Ufunuo wa Mchungaji!

Hajasema hivyo. Labda ukirudia kusoma ujumbe wake utamwelewa fasaha.
Watanzania wengi ni mafisadi siyo kweli ....Watanzania wengi (70%) wanafanya kazi za kilimo, 20% wanafanya kazi kwenye informal sector kazi binafsi kwa maana hiyo kama asilimia 90% wanajishughulisha na kazi zao binafsi kuwa fisadi kwa mkulima wa Tanzania ni ndoto ya mchana... kabisa??? ila yeye anaibiwa na watu wengine??
10% ya watanzania ndio wako serikali na wanasiasa (technorat) hawa ndio wanaofanya ufisadi katika serikali na si watanzania wengi! NO NO big NO!
Rev. Kishoka asema wakulima/mkulima yupi ni fisadi Tanzania?? watu tunakula hard earn money kwenye informal sector wala hakuna uwizi na kodi tunalipa sana...washenzi wako serikali wanatafuna ..ambao less than 10% of all population???
 
Kwahiyo unachosema ni kwamba na wewe Rev. Kishoka!! ni fisadi wa aina fulani...kazi kwelikweli....
Tanzania iko nafuu (lakini ni mgonjwa ukilinganisha na zambia) labda ungelinganisha na nchi yeyote ndio ingekuwa balanced information
Kuna watanzania wengi si mafisadi (wengi sana) ila wanakubali kudanganyika (hapo sawa sawa) ..elimu ya uraia (intensive) will change the minds and behaviour

Tumaini,

Inapofika mahali Mtanzania anatoa fedha apate haki yake kikatiba na kufanya kitendo hicho kuwa ni kitu cha kawadia ili asibugudhiwe, hilo ni ufisadi wa namna yake.

Swali ni kwa nini Mtanzania huyu asifuate taratibu na kanuni?

Mfano majuzi pale Dar kulikuwa na kupewa stika za Usalama barabarani ambazo ni shilingi 3,000/= lakini kutokana na upuuzi wa mapolisi na kujivutavuta, Watanzania wanaamua kununua stika kuonyesha kuwa gari limekaguliwa kwa shilingi 10,000/= kisa kuachana na usumbufu wa polisi na kupoteza muda na kukaa siku nzima ukibabaishana na Polisi wa Trafiki wanaotaka kukutoa upepo!

Sasa kama huo si Ufisadi ni nini?
 
Watanzania wengi ni mafisadi siyo kweli ....Watanzania wengi (70%) wanafanya kazi za kilimo, 20% wanafanya kazi kwenye informal sector kazi binafsi kwa maana hiyo kama asilimia 90% wanajishughulisha na kazi zao binafsi kuwa fisadi kwa mkulima wa Tanzania ni ndoto ya mchana... kabisa??? ila yeye anaibiwa na watu wengine??
10% ya watanzania ndio wako serikali na wanasiasa (technorat) hawa ndio wanaofanya ufisadi katika serikali na si watanzania wengi! NO NO big NO!
Rev. Kishoka asema wakulima/mkulima yupi ni fisadi Tanzania?? watu tunakula hard earn money kwenye informal sector wala hakuna uwizi na kodi tunalipa sana...washenzi wako serikali wanatafuna ..ambao less than 10% of all population???

I'm impressed by your counterargument. Plausible and exceptionally brilliant. Yet, I think there is a clause in his narrative you seem to have overlooked and therefore excluded from your disputation. Please take a look at at this one " ...Mafisadi kwa namna yao." Je, wakulima kutokuwa mbele kwenye kudai haki zao ni moja ya ufisadi? Kwa maana kwamba wakulima wangelikuwa pro-active kuwawajibisha wabunge (kutokubali kulaghaiwa - ufisadi) vijijini kwa ahadi zao time and time again kwenye majukwaa yaleyale na ahadi zilezile zisizotimilika wangelifanya jambo la maana na hivyo kupunguza ahadi hewa za wabunge. In return kuwa mfano kwenye sectors nyingine. What is your opinion on this?
 
Kuna jamaa alipata ofa ya kazi ofisi moja ya serikali sasa akawa anasitasita kutokana na mshahara aliotajiwa alikuwa anauona kuwa ni mdogo. Wenyeji wakamwambia asiwe na wasiwasi kuhusu mshahara mdogo mambo yatajiseti yenyewe, in fact atafikia mahali atakuwa haugusi kabisa huo mshahara!
 
Hapo ndipo mimi naposema wanaoshindwa kufuata utaratibu na kutoa huduma ni "technorat" mfano polisi, public servants, walimu etc ambao ni asilimia chini 10% ya watanzania wote comredi hao ndio mafisadi ambao wanatusababishia usumbufu asilimia 90% ya wabongo wote tunaonekana tumeoza..kisa wao..wengine kwenye sector zetu (informal) unatafuta shilingi haki bin haki halal bin halal lakini..mafisadi (10%) always wanachukua zaidi na zaidi...bado naamini wengi wa waTanzania ni wazuri tena sana infact ni wacha mungu..ila wasomi (officers) na politicians ndio greedy greedy ..hence all problems ulizozitaja??
 
Kuna jamaa alipata ofa ya kazi ofisi moja ya serikali sasa akawa anasitasita kutokana na mshahara aliotajiwa alikuwa anauona kuwa ni mdogo. Wenyeji wakamwambia asiwe na wasiwasi kuhusu mshahara mdogo mambo yatajiseti yenyewe, in fact atafikia mahali atakuwa haugusi kabisa huo mshahara!

Sadly, that is mostly the case!

Kama walivosema wengi rushwa imekuwa sehemu ya mfumo na mfumo umeihalalisha kwa namna yake!

Yaani sheria zinaatungwa ili kuhalalisha baadhi ya ufisadi huu wa kimfumo..mfano hili la wabunge kujilipa hadi 100,000 sitting allowance kwa siku, huku wakipokea unprecidented 7m per moth? na nasikia itakuwa 12m...
hapo hapo mkulima wa korosho au wa pamba anapambana na ponjoro anayetaka kununua kwa bei anayotaka kwa kisingizio cha soko huria (isomeke soko holela)
 
I'm impressed by your counterargument. Plausible and exceptionally brilliant. Yet, I think there is a clause in his narrative you seem to have overlooked and therefore excluded from your disputation. Please take a look at at this one " ...Mafisadi kwa namna yao." Je, wakulima kutokuwa mbele kwenye kudai haki zao ni moja ya ufisadi? Kwa maana kwamba wakulima wangelikuwa pro-active kuwawajibisha wabunge (kutokubali kulaghaiwa - ufisadi) vijijini kwa ahadi zao time and time again kwenye majukwaa yaleyale na ahadi zilezile zisizotimilika wangelifanya jambo la maana na hivyo kupunguza ahadi hewa za wabunge. In return kuwa mfano kwenye sectors nyingine. What is your opinion on this?
Pro-active kwa Mkulima bro..unachekesha..wewe ulishafanya kazi ya kilimo na ugumu na unavykuwa busy..na elimu ya hao jamaa hakuna muda wa ku-think sana kwenye sector hiyo ...hiyo ni problem number elimu, busy, lack of infomation etc
Nilitoa suggestion kwamba katika hao mafisadi (10%) of the population ndio kuna wasomi, wanasiasa, officers (public servant), walimu, polisi etc hawa wote wana-advantage mbili first wana elimu lakini wameamua kuwa mafisadi -they are competing in doing sins (polisi anaiba, public servant anaiba, pccb anaiba etc hakuna wa kumshika mwingine ..deals tu kwa mbele??? second advantage wako informed ..(information is power)..
Bottom line: wasomi + wanasiasa waki-change ufisadi utaisha
how?: civil education and political will (change) ...
 
Sadly, that is mostly the case!

Kama walivosema wengi rushwa imekuwa sehemu ya mfumo na mfumo umeihalalisha kwa namna yake!

Yaani sheria zinaatungwa ili kuhalalisha baadhi ya ufisadi huu wa kimfumo..mfano hili la wabunge kujilipa hadi 100,000 sitting allowance kwa siku, huku wakipokea unprecidented 7m per moth? na nasikia itakuwa 12m...
hapo hapo mkulima wa korosho au wa pamba anapambana na ponjoro anayetaka kununua kwa bei anayotaka kwa kisingizio cha soko huria (isomeke soko holela)

System yetu inahalalisha watu kupata income zisizo rasmi; watu wanaishi kwa allowances, per diems etc...wasio kwenye nafasi hizi wanaishia kufanya utapeli kwa namna nyingine.
 
Ujinga ni pale wanapobadilisha income zisizo rasmi kuwa ni allowance?...inakuwa balaa??
 
Labda niandike kwa namna nyingine nitumie takwimu na data nyepesi!

Mtu A anakaa Kibamba ambayo ni Kilometa 25 kutoka katikati ya jiji la Dar. Mtu huyu tumpe jina Masumbuko.

Masumbuko ana gari lake, ki-Rav4 na anafanya kazi pale NDC kama mtathmini wa Takwimu. Ana mke na watoto watatu.

