Ugonjwa wa Dr. Mwakyembe ni Huu! Jee Unasababishwa na nini?!

Naamino JF Doctors wanaweza kuja na hoja nzuro zaidi baada ya kuipitia taarifa ya Mwakyembe.

Ni wazi Mwakyembe atakuwa kwa imani yake anaamini amepewa sumu.
 
Pasco!

Nakwambia haya yote ya Dr H. M ni tamaa ya Kodi ya Watanganyika pale alipotaka kurejesha matumaini ya chama chao kwa Watanzania waliopoteza imani kbs kwa uongozi uliopo madarakani!

Pale tu alipotaka mafisadi wawe na huruma na kodi majasho ya Watanzani na ndiyo imempelekea mpk leo mauti inamnyemelea!

Tusipokuwa makini na hawa mafisadi hakika wanatamani watuzike tukiwa hai kweupe!

Na sijui wao watakaa na nani ktk Nchi hii ya maziwa na asali.
Chanzo kubwa ni hiyo tu na nafikiri wewe Pasco ndio uko nyuma jamvini maana Kamanda wetu mpiganaji wetu Jason bourne alishaanika kila kitu hapa A to Z!

Tamaa mbele MAUTI nyuma!
 
Hivi ile ripoti ya JB ipo wapi? Mwenye nayo itumpie hapa!
Ukisoma maelezo ya Dr Mwakyembe yanaonyesha anaamini kwa 100% kuwa ugonjwa wake umetokana na suma ya hujuma, sasa wakati wakutumia hisia hizi na ushahidi wa India ndio huu, wizara ya afya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wameuhuisha mjadala na kubadili sura sasa ukweli kukaribia!

Sasa tunaomba majibu (ORIGINAL Copy) waliyonayo wizara toka india ambayo jeshi limetumia kukanishia!

Ifahamike kuwa kwamujibu wa Mwakyembe Madaktari wa Apolo hawajatoa majibu ya ugonjwa, sasa jeshi limepata wapi hayo majibu??
 
Pasco,
Sikuwa na nia ya kuchangia hii thread lakini umenilazimisha kufanya hivyo.

Ndugu yangu punguza siasa kwenye taaluma za watu. Taarifa ya mwakyembe wote tumeisoma, hakuna mahali ametaja ugonjwa anaoumwa, zaidi ya kusema mzizi wa tatizo lake uko kwenye bone marrow, sasa wewe mwanasiasa- mwanahabari umezipata wapi hizo facts?

Unajaribu kuwaongoza madaktari kwenye fani yao ili iweje? Una upande katika huu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe?

Ilitosha tu kuweka taarifa ya Dr. Mwakyembe na kuwaacha madaktari wenyewe waogelee. Lakini kwakuwa umei-jeopardise mwenyewe hoja yako uwe mvumilivu na sisi wanasiasa wenzako tunaopotoa maoni yetu dhidi ya hoja zako, wakati huo nikiwaomba madaktari wajielekeze kwenye taarifa ya Mwakyembe wanapojibu.

Ni vizuri ukaacha siasa ktk jukwaa la JF Doctors ili sote tunufaike kuliko kujaribu kuwapotosha madaktari, sijui kwa faida ya nani!?

Jirani umesema kitu muhimu sana, ndugu yetu japo lengo lake lilikuwa zuri lakini miitikio chanya ya siasa za kijani ilimtoa kwenye lengo!
 
pasco.., kwa sababu umeskia tatizo lipo kwny bone marrow na sio ini kwhy unaamini sio sumu!

mm sio daktari, ila kwa proffession yangu naelewa kuna kitu kinaitwa radiation poisoning..., mtu akiwa exposed to lethal dose za hizi radiations (acute radiation poisoning) lazma apate madhara makubwa sana kama si kifo...,

baadhi ya hizi radiations hu-disturb normal functions za central nervous system, na kwa elimu ndogo ya biology, tunajua tunazungumzia nn hapa..., unakumbuka picha za mwisho za yasser arafat kabla hajapelekwa france? Au kuna rais mmoja pale baltic states alikua anti-putin, walimuharibu sura vibaya sana,

tuache kuleta siasa kwa maslahi yako binafsi..., tunaongelea maisha ya kiongozi, baba wa familia, kaka, mjomba, ba mkubwa, ba mdogo, mentor, wa watu wengi ambaye selfish bastards wanataka kumpoteza...,

