Ugonjwa wa Pumu (Bronchial Asthma): Chanzo, dalili na tiba

Thanx mdau na wote mliochangia.
Unajua mitaani kuna mengi, eti wanadai kunadawa ya kutapisha na athma inakwisha kabisa

dont do that, uswahilini wanahisi pumu inatokana na kulishwa kitu,au wadhani kuna kitu kimekwama kwahiyo ukitapishwa inaisha.
kama nilivyokwambia,niliumwa pumu,na nilipewa kila dawa,hiyo ya kutapisha ilikuwa moja wapo,sijawahi ku experiance ladha mbaya kama ile,lazima utapike,ila haisaidii kabisa,ni mateso tu,jaribu kila ushauri unaopewa lakini sio kutapisha.
au kama sehemu uliyopo kuna joto,jaribu kumpeleka sehemu yenye baridi kama lushoto,mbeya,sio arusha kwasababu kuna vumbi sana.
maana hata mimi nilikuwa masaa 24 natumia feni,umeme ukikatika tu,nabanwa na pumu,kwahiyo inabidi mama anitoe nje usiku wa manane mpaka nipate nafuu na nipitiwe tena na usingizi.
asikwambie mtu,pumu inatesa,nikimuona mtoto amebanwa yaani lazima nilie,maana najua jinsi anavyoteseka.
 
Niliwahi kuwa na tatizo kama hilo, kuna dawa nilielekezwa na Mkibizi from Rwanda ilinitibu kabisa, ni magombe ya mti wa matawi ( yale tunayoshika siku ya J2 ya Matawi) unachovya kwenye asali kisha unatafuna. Itakusaidia.
 
Wadau naombeni mawazo yenu nina mtoto wa dada yangu anasumbuliwa sana na kifua, haipiti miezi miwili lazima atabanwa na kifua sana.

Baada ya uchunguzi ikaja gundulika baba yake anamatatizo ya pumu na kwakuwa ugojwa huu ni wa kurithi, basi amemuachia na mwanae.
Katika harakati za matibabu kuna nesi akamwambia sister pumu kwa hospitali haina dawa ila kuna mitishamba yaani dawa za kienyeji zinaponesha pumu na hasa akiwa bado mdogo.

Je kuna yeyote mwenye experiance na hili au amewahi sikia tufahamishane.
Nawasilisha.
Pole sana, inasadikika kuwa magome ya mti wa msufi ndio yanatibu huu ugonjwa,unaweza ku-google more info kwa kutumia jina hili Bombex Rhodognaphalon,mke wangu pia ameshudia kutibiwa na kupona kwa kuchemsha magamba ya mti huo,unatoa magamba ya nje,then gome la ndani unalitwanga,unakausha vipande,unapata unga,then ule unga unaweka kwenye uji, but I think hata ukishemsha na kunywa itasaidia
 
Pole sana mkuu, mimi nilikuwa na pumu lakini kwa sasa naona kama imepona ila kinachonisaidia ni kuepukana na mazingira sababishi kama yenye harufu kali, vumbi, nk
 
Ndugu inatibika,

I used to be asthmatic...Ilinitesa sana nilipokuwa mdogo, sindano za masaa, vidonge vile vya salbutamol, kukosa shule..afu baadae nilipokua kidogo zikaja hizi inhalers. Zilisadia wen i had an attack..lakini hazikuponyesha!

Siku moja rafiki yangu (tukiwa form 5 majengo sec. Moshi)akaniambia wewe na hizo dawa si utakuwa addict? akanipa stori ya brother ake alikuwa na pumu na hakutumia dawa yeyote!

The only thing alifanya ni kwenda gym, mazoezi ya kufa mtu na sasa ivi u will neva believe, amepona. So, nikasema y nt giv it a try maana mi nlichoka enzi izo unapiga PCM afu unashindwa kwenda shule, inauma!

Nikaingia gym, palepale maeneo ya Majengo kila siku..mdgomdogo (samtymz unakata tamaa), weekends naenda kukimbia au kucheza mpira uwanja wa ushirika (now MUCCoBS)..na bado kifua kilikua kinabana. But hata sijui nisemeje, after sometime, nilijikuta tu kimeacha! since then..trust me..sijapatwa attack yoyote na sijaacha mazoezi!

Observation:
Watoto wengi wenye pumu wanakuwa reserved and antisocial..hali hiyo inawafanya wasiparticipate in sporting and other extracurricular activities. Little do they know that their chests need the exercise to expand. So, kwa ushauri tu, hakikisha wanao wanafanya mazoezi frequently..wasiogope kupata ataack because in the long itaisha.

Hakikisha hawawi addicted!!! please!!! Nilipata wanafunzi wawili nilipoenda chuoni, yani wao wakipanda ngazi floor moja tu wanapuliza kale kakitu..mpaka nikawaonea huruma. but wao walikuwa beyond help! don't let your kid reach that stage..It can be controlled.
One last thing, check on their diet..more fat means more attacks!
Thanks.

*Above all, hakikisha unawaombea sana kwa Mungu maana yeye anaweza yote!

Methor,

Ushauri wako wa mwisho ndo naweza nikaafiki.

Ugonjwa wa Pumu hautibiki hospital hata kidogo, mimi ni mwathirika wa pumu tangu nizaliwe ila asthma yangu c ya kuattack km wengine coz sijawahi kutumia dawa yoyote ya hospital zaidi ya kuvaa makoti, kujifunika blanket,kuepuka matumizi ya vitu vya ubaridi na vumbi.

Naungana na aliyeshauri kwamba dawa za asili zinaponesha pumu.
 
Dawa ya Ugonjwa wa Asthma Au kwa jina la kiswahili inaitwa Pumu Upate kiazi cha figili cheupe uchanganye na Asali Safi mbichi kiazi cha figili kimoja Asali kipimo cha kikombe cha chai ukisage kile kiazi cha figili kwa kutumia mashine ya blender kile kiazi cha figili tia kidogo

sana maji ndani yake kipate kusagika kwa mashine ili kiwe kama uji mweupe kisha sagika kile kiazi cha figlii changanya na ile asali ya kipimo cha kikombe cha chai. Matumizi yake awe anakula kijiko

kimoja kila siku Asubuhi na Mchana na Usiku kutwa mara tatu Kabla ya kula kitu kwa muda wa siku 40. tafadhali kila inapokwisha uitengeneze hiyo dawa na usiache hata siku moja kuto kutumia ile

dawa yaani usiruke hata siku moja baada ya siku 40 matatizo yake yamekwisha huyo mtoto wako jaribu utanijuulisha matokeo yake asanteni.
 
Pole sana mpendwa unayeuguliwa na mtoto wa dada yako. Naomba na mimi nikupe experience yangu, nina mtoto wa miaka mitatu sasa alikuwa anasumbuliwa na pumu tena kali sana, alikuwa akipata mafua tuu basi lazima kifua kimbane, yeye ikimpata ilikuwa ni lazima apate sindano, nebulizer, salbutamol. antibiotic na antiallergy amabyo ni kali. Kwa kweli ilikuwa ni experience ngumu sana na wakati huo alikuwa na mwaka mmoja tuu.

Namshukuru Mungu, nilikuwa naenda naye kwenye maombi kila wiki na kumwombea sana na siku moja nikakutana na mtu akanieleza kuwa kuna daktari anayetibu na miti shamba. Kweli nilienda akanipatia dawa nikaipeleka kanisani kuoiombea na tangu amekunywa dawa hiyo ilikuwa ni mwaka jana Februari hajapata tangu kipindi hicho hajapata tena attack mpaka leo hii. Hata mafua hapati. Ila nilimpatia na nyingine kwa pamoja, ila huyo dada aliyenipa hapatikani tena kwa simu.

Dr anaitwa Chacha no 0684 729820 anakaa banana
 
Sasa dedam

kwanini usimsaidie mwenzako kama unamjua DR ambaye anaweza kutatua hilo tatizo kwa kumuelekeza huyo DR anapatikana wapi?
 
Wadau naombeni mawazo yenu nina mtoto wa dada yangu anasumbuliwa sana na kifua, haipiti miezi miwili lazima atabanwa na kifua sana.
Baada ya uchunguzi ikaja gundulika baba yake anamatatizo ya pumu na kwakuwa ugojwa huu ni wa kurithi, basi amemuachia na mwanae.
Katika harakati za matibabu kuna nesi akamwambia sister pumu kwa hospitali haina dawa ila kuna mitishamba yaani dawa za kienyeji zinaponesha pumu na hasa akiwa bado mdogo.
Je kuna yeyote mwenye experiance na hili au amewahi sikia tufahamishane.
Nawasilisha.
kwanza nakusalimu,kwa jina la mwenye'ezi, pili kila ugonjwa una dawa yake,lakin sisi waafrica ndio tunakasumba ya wazungu.ningekushauri uwasiliane na mimi vizuri,na inshalla kuna dawa ya pumu,dawa ya mitishamba,na mimi mwenyewe nimetumia na nashukuru mungu nimepona kabisa.na wengi wametumia hiyo dawa nao wamepona. RASAKA.
 
Mimi nimeugua pumu utotoni. Baba alinipeleka hospitali zote za wahindi (maana ni wazuri kwa haya magonjwa) sijuhi dr Khani sijuhi Dr Hashimu nakumbuka majina tu maana ilikuwa miaka ya 80. Wazazi wakaamua kuanza kutafuta waganga wa miti shamba. Well nimekunywa madawa ya kienyeji kiasi kwamba sijuhi nani kanitibu. Ila baba anajigamba kuwa mzee mmoja wa gongo la mboto ndo kanitibu na dawa yake anayochanganya na muwa. Kwa ufupi I am above 35 below 40 huu ni mwaka wa 20 sijawahi hata kupata kikoozi.

Madawa ya hospital hayasaidii kabisaaa. Yaani nilikuwa sisikii relief kabisa baada ya sijuhi sindano au vidonge mpaka ilifika kipindi nikiugua namwambia baba sitaki wkenda hoospital maana nilikuwa najua naumwa sababu ya hali ya mawingu (sijuhi nilikuwa sahihi) baada ya two thre days nilikuwa napata relief mwenyewe bila dawa nilikuwa nimekata tamaa kabisa.

Ushauri wangu, angaika na miti shamba from one mganga to another utapona ila hospitali ni zero!
 
RASAKA mimi pia ningependa kumjua huyo alokuponya maana nina niece wangu nae karithi huu ugonjwa. Mimi aloniponya hata kwake siwezi pakumbuka nilikuwa mdogo (around 15 years) na su=ijuhi kama yuko hai. Ila nina imani kubwa na miti shamba na naamini mtu unatakiwa ujaribu waganga tofauti mwisho unafanikiwa kwani mitishamba haina side effect

kwanza nakusalimu,kwa jina la mwenye'ezi, pili kila ugonjwa una dawa yake,lakin sisi waafrica ndio tunakasumba ya wazungu.ningekushauri uwasiliane na mimi vizuri,na inshalla kuna dawa ya pumu,dawa ya mitishamba,na mimi mwenyewe nimetumia na nashukuru mungu nimepona kabisa.na wengi wametumia hiyo dawa nao wamepona. RASAKA.
 
nimeidesea mahali.
LISHE YA MGONJWA WA PUMU (ASTHMA)
Baadhi ya vyakula vinavyoaminika kutoa ahueni na kuwa kama tiba kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na asali, juisi ya limau, mchanganyiko wa vitunguu swaumu na maziwa na mchangayiko wa abdalasini pamoja na asali. Vyakula hivyo vikiwa sehemu ya mlo wa mgonjwa kila siku, atapata ahueni ya ajabu. Pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mgonjwa wa pumu anatakiwa pia kula kwa kiasi kidogo mlo wenye matunda, mboga za majani na vyakula vingine vitokanavyo na nafaka ambavyo hutoa ‘alikalaini'.

Aidha, wagonjwa wa pumu wanatakiwa kujiepusha na ulaji wa kiasi kikubwa cha wali, sukari, mtindi (yoghurt), unywaji mwingi wa chai, kahawa, pombe na vyakula vote vya kusindika au kwenye makopo. Mgonjwa anashauriwa pia kufanya mazoezi ya kuvuta hewa safi na kuishi katika hali ya hewa isiyo na baridi, kunywa maji mengi mara kwa mara, kufunga kula (fasting) japo mara moja kwa wiki. Kwa kufuata masharti hayo, mgonjwa anaweza kuishi na pumu bila kusumbuliwa wala kutumia dawa kali kwa maisha yake yote. Pia unatakiwa kuepuka kufanya mazoezi kwenye baridi, epuka moshi wa sigara, dhibiti ugonjwa wa kucheua na kiungulia, epuka kukaa na wanyama na epuka kuishi katika mazingira yenye hewa yenye unyevunyevu.
 
Msada mada tajwa hapo juu madaktari wetu

Asthma (Pumu) ni ugonjwa sugu wa njia ya hewa ambao mara nyingi unajitokeza kama attack ambapo njia za hewa zinabana (bronchospasm) wakati unatoa hewa nje, na ndipo dalili zake kama kifua kubana, kushindwa kupumua na kasauti kama mluzi hivi (mara nyingi daktari akisikiliza kifua kutumia stethoscope anasikia) huwa kinatoka. Mara nyingi attacks hizi husababishwa na reaction kama allergy (asthma inabehave kama allergic reaction) kwenye vumbi, pollen, manyoya, hata hewa baridi mfano AC (allergens) etc.

Asthma ni ugonjwa wa kurithi, hauambukizi, japo kwa watu wachache inaweza ikatokea wakapata dalili kama za pumu kutokana na allergies mbali mbali kwenye njia ya hewa, lakini mara nyingi hii huwa haijirudii rudii kama kwa mwenye pumu ya kurithi.

Asthma haitibiki ukapona kabisaaa...ila huwa tunatibu zile attacks kuepusha kifo au madhara mengine makubwa ya njia ya hewa, kwa kutumia dawa ambazo zinaeffect ya kupanua njia za hewa (bronchodilators). Kuna dawa za spray (salbutamol inhalers), hizi waginjwa wa asthma wanakuwa wanatembea nazo, anapohisi kubanwa basi anaspray mdomoni na anaingiza ile hewa iliyochanganyika na spray mapafuni. Hii dawa ya salbutamol ina effect ya kupanua airways hivyo inamsaidia kuendelea kupumua vizuri. Wakati mwingine hizi inhalers zinakuwa zimechanganywa na steroids (corticosteroids) ambazo zina effect ya kustop allergic reactions hivyo kumsaidia mgonjwa hasipate attack.

Pia kuna dawa za vidonge kama salbutamol au aminophylline ambavyo vyote pia ni bronchodilator. Kama attack ikiwa kubwa sana ianbidi itibiwe hospitali chini ya uangalizi wa karibu kwa dawa za kuchoma (sindano) na nebulizer (kwa njia ya hewa) ambayo inakuwa na mchanganyiko wa bronchodilators, steroids na oxygen.
 
Hy jf mmbrz! Am new here..naombeni msaada kuhusu apopic dermatitis ama pumu ya ngozi..ntk kujua km huu ugonjwa huweza sababsha ngozi kuwa nyeupe?! Km ni hvyo naomba mnipe dalili nyinginezo za ugonjwa huo! Na jinsi ya kuutibu..
 
DAWA YA UGONJWA WA PUMU

Chukua kete kwa jina jengine soo zile zinazochezwa kwenye bao. Ivunje (crash) upate mbegu yandani. Saga hiyo mbegu moja upate unga wake na gawa huo unga sehemu 4. Tumia sehemu moja usiku wakati wakulala baada yachakula na asubuhi unapoamka kabla yachakula kwa nusu saa. Fanya hivi kwa muda wa wiki moja. Kwa watoto punguza dose.

MUHIMU:
Tumia dawa hii kiwango nilichoeleza koroga namaji glasi moja unywe pale pumu inapokukamata barabara na endelea kutumia mfululizo kwa muda wa wiki moja asubuhi na usiku.
 
Ndugu yangu niPM nikuelekeze dawa ya pumu. Nina ndugu yangu amepona kabisa. Huu sasa ni mwaka tangu apone.
 
Ndugu yangu niPM nikuelekeze dawa ya pumu. Nina ndugu yangu amepona kabisa. Huu sasa ni mwaka tangu apone.
Mkuu mambo ya kusema ni P.M hatutaki toa hapa hiyo dawa ya Pumu iliyomsaidia ndugu yako tafadhali. ukisema aku P.M na Mtu mwengine atakuja kusema kama ulivyo sema wewe mkishatimia watu kumi basi mumeshaharibu hii Thread maana yake. Tafadhali toa hapa ili na watu wengine wapate faida kama unaweza fanya hivyo la huwezi bora usichangie kabisa hii thread.
 
Mr. Masasi, PUMU (Asthma), Kubana kifua na matatizo mengine katika mfumo wa upumuwaji si MAGONJWA, ni Ishara tu za mwili kukuambia kuwa unapungukiwa maji kwa kuwa hatunywi maji ya kutosha siku hizi, mbaya zaidi tunasubiri kiu ndipo tunywe maji tena ya baridi!!!.

pumu, kuvimba mapafu na kuziba pua :


MAJI HUZUIA NA KUTIBU PUMU NA MATATIZO KATIKA MFUMO WA UPUMUWAJI:

Utajuwaje kuwa pumu ni ishara ya mwili kupungukiwa maji?


Tunapopumua, hewa huvutwa ndani ya mapafu wakati kiwambo (diaphragm), ambacho ni mfupa kinapokuwa kimejikaza kikivuta chini, kikiondoka kutoka chini ya mapafu na kutengeneza chumba ili mapafu yatanuke.


Mwendo huu hutengeneza uwazi katika mapafu yote, ukiyajaza hewa mapafu. Wakati kiwambo kinasinyaa huchupa nyuma juu kikisukuma hewa nje ya mapafu.

Hewa huingilia puani ambako huchujwa na kupashwa joto au kupitia mdomoni wakati pumzi nzito imehitajika.

Kwenye mzizi (nyuma) ya ulimi kuna kifuniko (valvu) kimetengenezwa kwa katileji iitwayo kidakatonge (kimio). Hiki ni kifuniko kinacholinda kisanduku cha sauti (larynx) ambamo bomba la upepo (trachea) ambalo ni tyubu kubwa huanzia. Kifuniko hiki kitajifunga wakati unameza chakula au ukinywa kimiminika, pia hubaki wazi wakati ukipumua hewa ndani au nje.

Tyubu hiyo kubwa (bomba la upepo) kisha imegawanyika katika matawi mawili yaitwayo vikoromeo (Bronchials) vilivyojishikiza katika kila pafu.

Pafu la kulia limegawanyika katika sehemu tatu (lobes) wakati pafu la kushoto ni dogo kidogo na limegawanyika katika sehemu mbili (lobes). Madaktari wanaweza kuondoa sehemu moja na pafu bado linaweza kuendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kikoromeo (Bronchial) kisha kimegawanyika katika tyubu ndogondogo ziitwazo neli neva za umio (Bronchioles). Kilichojishikiza mwishoni mwa neli neva za umio ni mkusanyiko wa vifuko vya hewa viitwavyo Alveoli.


