Asante sana mkuu kwa elimu kubwa unayotoa! Naomba kujua, kuna maneno ambayo mara nyingi watu husema kukitokea mgonjwa wa namna hiyo! Je ni kweli kwamba mgonjwa akianguka wakati bado kazimia akikukojolea anakuwa amekuambukiza naww? Msaada tafadhaliMatatizo yaweza tokezea wakati wa matibabu? Je kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?
Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya mda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.
Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.
Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa?
Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa zingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali zingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.
Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.
Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii,dawa ya pili na saa zingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.
Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.
Ni kwa mda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa?
Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa, wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote.Katika watoto,hata hivyo mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye kifafa angehitajika kutumia.
madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi dakitari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa baada ya kumfuatilia mgonjwa kwa
kipindi fulani cha mda. Ni muhimu maamuzi haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai kunaweza kujirudia.
Kwa hivyo, jambo muhimu ni kuzungumza na dakitari wako kuhusu kusimamisha matibabu. Ikiwa mtoto hajafuzu kwa ajili ya kusitishwa matibabu kwa sasa, na kisha aendele kutokana na ushauri wa dakitari. Ikiwa mtoto atafuzu, basi hili linafaa kufanywa kwa utaratibu. Wakati kipimo cha dawa kinapunguzwa, ni muhimu kukumbuka ya kwamba mtoto anaweza kushikwa na kifafa. Waweke wakiwa salama na waangalie kwa karibu hadi dawa zote zimesitishwa kabisa na kila kitu kiko salama.
Mkuu Mgaya.com Hawezi kukuambukiza mtu mwenye ugonjwa wa kifafa kwa njia ya mkojo imani za kiswahili hizo Mkuu.Asante sana mkuu kwa elimu kubwa unayotoa! Naomba kujua, kuna maneno ambayo mara nyingi watu husema kukitokea mgonjwa wa namna hiyo! Je ni kweli kwamba mgonjwa akianguka wakati bado kazimia akikukojolea anakuwa amekuambukiza naww? Msaada tafadhali
Kama wewe unaamini uponyaji ndani ya Jina la Yesu mpeleke kwenye maombi. Maombi ni zaidi ya mitishamba! Kumbuka alipo Yesu yote yanawezekana!
Yesu anaponya sana lkn mitI shamba si uchawi..ni mimeo iliyooteshwa na Mungu..so kusali asali na dawa atumie
Mkuu Undu Kuhusu Vipimo vya kifafa nenda kamuone Daktari hospitalini atakupima na kujuwa kama una kifafa au huna.Nashukutu elimu nimeipata je vipimo vyake ni vipi ili kujua ni kwi ni kifafa au siyo kifafa