Kila siku, Masumbuko anaamka saa 10 asubuhi, ili aanze kujiandaa kwenda kazini na kuwaanda Watoto wanaokwenda shule. Masumbuko anaondoka nyumambani kwake pale Kibamba ambako ni katikati ya Kwembe na Mbezi Luis saa 11 na nusu alfajiri. Safari yake ya kwenda kazini inamchukua masaa mawili au mawili na nusu. Kazini anatakiwa aingie saa 2 kamili asubuhi.

Tangu anapoingia barabara kuu ya Morogoro kuelekea mjini Dar Es Salaam, Masumbuko anasuasua kwenye foleni kwa masaa mawili huku gari likipiga kati ya gia ya kwanza na ya pili kutokana na msongamano. Kila baada ya kilometa moja au mbili kuna matuta seti tatu.

Masumbuko anaingia kazini saa 2 kasorobo, hapo katumia masaa mawili na karibu lita 6 za mafuta.

Muda wa kazi kwa kila siku kwa Masumbuko ni masaa 8 ya kazi tangu akiingia saa 2 asubuhi mpaka saa 11 jioni. Mahesabu ya haraka yanasema Masumbuko anaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa masaa matano na nusu (5:30) kwa siku na hayo masaa mengine ni muda wa majeraha.

Ikifika saa 11 jioni, Masumbuko anaanza safari yake ya kurudi Kibamba na anakwama kwenye foleni kwa muda wa saa kaibu tatu, na hapa anamaliza lita karibu 8 za mafuta!. Haingii nyumbani mpaka saa 2 usiku.

Akifika nyumbani ndio asalimiane na mke na watoto, awajulie hali, aandalie mchicha wake pale nje kwa kutumia kurunzi na ahangaike kwenda kujaza maji kwenye Tanki la maji. Lakini kwa bahati mbaya, hakuna umeme, kuna mgao na maji pamoja na kuwa yana nguvu kidogo, lakini hawezi kujaza mapipa yake ya maji mpaka umeme urudi saa 5 usiku!

Masumbuko anakaa macho mpaka umeme unaporudi hapo saa 5 usiku na anatumia saa moja kujaza mapipa yake ya maji na anapoingia kitandani kulala ni saa 7 Usiku.

Ikifika saa 10 asubuhi, jogoo la pili linapowika, Masumbuko keshaamka, anajiandaa haraka ili awaone watoto na akimbilie kuwahi foleni.

Leo ni Jumatano, masumbuko ameamua kuacha gari na kupanda Kipanya, nacho kinachukua muda ule ule wa masaa mawili asubuhi lakini anapata ahueni maana nauli ni shilingi 1,500/= kwa safari yake mpaka mjini na si kumaliza lita 6 akiwa ndani ya Rav 4 yake.

Akiwa kazini, leo JUmatano, Masumbuko anawaza kama kutakuwa na maji akirudi nyumani maana Dawasco wamekata maji wakidai kuna maji yanaletwa na Wachina. Ama Masumbuko anatafakari kama kutakuwa na umeme akifika nyumbani na kama foleni itakuwa na ahueni maana kapanda kipanya!

Siku nzima Masumbuko katawaliwa na mawazo ya tangu alipoamka na atarudi vipi nyumbani ili awahi kuwaona watoto wake, aende kununulia wale kuku zake chakula na apate kupumzika kwa kutosha.

Matokeo ya tija na ufanisi kwa siku ya leo kutoka kwa Masumbuko ni saa moja na nusu la yyeye kufanya kazi kwa ufanisi na tija.

Jioni inafika Masumbuko huyo anakimbilia Posta mpya akapande Kipanya arudi Kibamba.

Sasa Masumbuko ni lini na ni wakati gani atakuwa na amani ya moyo kuwa anaweza kuleta uwiano wa maisha yake ya nyumbani na ajira yake? Je Masumbuko atawezaje kuendelea kuwa na tija na ufanisi ikiwa siku nzima akiwa kazini anawazia kero za yeye kuja kazini kwa kuganda kwenye foleni, kukosekana maji na umeme na kikubwa kukosa muda wa kukaa na mke na watoto kwa muda unaotosha?

Je ile ndoto ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania itatimilikaje ikiwa Masumbuko anasumbuka kila siku kwa hizi kero pamoja na kuwa ana ajira?
 
Watanzania wengi ni mafisadi siyo kweli ....Watanzania wengi (70%) wanafanya kazi za kilimo, 20% wanafanya kazi kwenye informal sector kazi binafsi kwa maana hiyo kama asilimia 90% wanajishughulisha na kazi zao binafsi kuwa fisadi kwa mkulima wa Tanzania ni ndoto ya mchana... kabisa??? ila yeye anaibiwa na watu wengine??
10% ya watanzania ndio wako serikali na wanasiasa (technorat) hawa ndio wanaofanya ufisadi katika serikali na si watanzania wengi! NO NO big NO!
Rev. Kishoka asema wakulima/mkulima yupi ni fisadi Tanzania?? watu tunakula hard earn money kwenye informal sector wala hakuna uwizi na kodi tunalipa sana...washenzi wako serikali wanatafuna ..ambao less than 10% of all population???

Tuma,

Hata vijijini kuna Ufisadi, usijidanganye. Tena huko ndio mbaya kabisa unaandamana na wivu, ulevi na ushirikina!

Umeshaona jinsi watu "wanavyosaidiana" mbolea? watu wanakwenda pulizia mbolea shamba la jirani ili mazao ya nyauke!

Kule Singida Wamang'ati wamekwenda na kuhakikisha ng'ombe wote wa Wanyaturu na wanyiramba wanaugua na kufa hivyo wenye ng'ombe wamebakia ni wao pekee!

Nenda Uchagani, watu wanaibiana mahindi kupeleka Kenya.

Kyela je, fitina kila kona na koo kazi kuchomeana kwa Serikali za vijiji na chama Twawala!
 
Pro-active kwa Mkulima bro..unachekesha..wewe ulishafanya kazi ya kilimo na ugumu na unavykuwa busy..na elimu ya hao jamaa hakuna muda wa ku-think sana kwenye sector hiyo ...hiyo ni problem number elimu, busy, lack of infomation etc
Nilitoa suggestion kwamba katika hao mafisadi (10%) of the population ndio kuna wasomi, wanasiasa, officers (public servant), walimu, polisi etc hawa wote wana-advantage mbili first wana elimu lakini wameamua kuwa mafisadi -they are competing in doing sins (polisi anaiba, public servant anaiba, pccb anaiba etc hakuna wa kumshika mwingine ..deals tu kwa mbele??? second advantage wako informed ..(information is power)..
Bottom line: wasomi + wanasiasa waki-change ufisadi utaisha
how?: civil education and political will (change) ...

Tumaini,

Nini maana ya Ufisadi na Fisadi? je kuna tofauti gani na Uhujumu na Mhujumu?
 
Rev. Kishoka..
Uendele hivi .....Masumbuko anafanya kazi tanesco ni mwanasheria ni katika wale walioshauri nchi kuingia mkataba mbovu akapata 10% akajenga nyumba kibamba na kununua gari Rav 4, na rafiki yake mwingine yuko dawasco ni injinia walimaliza wote UDSM amekata maji kibamba kwa sababu ana biashara ya kuuza maji maeneo hayo naye amenunua gari na kujenga nyumba kimara..on and on and on....cycle iko hivyo kwa hao wasomi wetu (10%) ya watu wetu wanatusumbua sisi 90% of population kwa hiyo napinga hoja yako kwamba wengi ni mafisadi, mafisadi ni less than (10%) wanasababisha mess up ya ajabu kwenye whole formula?
Ambacho masumbuko hajui ni kwamba yeye ni chanzo kwa kiwango gani?? bado kujua wala hajawahi kujiuliza ??
 
Tuma,

Hata vijijini kuna Ufisadi, usijidanganye. Tena huko ndio mbaya kabisa unaandamana na wivu, ulevi na ushirikina!

Umeshaona jinsi watu "wanavyosaidiana" mbolea? watu wanakwenda pulizia mbolea shamba la jirani ili mazao ya nyauke!

Kule Singida Wamang'ati wamekwenda na kuhakikisha ng'ombe wote wa Wanyaturu na wanyiramba wanaugua na kufa hivyo wenye ng'ombe wamebakia ni wao pekee!

Nenda Uchagani, watu wanaibiana mahindi kupeleka Kenya.

Kyela je, fitina kila kona na koo kazi kuchomeana kwa Serikali za vijiji na chama Twawala!
Well said...lakini impact ya mtu wa singida kumuonea wivu mkulima moja au wawili iko remote sana kwenye uchumi mpana wa nchi...mambo mengi vijijini siyo ufisadi ila "NI UHALIFU" ambao wanasiasa na technorat (mahakama, polisi, etc) wanweza kufuta kabisa??
Ufisadi wa kuchukua deal (richmond) for example umeme unakosekana, viwanda vinashindwa kuzalisha, ajira zinafutwa, mafuta yanapanda bei etc..mimi huo wa kijijini nauita uhalifu tu wala sio ufisadi...
 
