Uhalali gani serikali kutoa msaada kwa mchungaji mwasapila- loliondo

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Najaribu kufikiri itakuwaje watu wa dini ingine wakianza kuhoji uhalali wa serikali kumpa msaada mchungaji wa mstaafu wa KKKT katika kuendesha huduma yake.

Mara kwa mara waislamu wamelalamika kuwa serikali inawapendelea wakristo hasa wakatoliki katika kuwasaidia.

Tunajua serikali haina dini. Na hutenda kazi zake kwa kufuata sheria ya nchi, sheria ipi imetumika kumsaidia mchungaji mstaafu.

Sina ugomvi na mchungaji Mwakasapile kwani hata mimi ni muumini wa kikristo dhehebu la lutheran. Hofu yangu ni pale watu watakapoanza kuchokonoa maswala haya.

Nawasilisha.
 
Atokee mmoja wao aoteshwe ndoto, naye atibu watu akiwa porini sana, avute watu kiasi cha kila kona kumzungumza yeye! atibu magonjwa sugu, iwe kweli iwe uongo sijui, na yeye atapata msaada

Familia ya Mwinyi ilikuwa huko juzi na kwa bahati mbaya walipata ajali, ninamzungumzia ALHAJI hapa!!
 
Webby.
Hivyo vingezo ulivyotoa mimi sidhani kama ndio vinampa uhalali Mchungaji Mwasapila kupata msaada serikalini, kwani serikali wameishasema kama kuna Provable yoyote kutoka kwa Mchungaji Mwasapila? kikingine familia ya Alhaji Mwinyi kwenda Loliondo sio Reference, kama unakumbuka Alhaji Mwinyi alishawahi kupigwa kibao kwa misimamo yake ya kidini ya kukubali matumizi ya kondomu
 
Mkuu nimeweka famili ya mwinyi kuonyesha kuwa, hilo swala la kusema mbona babu anasaidiwa , halitatokea kamwe!
 
Hivi ule mtambo wa mawasiliano wa Airtel waliofunga lol ni kwa ajili ya simu ya babu tu ama watu wote wa Loliondo?
.
 
Najaribu kufikiri itakuwaje watu wa dini ingine wakianza kuhoji uhalali wa serikali kumpa msaada mchungaji wa mstaafu wa KKKT katika kuendesha huduma yake.

Mara kwa mara waislamu wamelalamika kuwa serikali inawapendelea wakristo hasa wakatoliki katika kuwasaidia.

Tunajua serikali haina dini. Na hutenda kazi zake kwa kufuata sheria ya nchi, sheria ipi imetumika kumsaidia mchungaji mstaafu.

Sina ugomvi na mchungaji Mwakasapile kwani hata mimi ni muumini wa kikristo dhehebu la lutheran. Hofu yangu ni pale watu watakapoanza kuchokonoa maswala haya.

Nawasilisha.
Kwanza kama kuna msaada wa serikali umetolewa, umetolewa kwa babu siyo KKKT. Pili swali hili lingekuwa na mashiko kama ungeuliza wakati mkapa anatoa chuo cha Tanesco kule Morogoro kuwa chuo kikuu cha kiislamu
 
Atokee mmoja wao aoteshwe ndoto, naye atibu watu akiwa porini sana, avute watu kiasi cha kila kona kumzungumza yeye! atibu magonjwa sugu, iwe kweli iwe uongo sijui, na yeye atapata msaada

Familia ya Mwinyi ilikuwa huko juzi na kwa bahati mbaya walipata ajali, ninamzungumzia ALHAJI hapa!!

Dah! Shetani anawafuasi kweli.
 
Atokee mmoja wao aoteshwe ndoto, naye atibu watu akiwa porini sana, avute watu kiasi cha kila kona kumzungumza yeye! atibu magonjwa sugu, iwe kweli iwe uongo sijui, na yeye atapata msaada

Familia ya Mwinyi ilikuwa huko juzi na kwa bahati mbaya walipata ajali, ninamzungumzia ALHAJI hapa!!
akitokea askofu kabaka. basi akitokea mwengine ambae sio askofu tusema asishatakiwe kwa kuwa askofu mbona kabaka? swala la familia ya mwinyi na liliondo hamna ralation.
 
