Ugumu wa kupata kazi partly tunajitakia wenyewe.........

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722

Tuna watu wamesoma, wana madigiriii kibao!
Kazi zikitangazwa, hizo applications ukisoma,
hadi raha maana kingereza kingiiiiii!
Kinachoshangaza, "lugha" kwenye izo applications
utadhani kuna mtu mmoja anawaandikia karibu wote!
Kumbe bana, templates za kwenye internet!
Mwite mtu kwenye usaili. Tumia lugha ile ile aliyoletea maombi.
Utachoka maana ni kigugumizi kwenda mbele!Wengi huishia kukosa
fursa za kazi.

Tujikumbushe vitu vichache ili tuboreshe ushindani:
1. Ukimaliza chuo na ukaona kimombo hakipandi, jiandikishe lugha hiyo
mara moja.Nashauri British Council English course hata kama
utalipa zaidi kidogo kuliko kwenda vyuo ambapo utafundishwa
na mtu asiyekijua kimombo vizuri.
2. Ukiwa shule jitahidi kujishughulisha hasa ujue grammar
na structure ya lugha ya kiingereza,
Mapuuza tunayoyaona na kuyasikia na hata kuyasoma hapa
yakiponda lugha ya kiingereza yanawa cost watu.
3. Jiandae uwe mahiri kabla ya usahili.Epuka kudesa ma template
ya internet na kuweka mbwembwe nyiiingi kwenye application letters kama hivi:
"Excellent in analytical and writing skills, with fluency in English"
huku ukijua kabisa lugha hii ni utata mtupu kwako!Andika barua
simple ujieleze kwa lugha yako mwenyewe!Bora hata uandike kwa kiswahili fasaha!
4. Kuna watu wanaamini ati kazi kama uhasibu au udaktari hazihitaji kuwa mahiri kwenye lugha.
Huu ni upotoshaji.Hamna kazi isiyohitaji kuandika taarifa au kuwasiliana kimaandishi.
Nani ana muda kumsimamia mtu mzima kama mwalimu wa lugha na mwandiko shule ya msingi?
Umahiri ni pamoja na kuweza ufanya kazi zako zote with minimum supervision.

Tujitahidi basi ili tuweze kushindana kwenye soko la ajira.
 
Hiyo ni kweli kabisa, niliwahi kuona apllication letters vijana wasomi kabisa na cv zao ni aibu kabisa,Mbaya kabisa nilisikitika livyoona na masters graduate ni human resources kutoka mzumbe karibia kulia.CV yake mbaya ajabu pamoja na cover letter.Vijana wengi wanahitaji capacity building ya hali ya juu sana katika eneo la kutafuta kazi bora. Kitu kibaya ni mob pschology ya wanafunzi kutozingatia na kutega masomo ya lugha na kujifanya ni ngwini na hayana manufaa kwao au pengine kujifanya wanayafahamu sana kumbe sivyo na sasa wengi yanawatesa katika kupata kazi bora.
 
Back
Top Bottom