Rev. Kishoka..
Uendele hivi .....Masumbuko anafanya kazi tanesco ni mwanasheria ni katika wale walioshauri nchi kuingia mkataba mbovu akapata 10% akajenga nyumba kibamba na kununua gari Rav 4, na rafiki yake mwingine yuko dawasco ni injinia walimaliza wote UDSM amekata maji kibamba kwa sababu ana biashara ya kuuza maji maeneo hayo naye amenunua gari na kujenga nyumba kimara..on and on and on....cycle iko hivyo kwa hao wasomi wetu (10%) ya watu wetu wanatusumbua sisi 90% of population kwa hiyo napinga hoja yako kwamba wengi ni mafisadi, mafisadi ni less than (10%) wanasababisha mess up ya ajabu kwenye whole formula?
Ambacho masumbuko hajui ni kwamba yeye ni chanzo kwa kiwango gani?? bado kujua wala hajawahi kujiuliza ??

Well huyu Masumbuko wako ni tofauti na wa kwangu. Wa kwako anafanya kazi Tanesco ndiye mhujumu, wangu yuko NDC, mtu wa kawaida lakini naye ana ufisadi wa namna yake kama vile kulipa shilingi 5,000/= ili ajaze mapipa yake maji lakini hapewi risiti na fedha hazifiki Dawasco!
 
Inawezekana masumbuko wako kampuni yake ndiyo iliyoshinda tender ya kusambaza mabomba ya maji kibamba kutoka dawasco of course kampuni ilitoa 10% ili ishinde lakini inabidi dawasco wakubali kazi ambayo ni below standard kwa hiyo mabomba yatasambazwa sehemu chache (siyo kibamba yote)...na kumbuka oficer wa dawasco (msomi) anayekuja kukusanya kodi ya maji...ana bei mbili bei ya kupewa maji bila risiti na bei ya kupewa maji kwa risiti..(masumbuko atachagua bei ndogo bila risiti)...wasomi wanakula wao kwa wao kwanza, halafu kwa pamoja wanatufyonza sisi (90%) of the population
Bottom line: watanzania wachache wanafanya ufisadi na wanafanya mess up whole formula.
 
Je yule mlinzi ple getini mambo ya ndani aliyenipia mzinga kisa kanionyesha ofisi ya Utawala naye tumuiteje?

Au wale jamaa wa Swissport pale JKNIA ambao walipogundua mimi mbeba maboksi kidogo wanifanyie sherehe kwa kudai chai na vitumbua nao huo si ufisadi?

Je Afande pale Ubungo terminal ambaye haishi kusimamisha mabasi na malori dizaini fulani lakini mengine yanapeta naye si Fisadi wa namna yake?

Kwani fisadi ni lazima awe msomi?

Je Mwenyekiti wa kijiji ambaye kaamua kuzuia maji yasiletwe na mtu mwingine kijijini ila mpwa wake pekee pale Msata jirani na Wami naye utadai ni msomi na si fisadi?
 
Hawa wote ni "WAHALIFU" siyo mafisadi
 
System yetu inahalalisha watu kupata income zisizo rasmi; watu wanaishi kwa allowances, per diems etc...wasio kwenye nafasi hizi wanaishia kufanya utapeli kwa namna nyingine.

Mi nakwambia kuna rafiki yangu kabisa kaajiriwa serikalini majuzi tu..kanambia kama ukiwa hufahamiani na wakubwa kwa maana ya wakuu wa vitengo na wakurugenzi 'deal' zinakupita mbali na nunaishia kusugua benchi tu..

lakini ukikaa nao vizuri..safari kila siku na huko ndo kwenye ulaji...hivi kwa mwezi ukiwa na siku 10 za 'safari' kwa rate ya 50,000/- hiyo ni laki tano safi kabisa! hujaweka za vikao vya ofisini visivo na kichwa wala miguu..mwisho wa mwezi una milioni moja na mshahara juu! ndo institutionalization hiyo! so sad indeed
 
Rushwa imekuwa kansa inayoanza kusambaa karibu mwili mzima. Huyu pepo wa rushwa atatumaliza. Lakini pia uvivu uliokithiri miongoni mwetu umetufanya tuwe wafanyakazi wa mazoea.Hatuna creativity yoyote kazini. Hatuna hamasa ya kuona tunaboresha mambo. Nchi sasa itaendeleaje? Kazi za kutumia maarifa tunagawa kwa kutumia rushwa. Ila tujue tunafanya haya yote hasara ni ya kwetu wenyewe
 
Back
Top Bottom