Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Habari zenu wadau, huduma ya kwanza kwa mtu mwenye Ugonjwa wa Kifafa ni nini? pia Ugonjwa wa Kifafa unaambukizwa kwa njia zipi?
 
Pole sana.


Ngoja wataalam wetu watakupa hasa
kile kinacholingana na hali ya mgonjwa.

cc MziziMkavu
Dr . Riwa
Na wana jf wote wenye msaada.
 
Ugonjwa wa kifafa hauambukizi.

Ni ugonjwa unaotokana na uwepo wa seli zinazotoa stimuli katika uncoordinated manner.

Uwepo wa seli hizo unaweza kupimwa kwa kipimo kinachoitwa EEG ambacho kinaonyesha electrical activities za seli za ubongo.

Kifafa kinaweza kusababishwa na matatizo aliyopata mtoto wakati wa kuzaliwa au kinaweza kutokea leter in life bila sababu kujulikana.

Huduma ya kwanza ni kuhakikisha njia ya kupumua inakuwa wazi mara mtu anapopata attack. Dawa za kulegeza misuli zinasaidia mtu aliyepata attack kutulia.

Ili kuepuka kupata attacks inabidi mgonjwa aende hospitali na kuandikiwa dawa, halafu atumie dawa hizo kama jinsi atakavyoelekezwa na mtaalam.
 
Kifafa

Kifafa ni nini?

Kifafa ni ugonjwa wa ubongo.

Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva.Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu

Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa mtu atashikwa na mshtuko wa kifafa?

Wakati mwingi, huduma ya kwanza ina maana ya kumfanya mtu awe salama wakati mshtuko wa kifafa unapotokea. Kwa bahati nzuri, mshtuko huwa mfupi na huisha baada ya dakika kadhaa.

Hatua ya kwanza katika kujitayarisha kwa ajili ya kifafa ni kufahamu kitu cha kufanya wakati ugonjwa huu unapotokea. Hii ni muhimu ikiwa unamchunga mgonjwa wa kifafa lakini pia kwa kila mtu. Ugonjwa wa kifafa unaweza kuanza katika umri wowote na kila mtu anahitaji kufahamu nini cha kufanya wakati mtu karibu nao anaathiriwa na kifafa.

Huduma ya Kwanza
  • Kuwa mtulivu na usiogope. Kifafa humuogopesha mtazamaji. Huchukua dakika chache na kwa kawaida huhitaji matibabu.Kumbuka ya kwamba mtu aliyeshikwa na kifafa huwa hafamu vitendo vyake na anaweza au asiweze kukusikia.
  • Walinde dhidi ya majeraha wakati wanaposhikwa na kifafa.Ikiwa inahitajika mweke chini kwa njia iliyo taratibu.
  • Sogeza vitu vigumu, vitu vyenye ncha kali na vilivyo moto na linda kichwa na mwili wa mgonjwa dhidi ya jeraha.
  • Usiweke chochote mdomoni ama ujaribu kubanua meno.
  • Mtu hayuko katika hatari ya kumeza ulimi wake
  • Usijaribu kuzuia mwendo wao kwa kutumia nguvu.Hili linaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia yule anayejaribu kuwasaidia.
  • Popote inapowezekana, jaribu kumlaza mtoto katika sehemu iliyo laini na wageuze upande mmoja.
  • Weka kitu tambarare na laini chini ya kichwa chake ili asijiumize.
  • Fungua nguo zilizombana haswa kwenye shingo kama tai, skafu na kadhalika
  • Usiweke chochote mdomoni.
  • Nakili mda ambao mshtuko umechukua.
  • Jaribu kutazama mwondoko ambao mtu hufanya wakati ameshikwa na kifafa.
  • Wakati mkutuo unaanza kupungua, hakikisha ya kwamba kupumua kumerudia hali yake ya kawaida.
  • Baada ya kifafa, mvingirishe mtu ili alalie upande mmoja.Hili hufanya mate kutoka mdomoni na kuhakikisha ya kwamba hanyongwi. Ikiwa kuna matapishi, mweke mtu kwa upande mmoja na safisha mdomo wake kwa kidole.
  • Usijaribu kumpatia dawa ama uoevu hadi aamke
  • Waondolee hofu, zungumza nao kwa upole na wasaidie kupata nafuu pole pole.
  • Usimwache mtu pekee yake hadi apate nafuu.

Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa nadhani nimeathiriwa na kifafa?

Ni muhimu kukumbuka ya kwamba kifafa ni hali ambayo inaweza kudhibitiwa. Sio kitu cha kuona haya. Sio laana ama ulemavu. Ni hali inayohitaji matibabu na kufuatiliwa kama hali zingine kama shinikizo la juu la damu, kisukari, pumu na kadhalika

Ikiwa unadhani ya kwamba umeathiriwa na ugonjwa wa kifafa ama ikiwa umewahi kuanguka chini na kuzimia ni muhimu kutafuta usaidizi wa dakitari aliye karibu. Ikiwa inawezekana andamana na mtu aliyekuwa nawe wakati ikifanyika ili waeleze kile walichokiona. Hili litasaidia dakitari kufanya ubainifu sahihi.
 
Habari Wadau,

Leo asubuhi nimejikuta katika wakati mgumu pengine kuliko siku yoyote ile,Nilikuwa nimekaa na mtoto wangu akawa ananiambia baba macho yanauma,mara kichwa kinaniuma nikamgusa akawa amechemka sana mwili,nikamwambia tulia nikupeleke hospitali

Tukaendelea kupiga stor na utani mwingi,ghafla akakamaa kama mti huku akitetemeka sana,nikamwita jina akawa haitiki tena, nikamkumbatia,Nilichanganyiwa sana,Ndipo nikamkimbiza hospital lakini ametibiwa.

Nimeona si vibaya kuwashirikisha magumu yangu ya leo
 
Pole sana!ni malaria makali hayo,mimi yalinitokea mwanangu alianza geuza macho ghafla wakat nacheza naye usku so naelewa what you went through
 
Pole sana!ni malaria makali hayo,mimi yalinitokea mwanangu alianza geuza macho ghafla wakat nacheza naye usku so naelewa what you went through

Asante Mkuu Lakini tumepima malaria hana kapewa dozi ya kunywa na Sindano ambazo ni anti-malaria.
 
Ni vizuri pia kuangalia kichwa chake huenda alipata tatizo la kuanguka akiwa mdogo na hizo ni athari zake. Apimwe vizuri
 
pole sana mpendwa kweli hiyo hali ni ngumu sana .degedege hutokana na homa kali ikipanda kuzidi 40 huwa ubongo unapata short. na hapo ndipo degedege hutokea.
Je alipoteza fahamu kwa muda wa dk ngapi?
mwanao ana umri gani?
je umepewa dawa gani?
je uko mkoa gani?
nipe majibu ya haya maswali ndipo nitakushauri la kufanya
 
pole sana mpendwa kweli hiyo hali ni ngumu sana .degedege hutokana na homa kali ikipanda kuzidi 40 huwa ubongo unapata short. na hapo ndipo degedege hutokea.
Je alipoteza fahamu kwa muda wa dk ngapi?
mwanao ana umri gani?
je umepewa dawa gani?
je uko mkoa gani?
nipe majibu ya haya maswali ndipo nitakushauri la kufanya

Ilimchukua kama dakika kumi kupata fahamu..! Ana miaka mitatu,niko Mbeya,Dawa nilizopewa ziko mbali kidogo nimetoka nyumbani,
 
Back
Top Bottom