Ugonjwa wenye utata

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Naishi na mdogo wangu miaka 16 yupo form one. Ameanza kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda wa saa nzima na ameanguka kama mara tatu katika kipindi cha mwaka mmoja.
Lakini akianguka hatoi mapovu, wala harushi miguu .

Naomba msaada kwa mtu anayejua kuhusu ugonjwa huu, na unasababishwa na nini?
 
Kawaone wataalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu (Neurologist), Muhimbili, Bugando, Mbeya na KCMC wapo.
Kuna dawa za kuzuia asiendelee kuanguka na dawa ni za kutumia muda mrefu (karibia maisha yake yote).
Mpeleke hospitali. Anaweza kuwa ana uvimbe ndani ya ubongo. Msimalizie pesa kwa waganga wa kienyeji.
 
Mpeleke hospitali haraka, kuna uwezekana mkubwa akawa na uvimbe kwenye ubongo.....
 
Kuanguka na kupoteza fahamu ni dalili ya tatizo katika mfumo wa ubongo na viunganishi vyake. Yaweza kuwa tatzi lipo sehemu ndogo sana lakini yenye ushawishi mkubwa katika Central Nervous system.(CNS)
Kifafa (epilepsy) ni moja ya matatizo ya CNS, siku hizi inaitwa Seizure kwa vile si kila aaungukae ana kifafa. Kwa faida ya wasomaji kifafa kinaweza kuwa cha kurithi, au kinachotokana na matatizo ya afya kama Birth trauma(wakati wa kuzaliwa), Pregnant(kifafa cha mimba) au hata High Blood pressure. Ndiyo maana inapendekezwa kuitwa Seizure hadi itakapogundulika vinginevyo.
Kwa huyo mdogo wako mpeleke kwa wataalam wa CNS (Neurologist) ambao watamwangalia kwa undani. Mara nyingi kipimo kinachoitwa CT Scan hutumika.
Tafadhali naomba uni PM
 
Back
Top Bottom