Uganda - Tanzania war on tbc1

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Ndugu

Kama uko na TV yako sasa hivi Fungulia TBC1 wanaonyesha kipindi maalumu kuhusu Vita ya Kagera , uzuri ni kwamba picha nyingi zina rangi kidogo , nashangaa sana wakati huo watu walikuwa na ari sana ya kujiunga na jeshi kwa ajili ya kutetea maslahi yao , picha hizo zinaonyesha watu kwa makundi walikuwa wanapelekwa kwa mabasi kuandikishwa jeshini kwa ajili ya kwenda katika Shuguli hiyo

Wewe Angalia TBC1 ujionee mwenyewe , hata katika magazeti ya Mtanzania wameanza kuchapisha baadhi ya makala ya matukio muhimu kwenye Vita hiyo

Pia unaweza kusoma makala hii The Steps to Interstate War in Africa ina mengi ya kueleza kidogo angalia attachment
 
SHY, kama inawezekana ukarekodi kisha ukaidumbukiza you tube itakuwa poa sana wengine hatuna TV.....hiyo makala nimeshaisoma juzi hapa thanks
 
Hata leo vijana wana ari ya kujiunga na jeshi kama sehemu ya kulitumikia Taifa lao,wewe unasemaje?
 
Niko hapa naangalia kwa makini sana.dah! jeshi letu lilikuwa imara sana.
 
Ndugu

Kama uko na TV yako sasa hivi Fungulia TBC1 wanaonyesha kipindi maalumu kuhusu Vita ya Kagera , uzuri ni kwamba picha nyingi zina rangi kidogo , nashangaa sana wakati huo watu walikuwa na ari sana ya kujiunga na jeshi kwa ajili ya kutetea maslahi yao , picha hizo zinaonyesha watu kwa makundi walikuwa wanapelekwa kwa mabasi kuandikishwa jeshini kwa ajili ya kwenda katika Shuguli hiyo

Wewe Angalia TBC1 ujionee mwenyewe , hata katika magazeti ya Mtanzania wameanza kuchapisha baadhi ya makala ya matukio muhimu kwenye Vita hiyo

Pia unaweza kusoma makala hii The Steps to Interstate War in Africa ina mengi ya kueleza kidogo angalia attachment
Watu wa wakati huo walikuwa na ari ya kujiunga na jeshi kwa vile walikuwa na uzalendo wa hali ya juu. Walikuwa tayari kuifia Nchi-mama Tanzania, na si kutetea maslahi yao kama ulivyoiweka.
 
Unajua wengi wetu tumezaliwa tume kuta nchi yetu ina uhuru tayari ndio maana hatuna ari kama ya watu wa enzi hizo.watu 10 walitoka kwenye kaya moja na kwenda kujiunga na jeshi.Kitu ambacho kwa sasa sizani kama kuna mtu/watu wanao wenza kufanya hivyo.Wakati huuu mtu kujiunga na jeshi hataki.
 
Inasemwa kwenye ile vita ya uganda waganda walivunja daraja la mtukula. lakini pia wengine wanasema watanzania ndio walivunja kwani walikuwa wamezdiwa na walivunja kuzuia majeshi ya amini kuzidi kuingia tanzania .

Inasemekana kuwa watanzania walivunja ili kwanza kukabiliana w na wanajeshi waliokuwa kagera. Taarifa hizi na nyingine kama vita ile iligharimu tanzania shilingi ngapi? wanajeshi wa ngapi walipoteza maisha na ni muhimu. wenye data watupe.

Kuna wazee wanasema vijana ambao hawajapita JKT ile yenewe kuna kitu muhimu wanakosa. Wengine wako tayarai hata kulipia ili vijana wao wapite JKT. Nadhani ni muhimu kwa JKT irudhishwe na iwe lazima. iwe ni funzo la UKAKAMAVU, UVUMILIVU na UJASIRI na UJASIRI.
 
Nimeona hapo mateka wa Uganda anatishiwa kwa kisu shingoni, Je huu hauwezi kuwa ushahidi kwamba tulikuwa wanyama na kukiuka mikataba inayolinda haki za POW!
 
Wengine mpaka leo hatujalipwa ,nilienda kule makao nilikoandikisha wakaniambia nani alikuita kuja kujiandikisha ,si umekuja mwenyewe ? Nikawashangaa kidogo ,halafu nikawambia tuliitikia wito wa Baba wa Taifa ,wakazidi kunikandia na kuniambia basi nenda huko ukadai .
 