Kila kifuko cha hewa (alveoli) kimezungukwa na kapilari za damu ambamo ubadilishanaji wa hewa hutokea. Upande mmoja wa kifuko cha hewa oksijeni huingizwa ndani ya damu na upande wa pili wa kifuko hicho hicho cha hewa, gesi chafu iitwayo kabonidayoksaidi hutolewa.

Kabonidayoksaidi ni taka toka katika seli zetu zinazounguza oksijeni na chakula na kutengeneza nguvu na kutuwezesha kuishi.

Vifuko hivi vya hewa (alveoli) lazima vibaki na unyevunyevu ili ubadilishanaji wa hewa uweze kufanyika. Vifuniko hivi havijazwi maji, bali kuta au usawa wake wa ndani lazima uwe na unyevunyevu ili ubadilishanaji wa hewa uweze kutokea.

Maji huzifunika sehemu za ndani za vifuko vya hewa na unyevu huu (surface tension) unahitajika ili kuwezesha kabonidayoksaidi kutolewa nje. Unaweza kuuona unyevunyevu huu (fog) kwa kuhema juu ya miwani ya jua au kioo chako.

Unapoteza glasi nne (4) za maji kila masaa 24 kwa kupumua tu.

Kila seli ndani ya mwili huwa na maji na lazima iwe na maji ili kubaki katika afya. Damu yetu ina asilimia 94 ya maji, ubongo wetu una asilimia 85 za maji na ogani na tishu zingine zina asilimia 75 ya maji.


Maji mengi kuzidi mwilini ni hatari kama ilivyo kwa chumvi nyingi kuzidi mwilini. Lazima kuwe na usawa wa chumvi ili kuhimili ujazo sawa wa maji ndani na nje ya seli kwa mujibu wa dr.Batmanghelidj.

Mahospitalini madaktari hutoa dripu la maji la lita moja lenye gramu 9 za chumvi ndani yake.

Ikiwa mtu anakunywa maji mengi na hatumii chumvi ya kutosha, maji yatakimbia kwa haraka nje ya mwili hivyo kutokuzipa seli za mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo. Yanaweza pia kutoa nje ya mwili madini na vitamini mhimu.

Hakuna mtu amewahi kupewa dripu la maji matupu bila chumvi hospitalini. Wanasayansi, wanakemia na madaktari bado hawaelewi ni kwa namna gani chumvi huyeyuka ndani ya maji na kuendelea kuyafanya maji kuwa na uchumvi na uchumvi kama maji ya bahari.

Dr. Batmanghelidj ameandika vitabu sita akielezea umhimu wa maji na chumvi. Kitabu kimoja kinaitwa: Asthma, Allergies and Lupus. Kitabu hiki kinafafanua namna magonjwa ya kuvimba mapafu (Emphysema), pumu (asthma) na kuziba pua (chronic obstructive pulmonary disease) yanavyojitokeza mwilini wakati mtu anapokuwa hana maji ya kutosha mwilini na ubongo kutuma ujumbe kwa mapafu ukiyaambia kubana matumizi ya maji.

Wakati mapafu yanaanza programu ya kubana matumizi ya maji yanaweza kuzarisha ute ute na makohozi na kurundika katika neli neva za umio ili kuibana njia ya kupitia hewa na hivyo maji machache yatoke nje kwa njia ya mvuke wakati tunapumua nje ndani.

Ute na makohozi hushikamana na hivyo kuendelea kubaki hapo, pia huwa na unyevunyevu ili kufanya tishu laini zisikauke, zisipate nyufa na kutokwa damu.

Watu wenye pumu/asthma hudhibiti hali zao kwa kumeza dawa kila siku na kutumia vipumuzi (inhalers) wakati neli neva umio (Bronchioles) zimejibana (draw up) na tishu za ndani zinapokuwa zimeumuka (swolen) zikibana zaidi njia ya kupitia hewa na kusababisha shambulio la maisha katika kupumua.

Kwa kawaida shambulio la maisha hutokea wakati unafanya mazoezi au muda mfupi baada ya kula. Kwanza kikohozi kikavu huanza, kisha kupumua kwa shida hufuatia (wheezing), kukifuatiwa na tishio la maisha ukihangaikia kupumua ikiwa kipumuzi (inhaler) hakikutumika.

Wakati unafanya mazoezi unapoteza maji kwa njia ya jasho (perspiring), na kupelekea mishipa kuhitaji maji zaidi. Upotevu huu wa ziada wa maji unaweza kupelekea mapafu kujifunga zaidi na kusababisha kifo ikiwa kipumuzi hakitachukuliwa kuzuia mapafu yasijifunge.

Wakati unakula, mwili wako huelekeza mtiririko wa damu katika utumbo mdogo sambamba na maji ya ziada yanayohitajika kukishughurikia chakula. Baadhi ya vyakula huhitaji maji zaidi ili kushughurikiwa (kumeng'enywa) kuliko vingine.


Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji na umekula chakula kinachohitaji maji mengi ili kimeng'enywe, basi, mwili unaweza kukopa maji toka katika mapafu na kukusababishia shambulio la pumu mara tu kisha kula.

Inashauriwa kwa kila mtu mwenye pumu au kuvimba mapafu kunywa ml 250 (robo lita) za maji kabla ya kula chakula chochote na kunywa kiasi kidogo cha maji wakati ukiendelea kula chakula.

Dr. Batmanghelidj pia anasema watu wenye pumu wanaweza kuhitaji kiasi kidogo cha chumvi zaidi kwa muda ili kusafisha ute ute na makohozi mpaka mapafu yatakaporudi katika hali yake ya kawaida kama anavyofafanua katika kitabu: ABC of Asthma, Allergies and Lupus ukurasa wa 144.

Kamwe usinywe zaidi ya glasi mbili za juisi ya chungwa kwa siku ikiwa unasumbuliwa na pumu au una tatizo lolote katika mfumo wa upumuwaji. Kumbuka pia kutumia robotatu gramu za chumvi ya baharini katika kila robo lita ya juisi yako ya chungwa.

Haya ni mazingaombwe rahisi yanayohitaji kuongeza kiasi cha unywaji maji wakati mwili unapopungukiwa maji.
Dr.Batmanghelidj anasema; 'hii ndiyo sababu pumu si kitu kingine zaidi ya upungufu wa maji, pumu si ugonjwa'.

Kabla ya kuamua lolote kuhusu tiba kwa kutumia maji, tafadhari soma vizuri: mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza tiba ya maji katika; maajabuyamaji2.artisteer.net
 
Msada mada tajwa hapo juu madaktari wetu

''Asthma haitibiki ukapona kabisaaa...ila huwa tunatibu zile attacks kuepusha kifo au madhara mengine makubwa ya njia ya hewa, kwa kutumia dawa ambazo zinaeffect ya kupanua njia za hewa (bronchodilators) - Dr. RIWA''. Hivyo ndivyo alivyoandika daktari wetu mpendwa dr.Riwa katika kuchangia thread hii.

Kwanini huwezi kupona kabisa pumu?, ni kwa sababu Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa.

Siyo pumu pekee isiyotibika kabisa. Watu wengi wenye Mzio (allergy), shinikizo la damu (BP), kisukari (diabetis), Upungufu wa kinga mwilini (ukimwi) na magonjwa mengi wanabaki nayo katika safari yao ya kuishi. Dawa nyingi hospitali hupunguza maumivu na kuahirisha tatizo kidogo lakini mwili utaendelea kuleta ishara (magonjwa) za kupungukiwa maji moja baada ya nyingine mpaka hapo utakapoupa mwili kile unachokihitaji.

Ni dhana ya zamani kusubiri kiu ndipo unywe maji na huku unajuwa kuwa maji ni uhai. Kwa kutumia maji watu wengi wamepona kabisa pumu na kusahau kutumia inhalers. Tembelea maajabuyamaji2.artisteer.net ujifunze namna ya kunywa na kutumia maji ili kujitibu ugonjwa wowote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom