Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Ngiri.

Discussion in 'JF Doctor' started by God bell, Sep 30, 2011.

 1. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF niko serious na wala ctanii, na naombeni mnipe ushauri utakaonisaidia mwenzenu. Imetokea kuwa nasumbuliwa na ugonjwa wa ngiri na hapa nilipo nackia maumiv c kawaida. Imepelekea mpaka sehemu 1 ya yai la kushoto kwenye uume ina mishipa yenye uvimbe najihic ni utumbo umezama huko nikishika. Nilienda hsptl doctor akanipa 2 vidonge ambavyo havikunisaidia. NAOMBENI USHAURI KWA ANAEJUA DAWA YAKE NIWEZE KUPONA MANAKE NIMEKATA TAMAA YA KUPONA. Nakaribia mwaka nikiwa na haya maumiv.
   
 2. s

  stan b Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hiyo ndugu yangu dawa yake ni opreshen, hlo ni tatizo ambalo wanaume wengi huzaliwa nalo, gharama yake si chin ya elfu 50, baada ya opreshen huitajik kufanya tendo la ndoa miezi 6 wala kaz ngum. uckubal kudanganyika na dawa za kienyeji onana na madaktar hospital kubwa za serkal.
   
 3. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu kwa ushauri.
   
 4. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Pole sana,wengi hupona kwa upasuaji so nenda hospitari.
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,839
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  jitahidi kuzingatia hapo kwenye red
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,001
  Likes Received: 4,289
  Trophy Points: 280
  Ndugu God bell,
  Pole kwa maumivu.

  Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'

  Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.

  Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.

  Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
  Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.

  Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
   
 7. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ubarikiwe mkuu kwa ushauri wako mzuri.
   
 8. P

  Piscine Member

  #8
  Oct 4, 2014
  Joined: Sep 28, 2014
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Vp inauhusiano nakupungua nguvu za kiume kabla na baada ya upasuaji?
   
 9. Hunyu

  Hunyu JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2014
  Joined: Aug 19, 2014
  Messages: 1,893
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimeuona huu uzi nisaidie pia. Mimi ilitokea zamani sana nilipigwa na barid kali nikahikuta sehemu moja ya kende haipo nadhani ilizama ndani. Nafanya sex kama kawaida sisikii maumivu yeyote. Sina hakika kama ilizama au ilisinyaa maana nilikuja kusitukia tu nina nanii moja.

  Naomba ushauri tafadhari na jee hali hii ni hatari kiasi gani
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Oct 5, 2014
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,001
  Likes Received: 4,289
  Trophy Points: 280
  Kabla sijajibu swali lako naomba niweke sawa manenoya Kiswahili ili twende pamoja.

  Ashakumu si matusi, natangauliza msamaha kwa lugha yenyeukakasi. Si makusudi ni katika elimu,hakuna namna nitakayoeweka vizuri kamasi kuweka mambo haya bayana.

  Kwanza, lile fuko lote ndilo linaitwa pumbu kwa lugha yetu.
  Zile tembe zinaitwa hasua, korodani au kende. Matumizi ya maneno hayayanategemea umri kwa lugha fasaha.


  Mfano, wazee na watu wa makamu watasema wana matatizo katika hasua.
  Vijanawatasema korodani, na chini ya miaka 16 ni kende, na chini ya hapo ni tembe
  au ndude.
  Watoto wdogo wa miak 6 au chini ksema ana tatizo lakorodan, hasua, pumbni tusi, ugha njema ni ndude au tembe

  Sijui una umri gani, naomba ufanye selfservice ya sehemuinayokufaa.
  Kuhusu tatizo lako, kimaumbile korodani, hasua n.k. hupandana kushuka kutoka katika fuko lile kubwa.
  Lile fuko hurekebisha joto la mwiliili kulinda uharibifu unaoweza kutokea kwa zile bidhaa laini


  Wakati wa baridi hupanda juu na wakati wa joto huteremkakama kupunga upepo.
  Ni mambo ya kawaida kifiziojia

  Kwa upande wako, hiyo mojailiyopanda na kutoweka ni tatizo.
  Kwa kawaida hupanda zote na kuremeka kwapamoja kwakuwa zinafanya kazi kwa muundo sawa.


  Sioni tatizo la haraka la tishio la maisha. Ninachokona nimatatizo ya kibaolojia.
  Athari zake hazipo wazi hadi itakapofahamika kwaninimoja imekwama huk darini

  Na hapo ndipo nina concern kuhusu uzazi tu, na hiyo haina maanahutafanikiwa.


  Ni sawa na kutembea na gari shock absorber moja imevunjika.Gari litakwenda, lakini je ni njia sahihi ?
  Na je hatuhitaji kwenda gerejikurekebisha?


  Kwa mukatadha naomba ukamuone mtaalamu wa mambo ya njia zamkojo, Urologist nina uhakika ataweza kutanzua kitandawili chako. Hata hivyohakuna hofu kwa sasa.  cc Ritz
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...