Ugonjwa wa Mifupa (Arthritis)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Arthritis ni nini?

Ni ugonjwa unaofanya viungo vyako kukauka na kuwa vigumu kuvisongesha kwani ukifanya hivyo, utasikia uchungu. Hali iliyo kawaida na kujitokeza sana sana ile inavamia viungo (Osteoarthritis) na ile inaathiri mwili mzima na kuufanya uvimbe ama kuleta mwasho viungoni. Mara nyingi, ugonjwa huu huwa haujitokezi bayana hadi pale ambapo mtu hufikia miaka arobaini au zaidi.

Ni nini dalili za ugonjwa huu? (Osteoarthritis)

Maumivu ya viungo baada ya mtu kufanya mazoezi ama shughuli za kutumia nguvu
Ugumu kwenye mikono, magoti, nyonga ama mgongo baada ya mtu kukaa kwa muda bila kusonga
Viungo kuvimba na kuwa vidhaifu na vyororo
Viungo kugongana na kutoa sauti mtu anajaribu kutembeatembea

Rheumatoid Arthritis

  • Viungo vyenye maumivu makali vyenye kukauka
  • Viungo kuwa na joto, vyekundu na kuvimba
  • Mtu kuwa na joto
  • Kuhisi mchovu na mdhoofu
  • Kukosa hamu ya chakula
Hutibiwaje?

Muone daktari kisha akufanyie uchunguzi. Unaweza kupata matibabu ya kumaliza maumivu na kufanya mazoezi ya kufanya viungo viwe vyepesi.

Source: Mzizimkavu
 
Ukiwa kama mtaalam wa tiba mbadala, unashauri watu watumie nini kujikinga na ugonjwa huu? Kuna vyakula au mitishamba inayoweza kusaidia?
 
mkuu hakuna tiba mmbala maana naona ni ugonjwa wa utu uzima ambao mii nipo jirani nao sana.kama kuna tiba mmbadala tuwekee mkuu. nimeku pm mkuu nipe msaada mkuu
 
Degenerative diseases mara nyingi zinaambatana na kurithi kinasaba (genetics).Kama kwenye ukoo wenu kuna wenye kuathirika zaidi na hali hii basi chances are nawe utapata zahama hiyo. Kwenye arthritis inashauriwa kuchunga uzito maana huu huweka tension hasa kwenye mifupa ya magoti kusuguana na kuleta maumivu. Utu uzima unapoingia utaumia zaidi kuliko yule aliyechunga uzito wake.Mazoezi pia ni muhimu.Wanawake hasa wenye umri mdogo kunyweni maziwa na kutumia calcium supplements maana wanawake hupata athari zaidi hasa wafikiapo menopause kwa vile mifupa huanza kuwa hafifu.
 
taya la chini halitembei baada ya kung'oa jino likiambatana na maumivu makali chini ya sikio tatizo nini dokta
 
Back
Top Bottom