Ndugu

Kama uko na TV yako sasa hivi Fungulia TBC1 wanaonyesha kipindi maalumu kuhusu Vita ya Kagera , uzuri ni kwamba picha nyingi zina rangi kidogo , nashangaa sana wakati huo watu walikuwa na ari sana ya kujiunga na jeshi kwa ajili ya kutetea maslahi yao , picha hizo zinaonyesha watu kwa makundi walikuwa wanapelekwa kwa mabasi kuandikishwa jeshini kwa ajili ya kwenda katika Shuguli hiyo

Wewe Angalia TBC1 ujionee mwenyewe , hata katika magazeti ya Mtanzania wameanza kuchapisha baadhi ya makala ya matukio muhimu kwenye Vita hiyo

Pia unaweza kusoma makala hii The Steps to Interstate War in Africa ina mengi ya kueleza kidogo angalia attachment

Hakika nimeona uzalendo wa kutisha kwenye filamu hii!! Je, uzalendo ule leo hii kweli upo? Miongoni mwa wazalendo walionishangaza zaidi ni raia mmoja aliyeenda kujiandikisha kwenda vitani huku akiwa amevaa shuka; mwingine suruali kaifunga kwa kamba(ndio mkanda); na mwingine yupo pekupeku kabisa!! Nazani waliokuwa pekupeku ni wengi zaidi!!! Leo hii litokee jambo kama lile ni wangapi watakuwa tayari kwenda kujitolea? Jambo moja limeniuma sana==jamaa mmoja (koplo ....) ambae kapigana vita aliyepo Old Shinyanga sasa ni fundi viatu!!! Inauma sana, waliopigania nchi wanashona viatu waliokuwa wamestarehe wanawanyonya wapigania nchi!!! Kuna lingine vilevile linaashiria uzalendo na umoja!!! Wananchi waliobaki uraiani walikuwa wanapewa mafunzo ya kujilinda/kujificha!!! Leo hii tulivyo kila m2 na lwake ni nani atakubali mafunzo yale?! Bila shaka ikitokea tena wengi wao watajazana kwenye balozi kutafuta viza na akina siye Ubungo kukimbilia sehemu salama!! M2 asiye mzalendo ni mbinafsi, hivyo atakachofikiria ni kukimbia badala ya mafunzo ya kujilinda!!! Inaniuma sana!! Kumbe kuna wengine walikuwa wanachangia ng'ombe na nafaka kwa ajili ya wapiganaji!!!! Wale ambao walikuwa matured enough wakati huo hebu tupeni stori zaidi!!!
 
Hivi wakulu hakuna kitu kama documentary ya hii vita jamani? manake sio siri vizazi vya siku hizi wanatakiwa kujua tumetoka wapi....
 
Ooops! Mods, kama kuna thread imeanzishwa tayari basi unaweza kuziunganisha!
---------------------------------------

Leo; karibu kwa siku nzima TBC1 imekuwa na vipindi maalumu juu ya miaka 30 baada ya Vita vya Kagera.

Hakika kuna mengi sana ambayo binafsi nimeyasikia kutoka kwa askari wetu mbalimbali wa JWTZ na waliostaafu na hata baadhi ya viongozi wetu kupitia kipindi hiki. Niliingiwa na hisia kali za uzalendo na hamasa kwa jinsi askari wetu walkivyotetea nchi yetu bila woga.

Natamani hata vita vya ufisadi vingepiganwa kama vita vya Kagera.

Katika kipindi hicho, nikiwa mwanafunzi wa darasa la saba sitosahau maneo ya Mwalimu alipotangaza vita wakati ule . . . .

Uwezo wa kumpiga tunao . . .

Sababu za kumpiga tunayo . . .

Na nia ya kumpiga tunayo . . . .

Je, wewe wakati huo ulikuwa wapi na unakumbuka nini? Au ni nini kilichokugusa zaidi katika kumbukumbu hizi?
 
Hivi wakulu hakuna kitu kama documentary ya hii vita jamani? manake sio siri vizazi vya siku hizi wanatakiwa kujua tumetoka wapi....
Kweli kabisa, inaweza kupunguza haya matatizo ya wizi mkubwa mkubwa na ufisadi
 
..wananchi waliombwa kujiandikisha kwenda mstari wa mbele.

..mkoa wa Mara ulielemewa kwa jinsi wananchi walivyoitikia wito wa kwenda kumngoa nduli Iddi Amini.

..matokeo yake serikali ikaruhusu mkoa wa Mara uandikishe wananchi wengi kuliko lengo walilokuwa wamepewa mwanzo.

..Msumbiji ilikuwa ni nchi pekee iliyotusaidia kwa kuleta askari wake kupigana bega kwa bega na ndugu zao Watanzania ndani ya Uganda.

..kuna vitabu viwili vya Kiswahili na kimoja cha kiingereza vinavyoelezea vita hii.

..nadhani wakati umefika JWTZ watengeneze documentary ya vita hii. makamanda na askari waliopigana vita ile wamezeeka na wengine wameanza kututoka.

..pia napendekeza JWTZ wajenge makumbusho ya vita vya Kagera.
 
Mataifa mengine ambayo yalikuwa katika umoja wa nchi huru za kiafrika yalikataa kwa sababu tanzania ilifadhili kumweka madarakani kiongozi aliyekuwa anafuata ujamaa huko sheli sheli
 
..wananchi waliombwa kujiandikisha kwenda mstari wa mbele.

..mkoa wa Mara ulielemewa kwa jinsi wananchi walivyoitikia wito wa kwenda kumngoa nduli Iddi Amini.

..matokeo yake serikali ikaruhusu mkoa wa Mara uandikishe wananchi wengi kuliko lengo walilokuwa wamepewa mwanzo.

..Msumbiji ilikuwa ni nchi pekee iliyotusaidia kwa kuleta askari wake kupigana bega kwa bega na ndugu zao Watanzania ndani ya Uganda.

..kuna vitabu viwili vya Kiswahili na kimoja cha kiingereza vinavyoelezea vita hii.

..nadhani wakati umefika JWTZ watengeneze documentary ya vita hii. makamanda na askari waliopigana vita ile wamezeeka na wengine wameanza kututoka.

..pia napendekeza JWTZ wajenge makumbusho ya vita vya Kagera.

Actually mkuu kuna kitabu nilikisoma nikiwa mdogo nadhani miaka ya 80 huko, kilikuwa kinaitwa 'Kuanguka kwa fashisti Iddi Amini', na nakumbuka publishers walikuwa TPH, sasa sijui ni kimojawapo ya hivyo viwili? na je naweza kukipata wapi?

Leo nilikuwa naangalia documentary kibao tu za 'raid on entebbe' zimejaa you tube na kwingineko, watu wa Israeli pia wametengezea za kwao, na ni tukio la dakika 90 tu! sasa sisi kwa nini tunashindwa jamani?
 
Kaizer,

..binafsi sikumbuki majina ya vitabu vya kiswahili vinavyohusu vita vya Kagera. lakini nakumbuka kimoja kilikuwa na rangi nyekundu.

..kile cha Kiingereza kinaitwa 'The War in Uganda' ni kizuri lakini kasoro moja ni kwamba mwandishi alikuwa attached na Kikosi kimoja cha JWTZ kwa hiyo ameandika zaidi kuhusu kikosi hicho na kamanda wake.

..sasa hivi navitafuta vitabu vyote vya vita ya Kagera. actually kitabu chochote kile chenye historia ya Tanzania.
 
jokaKuu,
Umetaja kujitolea kwa watu wa Mara ukanikumbusha kisa kimoja alichonisimulia Wassira.
Wakati huo alikuwa Regional Commissioner na kule Tarime mzee moja mwenye umri wa miaka zaidi ya 65 alisafiri kwenda ofisini mwake kujitolea kuandikishwa vitani. Huyo mzee aliwahi kupigana katika jeshi la KAR. Wassira alipomwangalia na kuzingatia kuwa amesafiri kutoka Tarime hadi ofisini kwake akamwambia kuwa si lazima aende kupigana Uganda lakini yeye atakuwa kinara cha internal defense huko huko Tarime. Mzee akaridhika akarudi na mgobole wake Tarime kuwa vanguard wa internal defence. Ni lazima tutafute njia ya kufufua tena moyo wa uzalendo Tanzania.
 
Jasusi,

..sasa utanifanya nikafukue kitabu changu cha "The War in Uganda."

..i believe i read in the book that someone older than 65 showed up to be enlisted.

NB:

..katika watu niliotegemea wana vitabu hivi ni wewe.
 
Nilikuwa nacho kile cha Tony Arvigan na Martha Honey lakini jamaa alikuja kuazima na hajakirudisha hadi leo. Nimekitafuta Amazon nikakuta bei imepanda ile mbaya. Lakini nitakinunua tu.
 
Back
Top Bottom