asha ngedere
Member
- Nov 6, 2009
- 92
- 11
Hatimaye Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) limeanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa kampeni ya CHADEMA kutoka viwanja vya Jangwani, leo, Jumamosi, Agosti 28, 2010, kuanzia takriban saa 9.30 alasiri.
Viongozi wote waandamizi wa CHADEMA, wakiwemo wagombea wote, wameonekana, na hivi sasa kuna utambulisho wa wagombea, baadhi yao wakiwa wamepangwa kuzungumza, kama vile Mpendazoe, Shibuda, Tundu Lissu, Halima Mdee, na wengineo, bila kumsahau mgombea Urais Dk. Wilbroad Peter Slaa na mgombea mwenza Mzee Ali Mzee.
Kumekucha!
-> Mwana wa Haki
P.S. Sugu ametambulishwa na "ana nafasi yake maalum".
Mheshimiwa Tundu Lissu amemwaga ugali na mboga. kumbe JK alihusika kusaini mkataba wa kuwafukia wachimbaji Bulyankulu? Hebu wadau tupeni uhondo huu.