Ugaidi wa serikali ya Marekani.

Na jana waziri wa marekani amesema Iran itapigwa na Israel kabla ya mwezi wa nne
 
kitu chochote chenye neno "serikali" maana yake ni ugaidi, nashangaa unavyo i single out Marekani.
 
Pia mmeangalia ,upande wa pili wa jamaa wanaopiga bao kwa kujibu kila tukio km inspector enzi zake?Wazungu wanapiga bao sana(wanatengeneza hela sana) kwa kutumia nature ya binadamu hasa wanaotoka nchi za middle east/africa na nyingine zenye misingi ya kijamma ambao huamini ktk conspiracy theories.Watu wanoshawishika kirahisi huwa wanaingia haraka km wale wa upatu...
 
Mimi naona kwa umaskini wa akili na ufukara wa mawazo wa viongozi wetu tutapigwa na kuoana wanaume kwa wanaume, mwanamke kwa mwanamke, watoto wataleta hawara zao ndani na haturuhusiwi kuwauzi watoto, watalalana ndani ya nyumba ya mzazi na anatakiwa kuwapa chakula watakapokuwa wamamemaliza kazi zao na kila jambo la kifirauni litafanyika Afrika maana atakayekataa atahukumiwa kufungwa maisha na sio kunyongwa lengo likiwa kuwa kuwaonya wanaozaliwa ili wajue na ili wafuate mila zao " EWE MUUMBA TUEPUSHE NA BALAA HILI NA TUNAOMBA ANGAMIZA WOTE WANAOKUWA NA NIA MBAYA NA WANYONGE"
 
Historia ya dunia imegubikwa na majanga ya kupanga.Hawa watu wanafanya ibada kwa mungu wao,wanatoa kafara ya damu za watu in exchange of power.Al-qaeda,Boko haram,Al Shaabab,Tamil tiger,na uasi wa aina zote duniani unadhaminiwa na UN,yes UN chini ya mataifa yote yenye nguvu unayoyajua duniani.Dunia haitakua na amani kamwe!
 
kitu chochote chenye neno "serikali" maana yake ni ugaidi, nashangaa unavyo i single out Marekani.

Hii tafsiri umeitoa wapi?Tafadhali Kiranga ukirudi hapa naomba ufafanuzi!
 
Last edited by a moderator:
Hii tafsiri umeitoa wapi?Tafadhali Kiranga ukirudi hapa naomba ufafanuzi!

Katika joho la "usalama wa taifa" kila serikali inaficha ugaidi dhidi ya watu wake.

Katika kushindana na serikali nyingine kila serikali inafanya ugaidi na ujasusi dhidi ya nchi nyingine.

Haya yamekubalika mpaka kutaka kuhalalishwa na wanafalsafa kama wakina Igor Primoratz.
 
Thanx Kiranga nimekuelewa.Ni kama vile tulivyo Watanzania,kila uchao tunapiga kelele eti wale mafisadi,wakati kila mmoja wetu ni tayari ni fisadi kwenye familia yake na anataka naye apate nafasi ya kuwa fisadi zaidi.Wanadamu ni wanafiki sana!
 
Last edited by a moderator:
Ngoma unapiga mwenyewe unaimba mwenyewe,unacheza wewe na unapiga vigeregere mwenyewe na unajipongeza mwenyewe hiki unachofanya umeonyesha wazi CHUKI uliyonayo dhidi ya wamarekani sasa unajaribu kupandikiza chuki hiyo kwa wengine kitu ambacho hutendi haki wewe ungeleta hapa hoja yako ya kuichukia Marekani na wana jamvi wangechangia kwa uhuru kabisa sasa wewe umebeba jukumu la kuihukuma Marekani peke yako angalia umeposti na kuchangia Topic 20 bila kuwapa nafasi hata wengine wachangie.umetoa mada wewe mwenyewe na umechangia wewe mwenyewe mara 20 wewe umeonyesha wazi una chuki binafsi na wamarekani mada zako zote bila kuishambulia Marekani huoni kama umechangia wewe ni shujaa wa kueneza CHUKI hongera sana
 
Echolima.
Huu ndio mchango wako?

Kwa nini umefikia hitimisho kuwa naichukia Marekani?

Nilichofanya mimi ni kudondoa kutoka vyanzo tofauti, video au mada zinanazokushawishi kuwa Marekani wanafanya ugaidi na kusingizia wengine kwa lengo la kutanua himaya yao.

Kama una vyanzo vya taarifa au video, weka hapa na onesha kuwa US hawafanyi ugaidi au hawatanui himaya yao kwa kutumia ugaidi.

Unaelewa maana ya chuki?

Watu wengine hawawezi kuhimili kusikia ukweli.

Hata kwa tafsiri yako kuwa mimi nimeleta mada au mjadala, hakuna ambaye amezuiliwa kuandika maoni yake vile apendavyo. Badala ya kutaka malumbano ya chuki/mapenzi nami ungeweka machango wako kama kuisafisha US au vyenginevyo.Chagua moja kati ya hizo 20 ulizoziona na toa maoni yako.

Kwa mfano, tetea uwepo wa AFRICOM katika nchi za Afrika(Bara la Afrika) au onesha madhahara ya uwepo wake kwa Afrika.
Karibu mkuu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom