Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
LIVE: Hivi sasa TBC1 inarusha matangazo ya moja kwa moja kutoka viwanja vya Jangwani hapa Dar, yakionesha uzinduzi wa kampeni ya CHADEMA.
Kampeni imezinduliwa kwa sala, ambapo mtoto wa Sheikh Yahaya Hussein, Hassan Yahaya Hussein ametoa dua kwa Kiislam naye Grace Shellukindo maombi kwa Kikristo.
Sasa baadhi ya wagombea na viongozi wa CHADEMA wanaongea. Kwa kweli kuna umati mkubwa sana wa watu wa rika mbali mbali, wengi wao wakiwa watu wazima, watoto ni wachache.
Waliosema TBC1 inawapendelea CCM sasa mkae mkao wa kula. TBC1 ni chombo cha UMMA, hakina ubavu wa kupendelea upande wowote ule wa chama cha siasa, kwa kuwa inaendeshwa kwa kodi za Watanzania, walio na wasio wanachama wa vyama vya siasa.
-> Mwana wa Haki
P.S. Dhana ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya inachambuliwa....