Ugomvi wa majirani wahamia kwa kuku!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Majirani wawili walikuwa na ugomvi wa muda ulioshindikana kupatiwa suluhu na majirani wengine. Sasa siku moja jirani A akaona jogoo la adui yake-jirani B likimfukuza kuku wake jike. Ghafla jirani A akapandwa na asira eti kisa, kaona jogoo la mgomvi wake jirani B. Sasa kituko ni jinsi alivyoporomosha mitusi na kumtimulia mbali yule jogoo, tena kwa mawe, ambaye tayari alikuwa juu ya kuku jike wa jirani B akijiandaa kuendeleza kizazi chake.

Maneno ya jirani A wakati akimkaripia: Shenzi taipu, ushenzi weko peleka huko huko kwa anayekufuga sio kuniletea kwa kuku wangu. Kawapande hao hao majike wa anayekufuga, mshenzi weeee!

Watu tukabaki midomo wazi, bhaaaaaaaaa, iweje mtu mzima amporomoshee matusi mazito kuku tu ambaye hata alikuwa hajui kinachoendelea juu ya ugomvi wa wamiliki wao wanaowafuga?

Duniani kuna mambo, na ukishangaa ya Musa utayaona ya Farao!

Jumapili njema!
 
Halafu akamrudia kuku jike...
Ole wako nikuone tena una mahusiano na yule jogoo tena,ntakuchinja kabla ya christmas
 
huyo jirani hamnazo kweli, yaani anawakata stimu kuku kisa ugomvi wake na jirani, mpuuzi.
 
Mhh, nimeambiwa hata Christmas hakuiona maana alikuwa kanona sana.

PASAKA ilipofika, wakashindwa kuvumilia.......
Halafu akamrudia kuku jike...
Ole wako nikuone tena una mahusiano na yule jogoo tena,ntakuchinja kabla ya christmas
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom