Uhaba wa dawa , watumishi unavyokatisha tamaa wagonjwa

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa muda mrefu sasa serikali imejikuta ikilaumiwa kwa kutowashirikisha kikamilifu wananchi katika kupanga matumizi ya huduma ya afya hususan vijijini. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hali hiyo imechochea malalamiko kutoka kwa watu wengi wakiwemo wenye vipato duni kwamba hawathaminiwi. Katika makala haya Mwandishi ,ABDUL MITUMBA ametembelea wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na kuzungumza na baadhi ya wakazi wa kata sita na wadau wa sekta ya afya juu ya hatua zinazochukuliwa kuboresha huduma za afya.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Moja kati ya malalamiko yaliyosikika kutoka kwa kila mtu aliyehojiwa ni ukosefu wa dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lalamiko lingine ni usiri wa utoaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za huduma za afya kwa wananchi ambapo sera inaagiza ziwe zinabandikwa katika ubao wa matangazo kila zinapotolewa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa kawaida matangazo hayo hubandikwa nje ya hospitali, vituo vya afya, zahanati na ofisi za watendaji wa kata au watendaji wa mitaa, vijiji au vitongoji.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lengo ni kuonyesha uwazi jinsi serikali inavyotekeleza sera ya huduma za afya ikiwa ni pamoja na kuonyesha jinsi fedha za afya zinazoelekezwa katika ngazi za kata na vijiji zinavyotumika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini kwa wilaya ya Bagamyo hali ni tofauti kidogo ambapo taarifa hizo zimekuwa siri kubwa na kata pekee iliyoweza kubandika taarifa hizo ni Dunda.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kata nyingine tano zinazounda wilaya hiyo kongwe ambazo zimeshindwa kuweka bayana taarifa hizo ni Kiromo, Zinga, Kiwangwa, Magomeni na Vigwaza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hali hiyo inawanyima wananchi fursa ya kujua ni kiasi gani cha fedha kimetumwa katika kila kata kutoka wilayani ili kuhudumia wananchi na zinabaki ngapi kila inapofika mwisho wa mwaka.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hali hiyo imeishawishi asasi ya kiraia inayojishughulisha na utoaji wa elimu ya afya, ustawi wa jamii na mazingira, Movement of Poverty Eradication (MOPE) kuendesha mradi wa kutoa elimu kwa wananchi ili wawe na uwezo wa kuhoji na kufuatilia matumizi ya fedha hizo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chini ya mpango huo uliofadhiliwa na asasi nyingine ya kiraia ya The Foundation for Civil Society, MOPE ilitembelea kata zote sita na kuzungumza na wadau wa afya kujua uwajibikaji wa serikali katika utoaji wa huduma hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mratibu wa mradi huo kutoka Mope, Dk.Joel Bwemelo anasema katika uchunguzi uliofanywa na asasi hiyo umebaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika utoaji wa huduma hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema uhaba wa dawa, uchache wa wahudumu wa afya katika hospitali, zahanati na vituo vya afya pia unachangia kwa kiasi kikubwa kuwavunja moyo wananchi.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Imebainika kuwa watu hufika kupata huduma katika vituo kadhaa, lakini mapungufu hayo yanasabisha watumie muda mrefu wakati mwingine hadi kufikia zaidi ya saa tano kabla ya kupata huduma, " alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati mwingine Bwemelo anasema kutokana na idadi ndogo ya watumishi na wingi wa watu wanaohitaji huduma baadhi yao hujikuta wakiondoka bila kupata huduma.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Subira Iddi mmoja kati ya wakazi wa kata ya Magomeni anasema pamoja na matatizo yote hayo, bado kuna baadhi ya viongozi katika vituo vya huduma za afya ambao wanadai hongo ili kutoa upendeleo kwa watu wanaofika kupata huduma.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema katika kutekeleza adhama yao wapo baadhi ya watoa huduma ambao huwachomoa watu katika foleni na wengine kuwaruhusu kupitia milango ya nyuma ili wapate huduma wakati siyo utaratibu.