Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Status
Not open for further replies.
Aisee hii ndo aina ya viongozi ndani ya CCM. Kwa hali hili kwa nini chama hiki kisife?
 
Hayo mamilioni kapewa nani au na wewe ni beneficiary?

Mkuu Maundumula sinufaiki na hata sh 1 kutoka kwa Bashe.Ninachouliza ni chanzo kipi cha mapato kinachompatia mamilioni kuendesha shughuli za siasa? Ukizingatia zoezi la kumwangusha Lucas Seleli 2010 alitumia zaidi ya 400m kwenye kura za maoni. Hii wakati mwingine ndo maana watu wanahoji kuna nini nyuma ya pazia.Ushauri wangu kama uraia wake una utata kiasi hicho aurekebishe ili asiendelee kukumbwa na kashfa hii mara kwa mara.
 
...mmmh!...tutasikia mengi kabla ya 2015...mleta uzi tunaomba usiishie kwa Bashe,emu sogea mbele kidogo hadi Tabora mjini kuna msomali mwingine kajificha hapo...
 
Acha wivu kwani uraia wako unakusaidia nini? Acha naye ale hata wazawa ni fisi tu. Pengine ana roho nzuri huwezi jua.
 
Imekuwa kasumba sasa. Oh wakenya wanamaliza kazi zetu. Uraia sasa hivi si kitu cha kutamba nacho. Ukiwa na mshiko unaamua uwe raia wa wapi. Watz tuache ushamba. Mbona wageni wanakula maisha kuliko wenyeji?
 
Nendeni kwanza mkamchimbe Alhaj Ismail Aden Rage na Abdulrahman Kinana kabla hamjakuja kwa Bashe!
 
hey!hii inanikumbusha enzi zile za biashara haramu ya pembe za ndovu na yale malori ya FIAT!maeneo ya NZEGA na IGUNGA!Nadhani hao Babu zake walikuwa ndo wenyewe.Ilikuwa si mchezo.Jamaa hawa walikuwa wanasafirisha pembe huku jamaa amekaa na SMG hapo mbele kuona kama kuna mtu yeyote atakayezuia gari eti anataka kuwakamata!ana uawa kama kama paka au sungura!Alshabab hatari!!!!
 
kisheria huyu Bashe angeweza kufanya kinachotakikana pengine muda huu tusingekuwa hapa kuzungumzi haya.

- Bashe ameonesha kujiamini kusiko kwa kawaida ktk suala zima la uraia wake (ni aina fulaiya kiburi)

- Pia anaonekana kuwa anautaka uongozi kwa njia na gharama yoyote ile. Tujiulize kwa nini anautaka uongozi namna hiyo?

- Kwa elimu yake, kazi na mwenendo wake ktk macho ya jamii Bashe kaonesha kuwa hana jipya kwa siasa za Tanzania na.i.e. he's got absolutely nothing special to contribute from various positions he so vyied.

- Wahamiaji haramu wa kisomali na mataifa mengine wameenea duniani wakitaka kujipenyeza, ambapo serikali imara/makini zinapambana nao na kufanikiwa mara nyingi; lakini ktk nchi zenye serikali dhaifu na zilizojaa rushwa hali huwa tete, nasikitika kusema Tanzania iko ktk kundi hili. Mpaka sasa sijui usalama wa nchi hii ukoje maana ikiwa tu kijana kama Bashe anawasumbua namna hii je hao mapapa walio nyuma yake itakuwaje?
 
Watanzania wenzangu, tufike mahali tukatae kwa nguvu zote ubabaishaji na uhuni wa aina ya Bashe. Kwa mfano hata kama kisheria Bashe angeweza kuwa raia wa Tanzania lakini kwa mambo aliyofanya ni wazi ameonesha HANA MAADILI wala SIFA za uongozi.

Mfano ni viambatanisho vilivyoko hapa. Chukulia mathalan Kiambatanisho Namba 4. :-

- Hapa Bashe alisoma elimu ya sekondari 1991-1998, jumla ya miaka 8 kwa nini?

- Miaka yake ya kuzaliwa pamoja na majina tofauti tofauti anayotumia sehemu tofauti tofauti

- Baba yake alizaliwa 1928 au 1947? Na je ni Msomali au Mtanzania?

Narudia tena rai yangu, Watanzania tufike mahali tukatae kwa nguvu zote aina ya watu wa Bashe, hata kama ni genius wa aina gani. Uhuni huu umelifikisha Taifa hapa lilipo. Uhuni huo huo umeifikisha CCM kaburini. Kama CCM inakufa kwa sababu ya aina ya mambo kama haya basi na Taifa hili pia linaweza kuangamia kwa gonjwa hilo hilo.
 
Huu ni uhuni. Bashe ni raia halali kwa mujibu wa taratibu na sheria za uhamiaji Tanzania. Sijui kwa nini watu wanaendeleza hizi porojo za kizamani. Wanashindwa kupambana na huyo kijana kwenye ulingo wa siasa, sasa wanajificha kwenye uraia wake! Very sad!

binafsi nadhani nchi hii ni sawa na shamba la bibi,hivi kweli hatujui madhara ya alshabaab?Wenzetu wajerumani wanauwezo mkubwa sana wa kulinda utaifa wao.Hata kama unaonekana mzungu kama wao wanauwezo wa kujua wewe si mwenzao.Sisi mbona ingekuwa rahisi zaidi kuwabaini wasio wetu?
 
Huu ni uhuni. Bashe ni raia halali kwa mujibu wa taratibu na sheria za uhamiaji Tanzania. Sijui kwa nini watu wanaendeleza hizi porojo za kizamani. Wanashindwa kupambana na huyo kijana kwenye ulingo wa siasa, sasa wanajificha kwenye uraia wake! Very sad!


Kweli mdau ila tumsubiri Bashe nae aje aseme maana hata watanzania wenzetu kwenye hili suala la kurudisha umri hawajambo hasa kwenye kugombea uongozi ambao unaonyesha kuna kikomo cha umri kwani UVCCM kuna watu ukiwaangalia wanaonekana kabisa vibabu, tatizo hii issue inaangukia kwa mtu ambae ana matatizo ya uraia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anakubalika na wananchi wa nzega na ni tishio kwa watu wa Nzega na ndio maana yote yanaibuka vinginevyo haya yote yasingetokea
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ulieleta mada naona unatumika mkuu.
Hata kingwangwala nae nasikia sio raia.....
So wote mwaka 2015 mnatakiwa kupigwachini na kuweka majembe ya CDM
 
Maganga Masanja amefanya kweli tena, ameleta document zingine tena ofisini kwetu, nitazibandika hapa nikifanikiwa kuzipata. huyu jamaa ni kiboko sijui ana maslahi gani kwenye hili suala. naona wakubwa wanajadili kisha wanaachana bila maamuzi
 
Akina Bashe na mifumo inayowalinda ni balaa kwa Taifa hili. Aende Somalia kuna nafasi kibao zinatafuta watu wa kuziongoza. Hongera mwandishi wa habari hii kwa uzalendo wako.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom