Ugonjwa wa kiharusi/ kupooza (stroke): Kinga, tiba na jinsi ya kukabiliana na maradhi haya

ni ya kupanda
Kama ni Maradhi ya Presha ya kupanda High Blood Pressure mwambie mama yako awe

anatumia kila siku asubuhi kabla ya kula au kunywa kitu ale punje mbili za kitunguu Saumu avitafune na kumeza na maji na akae kama

saa moja ndio anaweza kula mlo wa asaubuhi. Na mchana afanye hivyo hivyo na usiku hivyo kwa muda wa siku 3 kisha mwambie aende

kupima atakuta hiyo Presha ya kupanda itashuka tu inshallah. Atumie kisha uje hapa unipe Feedback.
 
KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI


attachment.php


SOTE tunajua ugonjwa wa kiharusi (stroke) ni miongoni mwa magonjwa hatari kwani ukikupata unaweza kudhoofisha baadhi ya viungo vyako vya mwili kama siyo vyote na kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za kawaida na kuwa mtu wa ndani tu kwa maisha yako yote.



Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.

Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na

pilipili. Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.

Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi hufariki dunia nchini humo kutokana na

kiharusi kwa idadi sawa na wale wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Utafiti mwingine katika eneo hilo umeonesha pia kuwa wanaume wana hatari kubwa zaidi ya kufariki dunia au kupatwa na matatizo mengi kutokana na ugonjwa wa kiharusi kuliko

wanawake. Hivyo kati ya wanaume na wanawake, wanaume zaidi ndiyo hupatwa na kiharusi au matatizo yatokanayo na ugonjwa huo kuliko wanawake.


Utafiti huu mpya umeendelea kuthibitisha ukweli wa siku zote kuwa matunda na mbogamboga hutoa kinga katika mwili wa binadamu dhidi ya magonjwa mengi hatari,

hivyo wito umetolewa tena wa watu kupenda kula matunda na mbogamboga hasa nyanya, matikitimaji pamoja na pilipili ambavyo vimeonekana kuwa na kinga kubwa zaidi mwilini.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya matokeo ya utafiti huu, watu wamekumbushwa umuhimu wa kuendelea kula na aina nyingine ya matunda, kwani kila tunda au mboga

ya majani ina faida na umuhimu wake katika mwili wa binadamu.
Mwisho imeelezwa kuwa ulaji wa nyanya za aina zote una faida, iwe ni ile inayopikwa pamoja na mboga au ile inayoliwa ikiwa imeiva bila kupikwa. Ni vizuri kuchangamkia ulaji

wa vitu kama hivi ili kuipa miili yetu uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi hatari, yakiwemo yale ya saratani ambayo kwa kiasi kikubwa huweza kuzuiwa kwa kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali.


 

Attachments

  • tomato.jpg
    tomato.jpg
    37.6 KB · Views: 3,767
Mkuu MziziMkavu, asante sana kwa kuendelea kutupa elimu ya mambo mengi.Mwenyezi Mungu azidi kukujalia afya njema na nguvu.
 
Wanajamiiforum nahitaji msaada wa hospital nzuri au daktari mzuri hapa Dar wa ugonjwa wa kiharusi au stroke.

Nina uncle wangu kwa week 3 sasa tokea aanguke na kupata hili tatizo, ameathirika upande mmoja wa mwili,mkono na mguu. Tafadhali anayejua anisadie.
 
Kwa Dar sijui ila pale Bugando kuna Weill Cornell Program mahususi kwa ajili ya wagonjwa wa Kiharusi and likely
 
Mwanzo nilipata vidonda ndani ya mdomo, vidonda hivyo vilimea kushoto mwa mdomo ndani, nilitumia limao kublash, baada ya siku 2 vilipunguza kasi na hatimaye vilipona. Kilichofuata ni mdomo, pua, na jicho kuelekea upande mmoja wa kushoto.

Jina kamili ya tatizo hili sijajua laitwaje, labda kiarusi au kupooza.

Muhimu naomba mnisaidie nitumie tiba gani ili nipone? hii ni wiki ya tatu sasa.

Ushauri Tafadhali.
 
Una umri gani kwani,na vp kuhusu mguu na mkono wa upande mmoja?
 
Sio stroke. Hiyo ni facial nerve palsy,, nadhani ni bell's palsy. Tafuta mtandaoni uelewe zaidi. Ila nenda hospitali
 
Back
Top Bottom