Ugonjwa wa mafua ya ndege watangazwa janga la kitaifa Tanzania

HOMA YA MAFUA YA NGURUWE (SWINE FEAVER)
KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 8 kipengele cha (i) sehemu (b) inasema “Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa demokrasia na haki ya jamii; kwa hiyo lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa Wananchi”
Hii ina maana kuwa Serikali ina malengo mengi lakini lengo kuu ni kuhakikisha jamii inapiga hatua katika nyanja zote za maendeleo, na maendeleo hayo yalete tija na ufanisi kwa wananchi wenyewe na si kwa watu wengine.
Ndio maana Katiba ikasema lengo kuu la serikali ni USTAWI WA WANANCHI na si ustawi wa wawekezaji kutoka Marekani au Ulaya. Wala si kwa ustawi wa chama tawala bali ni kwa ustawi wa wananchi.
Sasa ikiwa ndivyo inakuwaje wawekezaji wa sekta ya madini nchini wachukue 97% ya faida ya madini na wananchi (kupitia serikali) kuambulia 3% tu kama mrahaba (cammision)? Hivi hapa kuna ustawi wa wananchi au ustawi wa wawekezaji.?
Serikali ya awamu ya tatu ilibinafsisha mashirika mengi ya umma na wananchi walipojaribu kuhoji walikemewa huku serikali ikisisitiza kuwa “Ubinafsishaji ni kwa manufaa ya umma”
Mwaka 2001 Shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) lilibadilishwa menejimenti kwa kampuni isiyo na uwezo ya Nett-Group Solutions ya Afrika Kusini, na wafanyakazi kulazimishwa kusaini mkataba mpya wa kazi. Walipojaribu kuhoji aliyekuwa waziri wa Kazi maendeleo ya vijana na michezo kwa wakati huo Prof.Juma Kapuya akanukuliwa na vyombo vya habari akisisitiza kuwa ambaye hatatia saini mkataba huo atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe.
Maskini: Watanzania wengi wakalazimishwa kuicheza ngoma wasioijua. Wakasaini mkataba ili kulinda vibarua vyao.
Serikali haikuishia hapo, ikazidi kuingia mikataba na wawekezaji kutoka nje, na kuzidi kubinafsisha mashirika ya umma na wananchi walipojaribu kuinua ndimi zao na kuhoji, kama kawaida serikali ilirudia kile kibwagizo chake cha siku zote kuwa “ubinafsishaji ni kwa manufaa ya umma”.
Hivi umma ni nani kama sio Wananchi? Na Wananchi wanapohoji maana yake ni kuwa hawajui na wanataka kueleweshwa wajue. Kama kweli Ubinafsishaji ni kwa manufaa yao kwanini wasjibiwe ipasavyo.?
Serikali ya awamu ya tatu ilijikita zaidi katika ubinafsishaji wa mashirika ya umma japo umma wenyewe haukushirikshwa.
Wakati mwingine matumizi ya nguvu na ubabe yalitumika kutekeleza azma ovu iliyokuwa imedhamiriwa na viongozi hawa wa Serikali. Pamoja na serikali kupewa 3% tu kama mrahaba na kampuni zinazochimba madini nchini, lakini bado Serikali iliendelea kuzikingia kifua kuwa eti ni kwa “Maslahi ya umma”
Mwaka 2001 wakati Rais Mkapa akifungua rasmi mgodi wa Bulyanhulu uliopo Kahama Shinyanga alinukuliwa akisema “Wanaopinga sera ya uwekezaji katika migodi ni wenye uchovu wa akili……….” Kwa tafsiri nyingine ni wehu, mataahira au wendawazimu wasiojua wanalopinga.
Kwa maana hiyo mtu yeyote atakayejaribu kupinga Serikali kupewa 3% tu ya faida katika madini, basi moja kwa moja atakuwa amejiingiza katika hilo kundi la Mkapa la “wachovu wa akili”
Maskini! Kumbe mhe.Zitto Kabwe nae ni “mchovu wa akili”. Dr.Slaa nae! Akina Selelii na wenzake nao ni mataahira.! Haah! Kumbe hata Engineer Stella Manyanya nae ni mwendawazimu (kwa mujibu wa Mkapa).
Ndio. Wote ni vichaa. Ni kivipi wataacha kuonekana wehu wakati wamekuwa mstari wa mbele kpinga uwekezaji usiojali maslahi ya Watanzania hususani katika sekta ya madini.!
Mikataba mingi ya uwekezaji iliyosainiwa wakati wa Serikaliya awamu ya tatu imegundulika kuwa haikuwa inamnufaisha Mtazania kwa namna yoyote ile. Zaidi sana ilizidisha unyonyaji na kupalilia mmea wa Ukoloni mamboleo. Iweje wachimbe madini yetu, tena kwenye ardhi yetu kisha watulipe 3% tu ya faida? Hakika hii haingii kabisa kwenye ubongo wa mtu mwenye akili timamu.
Sasa kama miradi hii inaonekana haina tija kwa taifa ilikuwaje wakati inasainiwa tuambiwe “ni kwa maslahi ya umma?”
Hivi “Umma” ni nani hasa?? Lakini nimegutuka kuwa ule “umma” uliokuwa ukipewa maslahi sio umma ule tuliouzoea yaani wananchi (majority).
“Umma” uliokuwa ukitajwa ni kundi la vigogo ndani ya Serikali waliokuwa wakinufaika na mikataba hiyo kandamizi. Umma ulikuwa viongozi wa serikali.
Hivi, kama Mkapa aliweza kujibinafsishia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, tena kwa kujiuzia chini ya 10% ya gharama halisi, angewezaje kupinga kuwa ubinafsishaji si kwa maslahi ya umma?
Alipokuwa akihutubia kuwa “ni kwa Maslahi ya umma” alijua alichokimaanisha, kwa kuwa hata yeye alikuwa sehemu ya huo “umma”
Cha ajabu wabunge wenye uchungu na nchi hii (hasa wale wa upinzani) wanapojaribu kuhoji Serikali inawajibu hovyo hovyo (rejea majibu ya waziri Sumari kwa Dr.Slaa kwenye kikao cha mwezi July 2008). Lakini mara nyingine wabunge hawa shupavu huzomewa (hasa na wale wa chama tawala), na wanapohoji zaidi hufukuzwa nje ya vikao vya bunge eti wamekiuka kanuni. (rejea kisa cha Zitto Kabwe kufukuzwa bungeni kutokana na kuhoji mgodi wa Buzwagi)
Lahaula! Kumbe bungeni kuhoji mambo yanayohusu mustakabali wa taifa lako ni kukiuka kanuni?
Ila wasife moyo kwani hata muasisi wa Taifa hili Mwl.Nyerere aliwahi kusema kuwa “….nchi hii itajengwa na wenye moyo lakini italiwa na wenye meno”. Lakini mimi naamini ipo siku isiyo na jina wala saa “kabla hajarudi mwana wa Adamu” wenye moyo watawashinda wenye meno. Na hapo ndipo kutakapokuwa na “kilio na kusaga meno”.
Maamuzi sahihi huja kwa fikra sahihi. Umefika wakati wa kupinga kwa nguvu zote uovu na unyonyaji wa namna yoyote ile unaofanywa na viongozi tuliowakabidhi dhamana za maisha yetu lakini wao wakachezea kamari. Inashangaza kuwa Watanzania wanauona uovu huu lakini wananyamaza kimya kana kwamba mambo haya yanatokea China au Mexico na si hapa kwetu.
Napoona hali hii nakumbuka kauli wa aliyekuwa gwiji wa Fizikia na Hisabati duniani, Albert Einsten aliyepata kusema kuwa “Duniani pamekuwa mahali hatari zaidi pa kuishi. Si kwa sababu ya kuwepo kwa watu wengi ambao ni waovu; bali kwa sababu ya kuwepo kwa watu wasio waovu lakini hawachukui hatua yoyote dhidi ya uovu”
Umefika wakati wa kukataa na kukemea waziwazi utawala usiojali maslahi ya wananchi. Kuwakataa na kuwapiga vita viongozi wote wanaohubiri demokrasia ya uongo huku wengi wao ni wanafiki. Tuwakatae na tuwapige vita usiku na mchana , kwani wanatisha kuliko Homa ya mafua ya nguruwe (Swine feaver). Ni heri homa ya nguruwe japo inaenezwa kwa hewa lakini haijatapakaa kila mahali, kuliko viongozi hawa wanaojieneza kwa mwavuli wa demokrasia lakini wametapakaa kila kona ya nchi.
Hakika hawa wanatisha kuliko swine feaver!!

Niachie ujumbe-
0712-025958
0715 187677
 
Niachie ujumbe 0712-025958
0715-187677

Back
Top Bottom