Staki maswali kuhusu yasser arafat
 
Tatizo Pasco unajulikana wazi kuwa wewe ni mpambe wa Lowassa na hilo hujawahificha liko wazi kabisa. Unapokuja na thread kama hizi za kuwalazimisha wamadaktari wa JF watoe wajibu ya ugonjwa wa Mwakyembe, sisi wengine tunakuona unatapatapa na juhudi zako za kusafisha jina la bosi wako. Post zako zinaonyesha wazi aina ya waandishi wa habari tulionao Tanzania. Watu wa habari kama mhimimili wa nne wa dola wenye jukumu kubwa la kuwapasha habari wananchi mlipaswa zaidi kuwa neutral kwenye mambo kama haya. Ikifikia mwandishi msomi kabisa kama wewe tayari unaonyesha hisia mapema kabisa za kushabikia wanasiasa ni hatari!. Sijui wale mnaita makanjanja ndio watakuwa na hali gani. Hivi tuwaeleweje?. Simple answer itakuwa either umeshakula chako mapema, either jamaa ni ndugu yako, au mnauhusiana wa kimapenzi maana wengine hatujui wewe ni mwanaume au mwanamke.
 
Mkuu Jackbauer, thanks for a good try, zile ulizoweka ni zile za matokeo ya chemotherapy ndio maana wengi hushauriwa kunyoa nywele zote kabla hazijanyonyoka. Hii ya doctor ni skin disorder due to something kwenye bone marrow. Naendelea kuwasubiria madaktari wetu, walijiunga wengi wakati ule wa mgomo natumaini bado wapo!.

umeshaambiwa kuna exposure to radioactive source. Hata hiyo radiation huwa inakuwa absorbed ndo inaleta systemic effects. Hata hao wanaoambiwa wanyoe nywele siyo direct effect ya mionzi ndo zinanyonyoa nywele,ni systemic effects on hair forming proteins. Areas of concentration zinatofautiana kulingana na hiyo element. na exposure ya radiactive material siyo radiotherapy 2,Aafu we jamaa mbona post zako unapenda kulazimishia upande unaoutaka wewe? Unakumbuka kipindi cha mgomo na hoja zako za kutishia doctors,kuna aliyefukuzwa? Nani amekutuma umsafishe kwenye hili saga la mwakyembe?
 
Moja ya Tabia ya Polonium-210 ni kushambulia Bone Marrow. Hii sumu ilitumika kumuua Alexander Litvinenko, Former KGB Officer.


Cheki hiyo video...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ng'wanza Madaso, maelezo kamili ni marefu na politics nyingi mule, hii ni thread ya kuujadili ugonjwa huo tuu na sio siasa za issue hii!

pasco kuna tofauti kati ya symtoms and sign na diagnosis. Ndo maana mtu akiwa na homa huwa huambiwi kuwa anaumwa homa,au huwa hatibiwi homa. Inatafutwa source ya homa ndo diagnosis. Yanayojitokeza kwa mwakyembe ni symptoms an signs tu, ndo maana inatafutwa source.!! Kwenye ugonjwa lazima uandikiwe NI UGONJWA WA NGOZI UNAOSABABISHWA NA,......... Kuna allergic dermatitis, bakterial dermatitis, kapos sarcoma. Nk. Sasa mwakyembe tunaambiwa ni ugonjwa wa ngozi tu. Yaani just dermatitis, basi watuambie hata idiopathic.
 
Ukisoma taarifa yake Mwakyembe utagundua ujumbe wa wazi kuwa source ya ugonjwa wake ni upinzani wake dhidi ya politics za maslahi binafsi!
 
Pasco is a snitch, I hope MUBYAZI hajamuweka karibu naye sana kujua iDS za members wa JF otherwise majina yenu yote yatakuwa UWT na kwa Lowassa!!
 
Kinachonistua kwenye hizi threads ni maoni yatokanayo na mioyo ya ganzi ambao wanahaingaika na mgonjwa binafsi, mapambano yake na jitihada zake za taarifa anazotoa.

Mimi binafsi nikifuatilia matukio naona mambo makubwa mawili

1. Foul Play aliyofanyiwa mgonjwa

2. Damage Control wanayoifanya wanaojua hiyo foul play imefanyikaje.

It has come to our knowledge hata huyu mama aliyetumika kutekeleza unyama kesha kufa (actually kesha uawawa). Pawepo na daktari au pasiwepo mtiriko wa matukio haya yanadhihirisha kuna tatizo kwenye jamii yetu na hasa linawakumba utawala wetu.

Baadhi yetu hatuna uwezo wala nyenzo za kukabiliana na hali hii, lakini ni ubinadamu kuwa kila chenye mwanzo kina mwisho; na siku zote kwa kibinadamu uovu hushindwa.

HATA TUKIJITAHIDI KUKUSANYA MAELEZO YA KISAYANSI BADO TATIZO TULILONALO KIJAMII LA UTAWALA MASLAHI LINATUKABILI. Tumegawanyika makundi mawili wale wanaomhurumia na kumuunga mkono mgojwa kwa sababu amepatwa na haya kwenye mapambano; na wale ambao wanajua na washiriki wa kutekeleza unyama huu. Tusubiri tu kwani kila siku tunaelekea kuyajua tusiyoyajua ILA UKWELI NA UONGO MWISHOWE UTAJITENGA, na utatufumbua wote pamoja na misimamo yetu.
 
Wanabodi,
Kufuatia malumbano yanayoendelea kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakiyembe. Hatimaye leo Dr. Mwakyembe mwenyewe ameka wazi ugonjwa unaomsumbua ni

Uchunguzi wa Apollo haujakamilika kujua chanzo, two facts are definite
1. Anaumwa Ugonjwa wa Ngozi!.
2. Source ni something kwenye bone marrow!.

Kwa vike humu jukwaani tunao madaktari kibao wanaoweza kutusaidia ugonjwa huu ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini na labda matibabu yeke ni nini?.

Angalizo, hili ni jukwaa la JF Doctor, nawaombeni sana this now is medical professional issue sio politics, hivyo kama na wewe ni mwenzangu na mimi, hujui lolote kuhusu ugonjwa huu, nakusihi sana jipitie tuu na kujinyamazia, na usichangie chochote ambacho hakihusiani na ugonjwa huu!.

Asante!

Pasco.
Mode, maadam mwenyewe ameshafanya ibada ya shukrani, hii inamaanisha kamuachia Mungu, but for records, je sisi jf nasi tuishie hapa?, au tuendelee kuhoji?.
 
Pasco is a snitch, I hope MUBYAZI hajamuweka karibu naye sana kujua iDS za members wa JF otherwise majina yenu yote yatakuwa UWT na kwa Lowassa!!

Someone said it here sometime ago that Pasco is a SNITCH!!!! Yumo humu kwa kazi maalum na kuwepo kwake karibu na INVISIBLE is not good to JF's health!!

Kuna kitu nilikuwa nafuatilia kuhusu siri ya mgonjwa na Daktari wake na familia yake, ndipo nikakutana na hii hoja. Kumbe tumewahi kuitana ma snitches humu, hivyo kumtafuta Mubyazi kumuweka karibu ili kupata IDS za members wa jf kuzipeleka TISS!. Kiukweli tumetoka mbali!.

Wakuu Bulesi, Ndinani, vipi mpaka sasa bado unaamini hii snitching humu jf?.
P.
 
Mubyazi is smart, JF is encrypted so snitches or no snitches we are covered!!! Moreover MUBYAZI is a solid professional!!
So it's the smartness of Mubyazi and the encryption.
Kumdhania mtu yoyote kuwa ni snitch it's a human beings lakini kumsingizia mzalendo wa kweli na kumtaja jina kuwa ni snitch, akitokea in reality kuwa sio snitch, whoever aliyemsingizia ana kuwa some little bit of karma to pay. Before you say anything, better be sure than sorry.

Hongera kwa smartness ya Mubyazi na ku encrypt JF.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom