Ugonjwa wa kusahu kwa msichana-ma Dr.naomba msaada!

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
481
145
Ma Dr na wana JF wenzangu-natanguliza heshima,
Nina mtoto ambaye sasa ana umri wa miaka 18,msichana na amemaliza kidato cha 4 kwa kushindwa mtihani -div.0.
Tatizo lake nimeligundua baada ya wazazi wake kunipa nikae nae ,ametokea kijijini.
Kusahau kwake ni kwa ajabu; Ukimpa kwa mfano glass ukamwambia -tafadhali peleka glass hii usiiweke kwenye kabati, basi yeye atachukua glasss hiyo na kuiweka kwenye kabati.

Au ukimwambia tafadhali leo usiende mjini,yeye atakwenda na ukimuuliza nilikwambiaje atasema nilisikia unasema leo niende mjini.

Je huu ni ugonjwa gani au kuna tiba gani ambayo inabidi nimfanyie na kwa sababu niko DSM nina uwezo wa kumpeleka hospitali yoyote au kwa Dr.yoyote kwa haraka.

Lakini vitu vingine vyote ambavyo vingefanya kuonekana labda ana matatzio kama ya ukichaa anafanya kawaida eg. kujifanyia shughuli zake, kujipendezesha kupika na kukaa na watu anafanya.
Natanguliza shukurani kwa atakayenijibu hapa au kwa kutumia email rakeyescarl@yahoo.ie
Rakey.

 
Atwange Dawa moja inayoitwa Halilaji achanganye na Asali Safi mbichi ya nyuki

kijiko kimoja kikubwa awe anakunywa kila siku katika maisha yake. Au Apate Mafuta ya siku nyingi ya

Zaituni ajipake nyuma ya kichwa upande wa kichogoni awe anajipaka kila siku inasaidia sana hayo mafuta ya Zaituni ya siku nyingi

kupoza ugonjwa wa kusahau. Na ingine awe anakula Sana Figili na Samli Safi ya Ng'ombe.

itamsaidia kuondosha ugonjwa kusahau. Au ale Zabibu kavu kwa wingi kila siku hiyo pia itamsaidia kuondosha huo ugonjwa wa kusahau.
ukitaka Dawa zaidi wasiliana na mimi kwa njia ya email yangu ni hii (fewgoodman@hotmail.com) .@rakeyescarl
 
Back
Top Bottom