Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Very contradictory!!!Naamini watanzania wana macho na masikio.Kama wapinzani ni wa dizaini hii,CCM itakuwepo for lots of years to come.

Uko sawa kabisa ndugu, mf sasa hivi kikwazo kikubwa cha CHADEMA ni wapinzani zaidi kuliko hata CCM yenyewe, sbb mi sion kwa nini hawajaunganisdha nguvu kum-support Slaa amabaye anaonekana anakubalika. Matokeo yake ni kwamba wanataka kura zigawanyike kusudi CCM ishinde. Vyama pinzani hapa Tanzania ni viwili tu CHADEMA na CUF ile ya Zanzibar (CUF ya bara ni mamluki tu hawana kitu). Inanishangaza sana unakuta watu waelewa kama akina Mvungi lakini eti wako TLP, unajiuliza maswali mawili unakaa kimya, ...sijui kama ni kweli!
 
Unauhakika Tanzania hakuna Tatizo la uchumu? Dr. Slaa ni kilaza ndio maana mpaka akumbushwe ndio afanye kitu.

Mkuu hata mimi nakubaliana na wewe 100% kuwa Dr. Slaa ni kilaza na kuthibitisha hilo inabidi Dr. Kikwete asimame na Slaa kwenye mdahalo ili tulithibitishe hilo, au wewe unaonaje?
 
Mheshimiwa nimebahatika kuhudhuria mikutano ya vyama vya CUF,CCM na Chadema vyama viwili vya mwanzo vinaeleza Dira na sera zao kwa wananchi kuwa mkituamini tutafanya hiki na kile karibuni kwenye kila eneo.Chadema aliingia Marando akasema watashughulikia Mafisadi,Mbowe akazungumzia Mafisadi na Elimu kuwa haina maana sana kwenye Uongozi.kuwa na darasa la saba Mgombea Mwenza haina tatizo.Alipopanda Slaa akaja na Habari za UFISADI akaanza kutaja kesi za kisutu na ufisadi wa nyimbo za kizazi kipya kuwa kazi zao zinafisadiwa na CCM, akaingilia Point ya Mr.Sugu na Ruge Ugomvi wa NO MORE MALARIA.siku muhimu kama hiyo unajadili mambo kama hayo ya ugomvi wa mtu na Mtu?

Mheshimiwa Shibuda alipoona mambo si Mambo akamuandikia kidesa-memo- Slaa kuwa Mzee sema Chochote kuhusu Uchumi. Mzee Slaa akapayuka Live kuwa Nakushukuru Shibuda kunikumbusha nizungumzie Uchumi.Kimsingi mtu makini atajiuliza mengi sana juu ya umakini unaodaiwa kuwa nao Chadema. nadhani unaweza kutafuta mkanda wa Video au jaribu kwenye You Tube uone walivyoshindwa kutumia simu muhimu wa kunadi sera zao kwa wananchi. akikazania kesi za Mahakama ya Kisutu inaoneka Slaa na Mbowe walipenda wawe waendesha Mashitaka na mwingine awe hakimu.dhamira yao haioneshi wanataka kuongoza Nchi inaoneka wanataka kuwa Prosecutors.

Kweli Shibuda kawapa mchango mkubwa sana tena siku ya kwanza kuhudhuria mikutano yao.Dj Mbowe kwenye kuongea alikuwa na nafuu kubwa kuliko Slaa aliyekuwa akijiumauma.Mbowe ametumia uzoefu wake wa UDJ jana.
Mkuu nilikuwepo kwenye mkutano, Ruge alitajwa mara moja tu tena na msanii wa bongo flava alipokuwa anatoa risala. Dr. Slaa aliongea zaidi mambo makuu 9 yaliyomo kwenye manifesto ya uchaguzi, mojawapo ni kubadili katiba ambayo wananchi hawafahamu kuwa ina uhusiano moja kwa moja na mustakabi wa maisha yao, kwa mfano kiongozi wa Takukuru atawajibika kwa bunge na sio kwa raisi ili rais akiiba aweze kukamatwa pia.

Pia alizungumzia kuwa maendeleo ya tertiary industries ambayo yanaignite uchumi wa nchi ndio kipaumbele na raslimali nyingi tunazo. Pia aliongea kuhusu mapato ya serikali karibu asilimia 75 yanatumika kuendesha serikali ambapo si vema.

Mkuu wa mkoa mmoja anatembea akiwa na zahanati ikiwa ni thamani ya shangingi lake. Na akasema CHADEMA watafanya nini badala yake.

Dr. Slaa is, in my book, a master of content, a master detail. No wonder Kikwete hawezi kusimama nae kwenye mdahalo!!
 
katika kuondoa dhana ya UDINI kwenye chama cha Chadema mgombea mwenza wa Chadema alivyalishwa Kanzu ili kuonekana ni chama cha wote.cha kujiuliza ni kuwa siku ya Slaa anatangaza nia ya kugombea watu wote walitokea.isipokuwa wabunge wa Kiislam walisusa baada ya kuona kuwa ni mpango wa maaskofu.kumpa shavu Slaa.Zitto KABWE,Muhonga na Alfi hawakutokea.

kitendo cha kuvalishwa kanzu mgombea yule mgombea ni danganya toto.cha ajabu ni mgombea yule akasema kuwa Chadema hakuna udini na yeye kapata chance ya ugombea.
akasema Chadema kuna usawa wa hali ya juu.swali jee kwenye viti maalum kuna mtu kapewa toka Zanzibar? jibu hakuna.

Ulichoandika ni tafsiri yako kwa vile tayari una udini ndani mwako. Unatakiwa uondoe 'prejudices' kwanza ili uweze kutoa hoja inayojitosheleza na siyo tafsiri yako. Kwani vyama ambavyo kiongozi ni mwislamu wakimchagua mkristo ni danganyatoto pia au ni kwa Chadema tu?
 
katika kuondoa dhana ya UDINI kwenye chama cha Chadema mgombea mwenza wa Chadema alivyalishwa Kanzu ili kuonekana ni chama cha wote.cha kujiuliza ni kuwa siku ya Slaa anatangaza nia ya kugombea watu wote walitokea.isipokuwa wabunge wa Kiislam walisusa baada ya kuona kuwa ni mpango wa maaskofu.kumpa shavu Slaa.Zitto KABWE,Muhonga na Alfi hawakutokea.

kitendo cha kuvalishwa kanzu mgombea yule mgombea ni danganya toto.cha ajabu ni mgombea yule akasema kuwa Chadema hakuna udini na yeye kapata chance ya ugombea.
akasema Chadema kuna usawa wa hali ya juu.swali jee kwenye viti maalum kuna mtu kapewa toka Zanzibar? jibu hakuna.

Kumbe tatizo lako ni kuwa wazanzibari hawakupewa nafasi wanayostahili! Wakati kuna wenye madigirii kibao amechaguliwa asiye na elimu ya juu! Lakini hao marais wenu wa Zanzibar wana au walikuwa na elimu gani ya kutisha? Wewe kama unaona hawa jamaa Chadema ni wadini na wenye haki ya kuvaa kanzu ni CUF peke yao, basi wanyeme kura yako! Wale ambao wanajali zaidi integrity kuliko kijikaratasi ( hasa ukizingatia vyengi ni vya kununua) watawapa kura zao!

Amandla.........
 
Nilitazama matangazo ya TBC1 ya moja kwa moja ya uzinduzi wa kampeni, na nilisikiliza hotuba ya Dk. Slaa.

Padri, Slaa HAKUWAZUNGUMZIA Ruge na THT, kwani hata kwa mtazamo wangu, hao ni watu WADOGO sana kuzungumziwa na mtu kama yeye. Ni wadogo kuliko piriton!

Slaa alizungumzia mipango ya CHADEMA itakayotekelezwa ndani ya siku 100 za urais wake. Ruge na THT wanaingia wapi kwenye agenda hiyo?

Nimekubaini, wewe ni MAMLUKI wa CCM, umekuja hapa kupandikiza maneno, kupoteza dira.

Nitaendelea KUWAUMBUA ninyi mamluki wote MPAKA MUONDOKE humu ndani. Mnachojua ni porojo, wala hamna HOJA!

Hatuna muda wa kuongea PUMBA! Tunataka hoja.

Kwa taarifa yako, Shibuda HAKUZUNGUMZIA uchumi!

Slaa HAHITAJI kukumbushwa na Shibuda. In fact, Shibuda aliwataka wananchi kumuunga mkono Slaa, na yeye pia alitangaza kumuunga mkono, lakini HAKUMKUMBUSHA juu ya uchumi. Hilo, Slaa HAHITAJI kukumbushwa na mtu yeyote!

NIPOTEZEE!

-> Mwana wa Haki

Padri, Nostradamus, na wengineo, nimewaongeza kwenye IGNORE LIST yangu!

Nafikiri wanaongelea kukumbushwa pale walipokuwa wakimgusa Slaa na kumnog'woneza, na hii ilikuwa ni ktk kumtaarifu juu ya muda na mkwara wa tbc1 kutaka kukatiza matangazo, sasa kwa mtu asiyeweza fikiria mbali kwake yeye hiyo ni kumkumbusha!
 
Back
Top Bottom