu ambaye ni mkenya aliye ingia nchini bila vibali na anafanya kazi nchini bila working permit, kanunua ardhi kama mtanzania, ana passport ya Tanzania na cheti cha kuzaliwa hapa nchini na anacho kipande cha Kenya.

Huyu amekuja nchini miaka ya 98 akiwa na umri wa miaka kama 26 hivi. Amewasumbua sana wa TZ. Nilipo ripot hakuna aliyefuatilia..nilieleza mpaka nyumbani kwao ni wapi na wazazi wake wanakaa wapi. Mpaka sasa anadunda tu na shughuli zake huku akiwadharau wa TZ.

Swali langu ni hili..je wamebadilika kiasi kwamba tukipeleka majina ya wahamiaji haramu yatafanyiwa kazi?
 
hii serikali inakuwa kama haina mwenyewe,watanzania tusipoamua na kuchukua hatua tutabaki kama tulivyo
 
Idara ya uhamiaji katika taarifa ya habari ya TBC 1usiku huu wamekiri kwamba kuna wahamiaji haramu kibao nchini wasio na vibali na wamewaomba wananchi kusaidia kuwataja. Kilichonishangaza, mie binafsi nilisha m-report mtu ambaye ni mkenya aliye ingia nchini bila vibali na anafanya kazi nchini bila working permit, kanunua ardhi kama mtanzania, ana passport ya Tanzania na cheti cha kuzaliwa hapa nchini na anacho kipande cha Kenya.

Huyu amekuja nchini miaka ya 98 akiwa na umri wa miaka kama 26 hivi. Amewasumbua sana wa TZ. Nilipo ripot hakuna aliyefuatilia..nilieleza mpaka nyumbani kwao ni wapi na wazazi wake wanakaa wapi. Mpaka sasa anadunda tu na shughuli zake huku akiwadharau wa TZ.

Swali langu ni hili..je wamebadilika kiasi kwamba tukipeleka majina ya wahamiaji haramu yatafanyiwa kazi?

Unaweza kuiweka hiyo kesi hapa kama ulivyo iweka huko ? JF ukisha weka kitu kesho utasikia mengi na serikali ita ingia kati.Kwa heshima zote hamishia hapa hiyo kesi tuta anzia hapa hapa .
 
Wahamiaji hapa TZ wako kibao hasa kutoka Burundi, DRC, Rwanda, Kenya na Uganda. Mikoa iliyoathirika sana ni Kigoma, Rukwa, Kagera, Shinyanga, Dar es Salaam n.k. Kigoma pekee inakadiriwa kuwa na wahamiaji zaidi ya 25,000. Uhamiaji wapo sijui wanafanya kazi gani.
 
Hawa uhamiaji wasitufanye watanzania mazuzu, wageni wengi wanawatambua na ni moja ya miradi yao ya kujipatia pesa! Tumekwisha sikia na kuona mara nyingi sana kwenye TV wananchi wa Ngara wakilalamikia wahamiaji haramu walivyovamia mapori ya misitu ya nchi hii na kuuwa wananchi. Viongozi wanawalinda kwa vile ni vitega uchumi vyao.

Tembelea wilaya za Ngara, Tarime, Geita hata ndani ya CCM wamejificha humo. Uhamiaji hawana dhamira ya dhati kama wanavyosema wanasiasa wakuu kuwa, kama RACHEL kala rushwa LETE USHAHIDI!
 
Kuna wimbi la Wahindi kutoka Pakistan.India na Sri Lanka ambao huletwa kwa mamia kila mwezi na baada ya kujifunza kiswahili kidogo hupata kazi kama watanzania.Wahindi waliokuwa wanaishi hapa miaka ya kabla ya 1990 wengi wamehamia Ulaya,Marekani/canada na Australia na kuwaachia biashara zao wahindi hawa wapya ambao huwatumia faida zao huko.Usishangae kwenda kwenye duka au kiwanda ukakuta muhindi anadai ni mtanzania lakini kiswahili chenyewe cha salamu tu.
 
Mimi Huwa kusema kweli sipendi wageni hasa wakenya lakini uhamiaji ndio wanotuletea matatizo humu nchi siku tukichoka tutaanza kuwachoma moto wageni kama walivyofanya Afrika Kusini
 
Kuna watu naweza wataja hapa lakini je nani atawarudisha kwao? Hilo nalo limeishinda serikali ya ccm maskini? wanalilia posho na mashangingi tu. Nani atatusaidia, nchi yetu imekuwa shamba la bibi.
 
Ni mafala tuu wasio na kazi ndio wanaweza kuwa na wasiwasi na wahamiaji,uhamiaji ni kitu kizuri sana dunia nzima na nchi nyingi zilizoendelea zimejengwa na wahamiaji,Tanzania haina tatizo la uhamiaji acheni hao wahamiaji waje labda wanaweza kuwafundisha kuwa serious na maisha.
 
Una akili timamu wewe? hawa wanaitwa wahamiaji haramu, maanake hawana sifa ya uhamiaji, wanakuwaje wazuri? hivi wewe unaweza hamia kenya na uishi bila vibali? ama nawe ni mhamiaji haramu? nchi zote duniani sasa zinarudisha wahamiaji haramu wewe unasema ni uhamiaji haramu ni kitu kizuri! Hawa wanatufundishaje kuwa serious na maisha?
 
Kuna tetesi kuwa baadhi ya viongozi wanasemekana sio watanzania na ndio maana hawana uchungu na hii nchi na wako tayari kuona maamuzi yanapitishwa kwa masilahi yao binafsi.

Nawakilisha.
 
Kuna tetesi kuwa baadhi ya viongozi wanasemekana sio watanzania na ndio maana hawana uchungu na hii nchi na wako tayari kuona maamuzi yanapitishwa kwa masilahi yao binafsi.

Nawakilisha.

Ungeanza kututajia japo mmoja ingekuwa vema.
Anyway mi naanza:
Mustafa Mkulo ni m-Malawi.
 
  • Thanks
Reactions: PSM
Muanzisha hoja tungependa utujuluishe wewe unatoka nchi gani kwakua hii nchi hatuna ukabila!
 
Muanzisha hoja tungependa utujuluishe wewe unatoka nchi gani kwakua hii nchi hatuna ukabila!

ndugu yangu ndalo jifunze kusoma vizuri na kuelewa kabla hujaandika nimezungumzia Utanzania ukabila umetoka wapi. inaelekea mitihani mingi ulifeli si kwa kutofahamu bali kwa kutoelewa maswali
 
Back
Top Bottom