Kwakweli serikali yetu haina nia njema na wananchi wake kwani imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwasaidia waathirika wa Ukimwi kwa hisani ya watu wa nje ya nchi leo kajitokeza mtu anayedaiwa kuwa anatibi magonjwa ambayo wao hawana hata chembe ya fikra kuwa kuna mtu ambaye anaweza japo ksaidia mambo kama hayo,kama wanekuwa na nia njema kwa watanzania wangeweza kumwezehs Babu afanye kazi hii ya kuwaokoa watanzania wenzake mahali pazuri...ona eti hata choo mpaka wagonjwa wachange hiyo ni aibu kubwa ingekuwa mimi ningejiuzulu madarakani kuwa nimeshingwa kuwatumikia wananchi ..Aibu ndugu zangu hawa wajamaa wataendelea kuumbuka hadi siku ya kiyama..
 
Kwanza kama kuna msaada wa serikali umetolewa, umetolewa kwa babu siyo KKKT. Pili swali hili lingekuwa na mashiko kama ungeuliza wakati mkapa anatoa chuo cha Tanesco kule Morogoro kuwa chuo kikuu cha kiislamu

serikali haijatoa msaada kwa babu!!!!!
barabara inayotengenezwa haitamsaidia babu bali wananchi wote na vijiji vya jirani.
dispensary iliyoboreshwa hatibiwi babu ila ni ya wananchi kwa ujumla.
nini kingine, msisahau pia serikali inakusanya road toll..
Actually kinachofanyika ni serikali inafanya kile ilichotakiwa kufanya siku zote kwa raia wake.
 
Kwanza kama kuna msaada wa serikali umetolewa, umetolewa kwa babu siyo KKKT. Pili swali hili lingekuwa na mashiko kama ungeuliza wakati mkapa anatoa chuo cha Tanesco kule Morogoro kuwa chuo kikuu cha kiislamu
Ongezea hivi:

Babu hajaomba msaada serikalini... pia hatibu watu wa dini moja.

Hajajengewa kitu na serikali..serikali ilichofanya ni kuwasaidia wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao kupata hiyo huduma.

Wanaotafuta huduma ni pamoja na waislam au unataka babu aseme ni kwa dini moja tu??
 
Kweli mkuu. Serikali haijatoa msaada kwa babu. Ilichofanya kama imefanya ni kuboresha mazingira kwa ajili ya wagonjwawanaomiminika huko. Watakaofaidika ni wagonjwa na wenyeji wa huko sio babu!!!!
 
Kweli mkuu. Chuo kilipotolewa kwa waislamu hakuna kelele hebu fikiria kama kingetolewa kwa wakristo! Duh! Ingekuwa balaa!! Ila wakristo endeleeni kutanganza amani kwa watu wote. Msaada ni kwa watu wa huko sio babu.
 
mpate kheri nyote. Ni kweli kabisa serikali haitoi msaada kwa Mch. bali inafanya yatakiwayo kwa wananchi wake. wasafiri salama , wakifika wakute dawa wanywe na kisha kurudi haraka wakiwa wazima, waendelee kulijenga taifa leo hili. Mbona serikali imekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi siku zote kwa kuongeza madawa hospialini na kadhalika.
 
Babu anatua huduma kwa jamii na kwa bei nafuu ambayo inasababisha watu wenge kwenda katika eneo moja ambalo serikali haikuwahi kufikiria hako kakijiji hata nadhani mbunge wao na mkuu wa mkoa hakukijua. Kwahiyo serikali inafanya kile ambacho inatakiwa kufanya kwa wananchi wake kuwawekea huduma muhimu kama barabara na huduma za afya. Au unataka serikali ijenge kijijini kwenu kunanini? Tanzania siye masikini serikali ya fanya lile liwezalo
 
shukrani ya jk kwa babu baada ya kupiga kikombe na kupona na kuchangamka siku hizi hadi kupata ujasiri wa kuwatema washikaji zake mafisadi wasulubiwe,..si unajua babu hapokei shukrani ya hela..they fill guilty.jk kachangamka siku hzi jamani eh..!!mwasapile fill my cup..
 
Nadhani serikali yetu ina upe mdogo sana na sikutegemea kama viongozi wa ngazi za juu wangejitokeza kuhamasisha watanzania kukimbilia kwenye tiba ambayo hadi leo tamko la serika lilotolewa juu ya dawa ya babu in kuwa haina madhara,vile vile wataalam wetu wa afya ni sifuri kabisa na hii inatokana na siasa kutumika hata pasipo takiwa,ni aibu ila yote ya yote napmongeza babu sana.
 
Back
Top Bottom