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini siyo kwa wataalam pekee, rushwa pia ipo hata kwa baadhi ya viongozi wa ofisi za serikali kuanzia ngazi za vijiji na kata ambapo watu wanalazimika kutoa chochote kupata huduma mbalimbali,” alisema Subira.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mfano wa huduma hizo ni kupewa barua ya utambulisho kazini, dhamana mahakamani na katika taasisi za ulinzi na usalama ikiwemo polisi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkazi mwingine wa Zinga, Athuman Mahenda anasema kitendo cha mgonjwa kufika hospitali au kituo cha afya lakini akabainika anaumwa malaria lakini mwisho anaambiwa hakuna dawa na kuonyeshwa duka la jirani ili akanunue kinakatisha tamaa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema katika mazingira ya kawaida ni rahisi kwa mtu yoyote kubashiri kuwa maduka hayo ni mali ya wahudumu wa serikali na kwamba upo uwezekano kuwa uhaba huo wa dawa katika zahanati za serikali unachangiwa na watumishi hao.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Ndiyo maana huwa hawataki kuwashirikisha wananchi katika kuwaambia ni kiasi gani cha fedha za huduma ya afya zinaletwa katika ngazi za kata," alisema Mahenda.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Muuguzi mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Rosweeter Mushi ,anasema pamoja na mapungufu y ote yaliyopo, ofisi yake inajitahidi kuwashirikisha wananchi kikamilifu[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]kwa kuwahusisha watendaji na wataalam hadi ngazi za vijiji ili kuweka wazi fedha na matumizi yake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema sera ya afya inaelekeza kuwa wizara inapotenga fedha kwa ajili ya mikoa utaratibu unapaswa kufuata ngazi husika ambapo maelekezo yanatolewa kwanza kabla ya fedha hizo kutumwa wilayani na baadaye ngazi ya kata na vijiji.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Naye Kaimu Katibu wa Afya wilayani Bagamoyo, Agnes Mkingwa amesema uchunguzi uliofanywa na Mope umechochea changamoto ya uwajibikaji katika kila ngazi ili kufikia malengo ya kutoa na kufikisha huduma za afya zilizo bora hadi vijijini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Kikubwa ambacho Mope imefanya kwa sasa ni kurudisha taarifa zilizotokana na uchunguzi wake juu ya ubora wa huduma za afya unaotolewa na serikali wilayani Bagamoyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hii ni tofauti kidogo na asasi nyingine zilizowahi kufika Bagamoyo na kuchunguza mambo mbalimbali," alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Zinga, Sharifa Msangu alisema tatizo lingine linalokwamisha utoaji wa huduma za afya ni mwitikio mdogo walio nao wananchi hasa wanapoitwa katika mkutano ya vijiji kwa lengo la kuwapa melekezo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema mikutano mingi inakosa watu na hata serikali inapolazimika kuandaa chakula na ngoma idadi ya wanaofika pia huwa ni ndogo, hatimaye wananchi wengi wanakosa taarifa muhimu zinazohusu upatikanaji wa huduma za afya.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza wakati wa mdahalo wa wadau wa afya wilayani humo, Mwenyekiti wa MOPE, Peter Nicolaus, alisema mradi wa kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuhoji na kufuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazoekezwa katika ngazi ya kata (PETS) ni sehemu ya serikali ya kujaribu kudhibiti matumizi ya fedha hizo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema mdahalo huo wa siku nne uliwashirikisha wananchi wa kawaida na wadau wa sekta ya afya kwa ngazi za vijiji, kata na wilaya na ni matokeo ya mradi wa mwaka mmoja uliolenga kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya watoa huduma na wananchi katika kufikia malengo ya upatikanaji wa afya njema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Diwani wa kata ya Kiromo, Stamili Mbonde alisifu utendaji kazi wa Mope ingawa hakusita kuweka wazi hofu yake ya kuwepo kwa baadhi ya asasi za kiraia zinazotoa takwimu sizizo sahihi za fedha zinazotumwa kwenye kata na matumizi yake na kusababisha migongano kati ya wananchi na serikali yao.[/FONT]

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom