Ugaidi utatumaliza?

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,121
10,829
Vita dhidi ya ugaidi ilianzishwa na rais George .W.Bush mwaka 2001.Katika uzinduzi wake wakati akijitayarisha kulipiga taifa la kiislamu la Afghanistan aliteleza na kusema kuwa ni Crusade.
Neno hili haraka waislamu walilikumbuka na kulirudisha mwaka 1095 A.D wakati watawala wa kikristo wa Ulaya walipojikushanya chini ya uongozi wa Pope Urban kuuangusha utawala wa kiislamu uliokuwa na makao makuu yake ndani ya Ulaya.Utawala wa Bush ukajaribu kulipoza na kutoa tafsiri nyingi tata.
Miaka takriban 10 sasa tafsiri ya vita dhidi ya ugaidi imekuwa dhahiri kwa walimwengu walio wengi, kwamba ni vita dhidi ya uislamu. Marekani yenye teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi na nguvu ya kiuchumi imeuwa maelfu ya watu hasa Iraq,Afghanistan na Pakistan na kuzitia mkononi nchi nyingi hasa zenye waislamu wengi kwa kisingizio hiki hiki cha vita dhidi ya ugaidi.
Marekani inapoangusha bomu kwenye harusi,matanga au sokoni hujitoa kimaso maso kwamba ilikuwa ikimlenga gaidi fulani.Mara nyengine husema imempata waliyemkusudia lakini hata wakimkosa hawajali hudanganya kuwa wataunda tume kuchunguza.Kabla hizi tume hazijatoa jawabu tayari huwa wameshaangusha mabomu mengine mengi.Hawajali kutoa jawabu wala kuulizwa jawabu. Hakuna wa kuwazuia wala wanayemuogopa.Ndio maana jawabu imekuwa nyepesi kuwa hii vita ni kuua waislamu tu, na kuwahofisha mpaka wasiweze kutoa sauti.
Kiburi cha Marekani kuua waislamu kimepanda sana. Wametangaza kuwa tofauti na zamani ambapo ili ndege (drone) iitwe kuua ilikuwa lazima kipatikane kigezo cha mtu fulani aliyekuwa akiwindwa kuwa alikuwa eneo hilo.Sasa askari kanzu akimdhania mtu vibaya tu itatosha kuagiza bomu lije limuue na wenzake hapo alipo.
http://www.cnn.com/2010/TECH/05/07/wired.terrorist.drone.strikes/index.html
Kwa mtazamo wa kiimani wapo baadhi ya wakristo na wayahudi walio wengi ambao hufurahi pindi waislamu wa maeneo tofauti duniani wanapouliwa au kuteswa kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi.Tuondokane na imani zetu tuje na ubinadamu wetu tu.Jee ni sawa kujifanya kijogoo kiasi hiki kwa binadamu mwenzako?.
Hivi kweli vita hivi kwa dhulma kiasi hiki vitashinda na kuwamaliza waislamu waliokusudiwa?.
 
CRUSADE AGAINST MALARIA.....CRUSADE AGAINST HIV....CRUSADE AGAINST TUBERCULOSIS.....CRUSADE AGAINST CRIME.......! Hivi malaria nayo ni ya kiislamu? TB nayo ni ki-islamu? HIV/AIDS nayo ni ya ki-islamu? CRIME JE? wajuvi wa lugha watupe maana ya maneno hayo....tunatoka na tafsiri potofu hali kitu ki -wazi kabisa.....! UGAIDI KAMA UGAIDI WETHER NI CRISTIAN TERRORISM OR ISLAMIC TERRORISM upigwe vita kwa mapana yake.....!MASOUD JOIN THE WAR AGAINST TERROR...AND YOU SEEM TO BE A GOOD FIGHTER......!
 
UNAPOAMUA KUWA BONDIA USIOGOPE NGUMI ZA USO.......ninyi wenzetu sijui vipi, mnaanzisha mavalangati mkijibiwa mnakimbilia vyombo vya habari na kusema NGUVU ZILIZOTUMIKA NI KUBWA MNO....kwani nyie mlitumia kidogo?
 
UNAPOAMUA KUWA BONDIA USIOGOPE NGUMI ZA USO.......ninyi wenzetu sijui vipi, mnaanzisha mavalangati mkijibiwa mnakimbilia vyombo vya habari na kusema NGUVU ZILIZOTUMIKA NI KUBWA MNO....kwani nyie mlitumia kidogo?
Vipi unawazungumzia Mayahudi nini?:
"When you go to war do not go as the first, but as the last, so that you may return as the first. Five things has Kanaan recommended to his sons:'Love each other, love the robbery, hate your masters and never tell the truth.' " - Pesachim F. 113B
 
UNAPOAMUA KUWA BONDIA USIOGOPE NGUMI ZA USO.......ninyi wenzetu sijui vipi, mnaanzisha mavalangati mkijibiwa mnakimbilia vyombo vya habari na kusema NGUVU ZILIZOTUMIKA NI KUBWA MNO....kwani nyie mlitumia kidogo?

Hapa nani ni bondia,nani anayetumia nguvu kubwa na kidogo na nani anayekimbilia vyombo vya habari kulalamika?.Au umeamua kutumia usanii wa maneno tu bila kuwa na maana maalum?.
 
Back
Top Bottom