Ugonjwa wa midomo na miguu (umm) - foot and mouth disease (fmd)

achengula

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
369
62
UMM ni ugonjwa wenye maambukizi makubwa unaowapata ng’ombe, nguruwe, kondoo, mbuzi na nyati na ni ugonjwa mgumu sana kukabiliana nao. Kwa ujumla ni ugonjwa unawapata wanyama wote wenye kwato mbili wa kufugwa na wanyama pori. Dalili kubwa za ugonjwa huu ni homa, malengelenge (vesicles) mdomoni na puani, chuchu, kwato/nyayo, na vifo kwa wanyama wadogo.
Madhara –Ugonjwa huu unasababisha upotevu mkubwa wa kiuchumi kwa sababu ya vifo vya wanyama wadogo, kupungua kwa uzalishaji (maziwa, nguvu kazi, na kuzaliana) na kuzuiwa kwa biashara ya nyama na mazao ya mifugo ndani na nje ya nchi husika.


Kwa maelezo zaidi juu ya ugonjwa huuu na magonjwa mengine soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
Back
Top Bottom