Ugonjwa wa ajabu

Thomas Juma

Member
Nov 9, 2010
88
17
Nisaidieni maana hadi najiogopa!
Ninakama siku tano sasa nimefikwa na ugonjwa wa aibu tena hata siufaham, katika njia ya haja kubwa kuna kama nyama imetokeza nje ikionyesha kama vile ni ya ndani na hairudi, hadi sasa kukaa na umia kutembea ndio kabisa na inapofika wakati wa kwenda haja kubwa mmh ni tabu tupu manake hadi haja ndogo wakati wa mwishoni inanasababishia maumivu huko. Waungwana niambieni hili ni gonjwa gani?, linasababishwa na nini? ni tumie au nifanyeje nirudie hali yangu ya kawaida?

Sina raha wala amani!
 
pole mkuu huo ni ugonjwa wa kawaida kabisa na unatibika si wa ajbu kama unavyofikiria nadhani kuna posti zinazoongelea huu ugonjwa nenda kule jf doctor watakusaidia
 
Kuna Riwa yumo humu ndani ya jamvi nami ndio amenisaidia kesi kama yako. Tena umenikumbuksha ngoja nitoe shukrani kwake mie nimeshapona.
 
Laura Mkaju, mwambie mwenzio afanye nini usimnyorishe bana, saidia dugu.:biggrin1:
 
nenda hosp ndugu. huu ugonjwa kiswahili wanaita bawaziri ama kidhungu ni haemorrhoids. google utapata nondo. kwa kifupi huenda ukahitaji upasuaji mdogo.usione aibu kutafuta matibabu,dr atakushauri pia kama unetokana na kazi unazofanya (manual work ama driving on bumpy roads for a long time). nafanya utafiti juu ya hii.pole,all the best
 
pole sn.
Huo sio ugonjwa wa ajabu, wala aibu, upo ni wa kawaida na unatbika. Wahi hosptalini.
 
Pole Thomas...kunathread tulidiscuss huu ugonjwa (Haemorrhoids) kwa kina, grade zake na matibabu yake kufuatana na hizo grade. Bahati mbaya mimi sio mtundu wa 'mtandao' kuweza kuitafuta na kupost link hapa..nadhania ingekusaidia sana.

Mafurahi sana Laura kwa kupona. Tafadhali mwenye ujuzi wa kupost link, au moderators msaidieni huyu mwenzetu hiyo link.
 
pole man, fata link aliyokupa Riwa kule tulielezea vizuri sana .....

get well soon
 
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/133229-tatizo-la-hameroids-vinyama-sehemu-ya-haja-kubwa.html

Thomas, hii ni ile link tulikuwa tunadiscuss kuhusu Haemorrhoids na matibabu yake, iperuzi..kama utakuwa na maswali ya ziada basi tutaendelea toka hapo.

Ubarikiwe sana Riwa kwa msaada wako mkubwa unaotoa katika jukwaa hili. Na wengi sasa wameshakufahamu kama Riwa ni Dr wa ukweli...hongera sana Mkuu kwa moyo wako wa kusaidia kwa kutumia utaalamu uliokuwa nao katika nyanja hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom