m_kishuri
JF-Expert Member
- Jan 27, 2010
- 1,484
- 372
FROM:MATONDO
Maprofesa wazee waliopitwa na wakati nao wanachangia. Pia umalaya kwa wanafunzi wa kike, uzembe, wivu na kutotakiana mema. Sababu ni nyingi. Mpaka imefikia hatua sasa msichana mzuri kama mimi ukipata A eti watu wanakuzushia kwamba umevua chupi kwa profesa. Tunahitaji kubadilika jamani, lakini hili ni tatizo kubwa sana na linavunja moyo kweli. Mtu unajisomea weeee halafu unaambulia B - hata kama mtihani ni take home.
#Wanajamii, nimelileta hili suala hapa jukwaani ili tusaidiane kimawazo kuhusu hili suala, kwani naamini kuna wanajamii wengi ambao wamepitia aidha Mlimani au SUA. J e ni vibaya kumpa mtu A+ au A kwa sababu Prof. ataonekana hajui kufundisha ? Binafsi sijuwi hii dhana wameitowa wapi.
- Utakuta darasa lina wanafunzi 100, na kati ya wanafunzi hawa pengine wawili, watatu na hata mmoja tu ndiyo atapata "A". Hata madarasa makubwa yenye wanafunzi 300, eti wanafunzi wanne au watano tu ndiyo wanapata "A". Kwa nini? Ni kwa sababu masomo ni magumu sana? Wanafunzi hawajisomei sawasawa (Na kama hawajisomei ni kwa nini?), maprofesa hawafundishi vizuri kiasi kwamba wanafunzi hawawaelewi? Au maprofesa wanatunga mitihani migumu kupindukia? Au pengine wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu ni mbumbumbu na hawana uwezo wa kupata A?
- Ninacholalamikia hapa siyo kila mwanafunzi kupata A bali ule ugumu uliopo wa kupata alama hizi kwani siamini kama kweli eti katika darasa la wanafunzi 300, ni wanafunzi watatu au wanne tu ndiyo wana uwezo wa kufaulu vizuri. Kama hivi ni kweli basi ni wazi kuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa elimu.
4. Hali ilivyo hapa Marekani
- Hapa kupata A ni jambo la kawaida na maprofesa na wanafunzi wanalijua hili. Mahusiano kati ya wanafunzi na maprofesa ni ya wazi na wanafunzi wanaweza kuuliza maswali na kujadili masuala ya gredi watakazozipata na maprofesa wao kwa uwazi. Hali hii inasababisha matatizo fulani na haya nitayaongelea siku nyingine.
- Ati, kwa nini ni vigumu sana kupata A na hatimaye "first class" katika vyuo vikuu vyetu? Tatizo hasa ni nini? Ni mfumo wa elimu tuliorithi kutoka kwa Waingereza? Pengine inabidi tulifikirie jambo hili kwani inawezekana tukawa tunawahujumu wanafunzi wetu kwa kuwapotezea nafasi za ufadhili katika mashirika mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu, jambo ambalo si jema hasa katika kipindi hiki ambapo kusema kweli mambo yako wazi sana kuhusu masuala ya ufadhili wa kimataifa.