Mimi ni mdau wa afya...kwa taaluma yangu nafahamu kuwa hakuna tiba ya Pumu (kwamba haitibiki ikakoma isitokee tena). Pumu inafanana na allergy jinsi inavyotokea, kunakuwa na kianzishi (allergen/trigger) halafu njia ya hewa ina'respond' kwa kubana haswa wakati wa kutoa hewa nje. Kikohozi na mafua ni moja ya vianzishi. Wakati mwingine Pumu inaweza ikaacha yenyewe (hasa inayoanzia utotoni) lakini sio mara zote.
Dawa zilizopo sasa na kupatikana hospitali au madukani husimamisha 'attack' inapotokea kwa kupanua njia za hewa ili mgonjwa apumue kawaida, hazitibu kuponyesha tatizo moja kwa moja.
Sijasikia bado dawa ya kienyeji iliyothibitishwa kuwa inapunguza kutokea kwa pumu au kutibu pumu kabisa. Kwa maelezo zaidi unaweza kwenda Muhimbili kitengo cha dawa asilia watakufahamisha.
Before cjakupa ushauri zaidi kwa sasa anatumia dawa gani? Je ana umri gani? I have two asthmatic kids so i have little advice for you.
Pole sana.
ana miaka mitatu, mwanzoni kabla ya kujua alikua akibanwa tunaenda hospital daktari akimcheki anasema nimonia anamuandikia kristapeni sindano za masaa,nadhani unajua zinavyouma, amechoma sana hadi makalio yana vinundu kwa ndani.
Baada ya kujua sasa akibanwa anaandikiwa salbutamol syrap inamsaidia sana.
magome ya msufi achemshiwe na kupewa kwa siku zaidi ya mara mbili. (anywe kama anavyokunywa maji haina madhara) na atapona kabisa kama ni mtoto hata kama inasababishwa na mzio. Kwa mtu mzima inapunguza tu kasi ya shambulizi
well,poleni sana.
Salbutamol ni nzuri kama itabidi inabid aanze kutumia inhalers. Watoto wangu walianza kutumia inhalers walipokua na miezi tisa. Yao ni mbaya sana huwa wanabanwa mpaka wanawekwa kwenye nebulizer. Ni beta umcheki dr,kama upo dar naweza kukuelekeza dr mzuri sana.
Kitu kingine kilichowasaidia watoto ni dawa ya pumu nilinunua pale muhimbili tradition clinic. Tangu walipotumia imepunguza frequency of attacks.
Halafu mjitahidi sana kuondoa vumbi la ndani ya nyumba,mapazia,vitanda,matres iwe covered na kitu ya plastic kuzuia vumbi. Manukato kwenye sabuni,mafuta,dawa za kudekia,air freshner,perfumes.angalieni vyakula anavyokula unaweza kuta vina allergens
kuna bibi mmoja anaitwa bi mbaazi,alitibu pumu yangu nilivyokuwa mdogo,sasahivi sina tena pumu,kuna maji(sijui ya nini) anakupa kwenye chupa unakunywa mara tatu kwa siku,anaweza kukaa miaka bila ya kupata tena pumu, au isirudi kabisa.
I'm almost 30 and at that time i was between 10 and 14 years old.
sijui sasahivi anaishi wapi, ila mara ya mwisho kumuona ni kwenye michezo ya kuigiza ya mzee janguo,mtafute mzee janguo akwambie huyo bibi anapatikana wapi. nakwambia hivi kwasababu aliitibu pumu yangu
nadhani kuna misufi miwili mitatu maeneo ya Kinondoni, na pia maeneo ya ukonga ipo. lakini mingi zaidi ilikuwa maeneo ya Kawe na Lugalo humo kama bado imo sijui unafanyaje!!!Pia pale karibu na Drive-in cimena zamani sijui siku hizi pana jina gani vile!? (Yale maji wanayopewa watu na wakapona na kupata nafuu kubwa - ndio hiyo dawa yenyewe ila huwa wanaifanya siri ili biashara iendelee) Akishapona mwanao nawe wasaidie wengine mkuu.Noted.
Hivi dar misufi inapatikana kweli?
Wadau naombeni mawazo yenu nina mtoto wa dada yangu anasumbuliwa sana na kifua, haipiti miezi miwili lazima atabanwa na kifua sana.
Baada ya uchunguzi ikaja gundulika baba yake anamatatizo ya pumu na kwakuwa ugojwa huu ni wa kurithi, basi amemuachia na mwanae.
Katika harakati za matibabu kuna nesi akamwambia sister pumu kwa hospitali haina dawa ila kuna mitishamba yaani dawa za kienyeji zinaponesha pumu na hasa akiwa bado mdogo.
Je, kuna yeyote mwenye experiance na hili au amewahi sikia tufahamishane.
Nawasilisha.
yupo DR mmoja anatibu pumu kwa kutumia dawa za kisasa na inapona kabisa nimeshuhudia watu wengi wakipona