Ufusadi mwingine wa Elimu-English medium primary schools za serikali

Andindile

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
304
16
Serikali katika sera yake ya elimu ilishatamka kuwa lugha rasmi ya kufundisha shule za msingi ni kiswahili na kiingereza kitafundishwa kama somo. Lakini cha ajabu serikali hiyi hiyo inaendesha baadhi ya shule zake kama English medium school. Shule hizi teule ni Olympio, Bunge, Kisutu na moja nimeisahau jina. Watoto wanaosoma katika shule hizo wanapata mahitaji yao yote kama watoto wanaosoma private english medium schools.

Kama wameona shule zinazofundisha kwa lunga ya kiingereza ni bora zaidi kwa nini basi wasibadili sera na kutamka kuwa shule zote za msingi nchini zitafunndisha kwa lunga ya kiingereza! Maana kinacho fanyika sasa ni ufisadi mwingine wa kupindukia wa kuwapatia "bora elimu" watoto wa makabwela na "elimu bora" watoto wa vigogo.

Jamani na tupaze sauti tuseme yatosha! Watoto wa shule za serikali wote wanastahili kupata elimu bora. Kama wameona kiingereza ni bora kufundishia, basi wakitumie katika shule zote.
 
shule hizo wanasoma watoto wa vigogo na watoto wa wafanyakazi wasomi mskini wote kalaga bao!bongo kazi kweli!
 
Back
Top Bottom