Ugonjwa wa Surua (Measles): Chanzo, maambukizi, dalili, athari, matibabu na kinga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,113
Surua ni mojawapo ya magonjwa ya kuambukiza yanayotisha kwa binadamu. Huu ni ugonjwa ulio na kiwango cha juu cha karibu asilimia 100 cha mashambulizi pindi mtu apatapo vimelea vya ugonjwa huu.

Pamoja na kuwepo chanjo ya ugonjwa huu, bado surua ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 katika baadhi ya maeneo duniani hasa kwa nchi zinazoendelea.

Ugonjwa huu ambao ulitoweka katika baadhi ya nchi, umeanza kuonekana tena hivi karibuni miongoni mwa watu ambao hawakupata chanjo katika nchi za Uingereza na nyingine za Ulaya.

Surua husababishwa na nini?

Surua huenezwa na aina ya virusi jamii ya paramyxovirus. Jamii hii ya virusi hupatikana katika mfumo wa njia ya hewa. Hukaa katika kamasi na majimaji yaliyopo katika mfumo wa hewa. Kwa sababu hii basi virusi hawa huenezwa kwa njia ya upumuaji.

Virusi hawa wanaweza kuishi hewani kwa muda wa hadi saa moja baada ya kutolewa kwa kupiga chafya au kukohoa au hata mazungumzo na mgonjwa. Hii ina maana kuwa, ili kuambukizwa surua, si lazima mtu akutane uso kwa uso na mgonjwa.

Baada ya kuingia ndani ya mfumo wa hewa virusi hushambulia seli za utando wa nje wa njia ya hewa (respiratory tract epithelium) na kuingia katika mzunguko wa wa limfu na kufika kwenye tezi zilizo karibu. Katika tezi huzaliana zaidi na kusambaa mwilini.

Muonekano wa mgonjwa

Dalili za awali za surua huanza kuonekana baada ya siku 8 ya kupata uambukizi. Mgonjwa huwa na mafua mepesi, homa, kukohoa na macho kuwa mekundu.

Baada ya siku 2-4 tangu kuanza kuonekana kwa dalili za awali, ukichunguza mdomo wa mtoto, na kama utamchunguza pembeni (ndani ya shavu) utaona vidonda vyeupe kwenye utando mwekundu wa ndani ya mdomo. Vidonda hivi huonekana kama chumvi iliyomwagwa kwenye zulia jekundu. Vidonda hivi huitwa Koplik spots. Hii ni dalili tosha ya kuthibitisha uwepo wa surua.

Lakini vilevile mgonjwa anaweza kuwa na vipele vidogo sana ambavyo inaweza kukuwia vigumu kutambua. Vipele hivi huweza kuonekana vizuri siku mbili baadaye. Kwa kawaida, vipele hivi huanzia usoni au nyuma ya sikio na kushuka chini kabla ya kutapakaa mwili mzima siku zinazofuata. Vipele huongezeka na kuwa vingi kadiri siku zinavyopita. Kawaida hali hii ya vipele inaweza kuchukua kati ya wiki 1-2. Vipele hupotea baada ya siku 7 na kuacha ngozi iliyobabuka. Hata hivyo, kukohoa kunaweza kuendelea zaidi ya siku 10.

Athari za Surua ni zipi?

Ingawa baadhi ya wagonjwa hupona katika kipindi cha siku 10 mpaka 14, baadhi hupata matatizo zaidi yanayoweza kuwa ya muda mrefu kama;
  • Maambukizi njia ya masikio (Otitis media)
  • Maambukizi njia ya chini ya mfumo wa hewa kama vile
    • Uambukizi kwenye mirija ya hewa ya koo (bronchitis) maambukizi kwenye njia ya sauti (laryngitis) na croup. Surua inaweza kusababisha kuvimba katika sehemu ya sauti na kuathiri uwezo wa kutoa sauti lakini vilevile inaweza kusababisha uvimbe katika kuta za utando wa njia ya hewa.
    • Homa ya mapafu (pneumonia) ambayo ni sababu kuu inayosababisha vifo vinavyotokana na surua. Mgonjwa wa surua ni rahisi kupata homa ya mapafu kwa sababu kinga ya mwili wake huwa imepungua. Homa hii ya mapafu yaweza kusababishwa na aina nyingine ya virusi kama adenovirus, herpes simplex au bakteria kama Staphylococcus aureus, Streptococcus pneumonia, Haemophillus influenza, Klebsiella pneumonia. Lakini vilevile Kifua kikuu kinaweza kutokea kwa kusababishwa na upungufu huu wa kinga mwilini.
  • Surua pia inahusishwa na aina mbalimbali ya mashambulizi kwenye ubongo kama vile
    • Acute encephalitis ambayo hutokea wakati au ndani ya wiki chache baada ya maambukizi.
    • Progressive encephalitis ambayo hutokea kwa wagonjwa walio na upungufu wa kinga mwilini unaotokana na sababu yeyote ile ikiwemo wale anaopata tiba ya kemikali (Chemotherapy) au kwa sababu ya VVU. Hali hii hutokea miezi 6 baada ya maambukizi, na inaweza kusababisha mgonjwa kufa.
    • Subacute sclerosing panencephalitis (SSPE) ni nadra sana kutokea. Iwapo ikitokea, mara nyingi huwa ni mwaka mmoja wa mgonjwa kupona surua. Dalili mojawapo ya tatizo hili ni kupungukiwa kwa uwezo wa kufikiri, akili kuzorota na hatimaye mgonjwa kufariki dunia.
  • Surua inaweza kusababisha utapiamlo kwa sababu ya ukali wake hasa kwa watoto ambao hawapati lishe nzuri. Inahusishwa pia na kuharisha na kutapika na kusababisha upungufu wa maji mwilini.
  • Surua husababisha upungufu wa Vitamini A na kusababisha tatizo la kutoona vizuri ambalo hijulikana pia kama Keratitis. Kwa mtoto ambaye ana upungufu wa Vitamini A tatizo la macho huwa kubwa zaidi na kwa kitaalamu hujulikana kama Keratomalaciaambapo sehemu nyeupe ya jicho hutoboka.
  • Maambukizi katika misuli ya moyo (Myocarditis)
  • Upungufu wa chembe sahani kwenye damu (Thrombocytopenia)
Utambuzi wa surua

Utambuzi wa surua inajumuisha historia ya mgonjwa kuwa na homa kwa angalau siku 3 na kuwepo kwa mojawapo ya dalili za mwanzo za surua ambazo ni kukohoa, kuwa na mafua mepesi, macho kuwa mekundu na upele mwilini. Aidha ikithibitika mgonjwa ana Koplik spotsbaada ya uchunguzi ndani ya mdomo ni utambuzi tosha wa surua.

Vilevile vipimo vya kimaabara ni pamoja na uthibitisho chanya wa antibodi dhidi ya surua(measles IgM antibodies) na uwezekano wa kuwapata virus wa surua kutoka katika mfumo wa hewa, damu au mkojo wa mgonjwa (isolation of measles virus RNA) au kwa njia ya kuoteshwa maabara (culture).

Matibabu

Hakuna tiba maalum kwa ajili ya surua. Lengo kubwa la matibabu ya surua ni kuhakikisha mgonjwa anapata mapumziko, maji ya kutosha, oksijeni na faraja. Mgonjwa anaweza kupewa dawa za kutuliza homa kama vile paracetamol. Imeonekana kuwa matumizi ya dawa ya virusi wa surua (antivirus) hayana msaada wowote katika kutibu surua.

Aidha dawa kwa ajili ya kuzuia magonjwa yanayosababishwa na bakteria (Prophylactic antimicrobial therapy) isipokuwa tu iwapo itathibitika kuwepo kwa maambukizi ya bakteria. Inasisitizwa sana mgonjwa apatiwe Vitamini A. Vitamini A hupunguza hatari ya kifo na madhara ya surua.


Kwa vile ugonjwa wa surua unaenea kwa njia ya hewa ni vizuri mgonjwa akatengwa na watoto wengine. Muhimu ni kutafuta ushauri wa daktari haraka pale unapoona mtoto ana dalili za surua.

Kinga

Surua huzuiwa kwa urahisi kwa njia ya chanjo. Watoto ambao hawajapata chanjo ya surua wapo katika hatari kubwa sana ya kupata surua.

Kumbuka

Surua ni ugonjwa hatari. Unaweza kuua au kusababisha madhara ya muda mrefu lakini chanjo dhidi yake inazuia hatari hiyo. Kwa hiyo pale unapohisi mtoto wako ana dalili za surua mpeleke haraka hospitali ili kujithibitisha na kupata matibabu yanayofaa.

Chanzo: Watoto
 
Habari wana jf, naombeni msaada wenu, nina mtoto wa miaka 4, alitoka vipele mwili mzima, kumpeleka hospital wakasema ni surua, amepewa dawa na amepona, sasa kaka yake wa miaka 6 naye ameanza kutoka vipele kama vya mwenzie, sasa nnachowauliza, je, watoto wa umri huo wanaweza kupata ugonjwa huo? Ingawa walishamaliza chanjo zote? Mana nahofia mwanangu mdogo acje naye akapata huo ugonjwa, na chanjo za surua ni miezi 9 na 15, na wote walishazimaliza, naombeni mnisaidie.
 
Mimi nliwahi ugua surua nikiwa 11years, unaambukizwa sana maeneo ya shuleni na watoto wanarudisha nyumbani.

Mnaweza kuugua hata wote iwapo yupo ambaye hajawahi kuugua lkn mkishatibiwa huwa haurudi tena.

Ugonjwa wa surua hujijengea chanjo wenyewe ukiugua, huwa haurudi.

Sijui chanjo ya awali huwa inaisha nguvu maana mimi nlichanjwa tena ktk ile kampeni ya mpaka miaka 15 ila nlishaugua wakati huo
 
Mimi nliwahi ugua surua nikiwa 11years, unaambukizwa sana maeneo ya shuleni na watoto wanarudisha nyumbani. Mnaweza kuugua hata wote iwapo yupo ambaye hajawahi kuugua lkn mkishatibiwa huwa haurudi tena. Ugonjwa wa surua hujijengea chanjo wenyewe ukiugua, huwa haurudi. Sijui chanjo ya awali huwa inaisha nguvu maana mimi nlichanjwa tena ktk ile kampeni ya mpaka miaka 15 ila nlishaugua wakati huo
Nashkuru kwa ushauri wako
 
140426144958_syria_refugee_children_624x351_afp.jpg


Taaarifa kutoka syria zinasema zaidi ya watoto kumi na mbili wamekufa na wengine kuugua baada ya kupewa chonjo ya surua inayosemakana kuwa haukuwa salama katika eneo linalodhibitiwa na waasi.

Shirika la Uingereza linahusika na uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria limesema chanjo hiyo ilitolewa katika maeneo ya vijijini kaskazini mwa Syria.


Ugonjwa kama surua na polio umesambaa tangu kutokea kwa mafarakano miaka ya 2011.

Huduma za afya zimevurugika sana nchini Syria.

Wapinzani kutoka chama Syrian National Coalition wa nchi hiyo wamesema watasitisha mpango wa chanjo ya surua kufuatia vifo hivyo vilivyotokea.

BBCSWAHILI
 
Habari zenu wana jamvi

Asubuhi ya leo mwanangu kapelekwa clinic kwa ajili ya matone lakini nilipopiga simu kuulizia nikaambiwa mtoto kuchomwa sindano ya bega.

Niipata shock iweje apewe tena sindano wakati tarehe 02/06 nilimpeleka akachomwa hiyo sindano ya surua?

Basi ikabidi niende kumuuliza nesi kulikoni na imeandikwa kwenye kadi? Basi akaomba msamaha kaniambia mtoto akifika miezi 18 hatachomwa tena.

Yaani nimekosa raha nina mawazo.

Naombeni ushauri wenu
 
Truly Ebu hujafafanua vizuri ebu ijazie nyama thread yako.

Kifupi nielewavyo sindano ya bega ni ya BCG namaanisha ya kifua kikuu na matone yale ni ya sabin namaanisha polio na sindano ya surua inachomwa kwenye paja la kulia kwa maelezo zaidi ntumie e mail yako nkutumia kitabu cha chanjo
 
Kachomwa chanjo ya surua kwenye bega kushoto. Kwenye kadi pia wameandika bega la kushoto. Sasa sijui hapo iko vipi tena lakini kachomwa begani.
 
UGONJWA wa surua ni moja ya magonjwa yanayoambukiza. Ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya “Morbillivurus paramyxvirus” vinavyoenea kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa pale mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya.

cdc_140606_measles_african_child_800x600.jpg

Ugonjwa huu huathiri watu wa rika zote,ingawa mara nyingi watoto wenye umri chini ya miaka mitano ndiyo huathirika zaidi kuliko watu wa umri kuanzia miaka mitano na kuendelea.

Mtu anapopata vimelea vya ugonjwa huu kiwango cha mashambulizi huwa juu zaidi ya asilimia 90. Hadi sasa bado ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya miaka mitano hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Virusi vinavyoeneza ugonjwa wa surua vinaweza kukaa hewani kwa muda wa saa moja baada ya kutoka kwa mtu mwenye maambukizi ambapo hutoka kwa njia ya chafya, mazungumzo au kukohoa.

Kutokana na uwezo huo wa virusi kukaa hewani kwa muda huo mtu anaweza kupata maambukizi hayo bila ya kukutana au kukaa karibu na mgonjwa.

Tuungane na Dkt Grace Chirwa kutoka Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaama anayetuelezea kuwa baada ya virusi hivyo kuingia mwilini hushambulia seli za utando wa nje wa njia ya hewa(respiratory tract epithelium) na kuingia katika mzunguko wa limfu na kufika kwenye tezi zilizo karibu. Baada ya kuingia katika tezi huzaliana zaidi na kusambaa mwilini.

Dalili za mgonjwa mwenye surua.

Mgonjwa mwenye maambukizi ya ugonjwa huu huwa na mwonekano au dalili za awali ambazo huanza kuonekana baada ya siku nane tangu mgonjwa huyo apate maambukizi.

Miongoni mwa dalili ni pamoja na kuwa na mafua mepesi, homa, kukohoa na macho kuwa mekundu.

Baada ya siku 2-4 tangu kuonekana kwa dalili za awali mgonjwa huyo akichunguzwa mdomoni hasa ndani ya shavu pembeni vitakuwepo vidonda vyeupe kwenye utando mwekundu wa ndani ya mdomo.

Vidonda hivi huitwa koplik spot. Vinapoonekana vidonda hivyo inakuwa dalili tosha kuwa mtu huyo anaugonjwa wa surua. Wakati mwingine mgonjwa anaweza kuwa na vidonda vidogo sana ambavyo inakuwa ngumu kuvitambua .

Vinaweza kuonekana vizuri baada ya siku mbili ambapo mara nyingi huanzia usoni au nyuma ya sikio na kushuka chini kabla ya kuenea katika sehemu nyingine za mwili.Vipele hivyo vinapoisha kati ya wiki moja hadi mbili huacha ngozi iliyobabuka.

Athari za ugonjwa wa surua.

Licha ya ugonjwa huo kuwa na uwezo wa kupona ndani ya siku kumi uwezekano wa mgonjwa kupata athari kubwa na hata za kudumu unakuwepo.

Mgonjwa anaweza kupata maambukizi ya njia ya masikio(otitis media), maambukizi kwenye mirija ya hewa ya koo(bronchitis), maambukizi kwenye njia ya sauti(laryngitis) na croup.

Ugonjwa huu unaweza kusababisha mtu kuvimba katika sehemu ya sauti na kuathiri uwezo wake wa kutoa sauti pamoja na kusababisha uvimbe katika kuta za utando wa njia ya hewa.

Athari nyingine ni homa ya mapafu(pneumonia) ambayo ni sababu kuu inayosababisha vifo vitokanavyo na surua. Mgonjwa wa surua ni rahisi kupata homa ya mapafu kwa sababu kinga ya mwili wake huwa imepungua.

Homa hii ya mapafu inaweza kusababisha aina nyingine ya virusi pamoja na ugonjwa wa kifua kikuu pamoja na maambukizi kwenye ubongo kama vile acute ancephalits ambayo hutokea wakati au ndani ya wiki chache baada ya maambukizi.

Pia mgonjwa anaweza kupata utapiamlo hasa kwa watoto ambao hawapati lishe nzuri.

Mgonjwa anaweza kupungukiwa na vitamin A linalopelekea lishindwa kuona vizuri. Kwa mtoto ambaye ana upungufu wa Vitamini A tatizo la kutoona huwa kubwa zaidi ya mtu mzima.

Utambuzi wa surua.

Utambuzi wa ugonjwa huu hujumlisha historia ya mgonjwa kuwa na homa kwa angalau siku 3 pamoja na kuwepo mojawapo ya dalili za mwanzo za surua. Mgonjwa huchukuliwa vipimo kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi wa kimaabara pamoja na uthibitisho chanya wa antibodi dhidi ya surua(measles igm antibodies) na uwezekano wa kupata virusi vya surua katika mfumo wa hewa.

Matibabu.

Hakuna tiba maalum ya ugonjwa huu. Matibabu ya ugonjwa huu ni kuhakikisha mgonjwa anapata mapumziko, maji ya kutosha, hewa safi pamoja na kupata faraja.

Licha ya kutokuwepo tiba maalum ya ugonjwa huu inasisitizwa mgonjwa kupewa Vitamini A ambayo hupunguza hatari ya kifo pamoja na madhara yatokanayo na surua.

Kutokana na ugonjwa huu kuenea kwa njia ya hewa ni muhimu mgonjwa akatengwa na watoto au watu wengine kuepusha uwezekano wa kuambuza watu wengi zaidi.

Kinga yake.
s1.reutersmedia.net.jpeg

Ugonjwa huu unazuiliwa kwa njia ya chanjo ambayo hutolewa kwa watoto. Watoto ambao hawakupata chanjo hiyowapo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom