Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Hapo Dar unataka kufugia ktkt ya mji au nje ya mji? Kuna mfugaji mmoja mzuri na ana mbegu bomba pale Mapinga, na mwingine yupo Msakuzi. Unataka piglets wangapi?

kwakua ndo naanza nilitaka kama 10 ivi,nataka nifugie nje ya mji maeneo ya bunju,kwa wastani anauza piglet m1 bei gan?
 
:happy:Mwanajamvi nimependezewa sana na hii idea.Ila nataka kujua kwa nguruwe ambae ni tayari kwa kuuzwa,anauzwa bei gani???
 
Mkuu, ni vizuri kuanza kufuga na piglets au wakubwa (kama vile majike wawili na dume moja)?
 
:peace:Mpwa hii ni zaidi ya kuelimika,nimeisoma ilivyo na nimeipenda sana.Yah,cha muhimu kama unavyosema ni kujitoa ilivyo(devotion),isitoshe kwa mafanikio yoyote yale yanakuja kwa staili hiyo.ngoja na mimi nifanye tathmini ya mtaji niingie msituni.NO RETREAT NO SURRENDER...
 
Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
Banda la mabanzi=1,000,000
Chakula = 1,000,000
Dawa= 200000
After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,
utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000
After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700
Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike)
Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.
Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha
Nguruwe tu.


nakupenda saana mpwa,

Sasa naona umeweka mazuri tu , lakini weakness zake hujaziweka, mi navyojua hii biashara inahitaji commitment sana , tena pasua kichwa, siku zote mwenye biashara hii ukipishana nae lazima usikie harufu ya nguruwe hapo inaonyesha ni jinsi gani commitment yake itakavyokuwa.
 
Sasa naona umeweka mazuri tu , lakini weakness zake hujaziweka, mi navyojua hii biashara inahitaji commitment sana , tena pasua kichwa, siku zote mwenye biashara hii ukipishana nae lazima usikie harufu ya nguruwe hapo inaonyesha ni jinsi gani commitment yake itakavyokuwa.

Uko sahihi sana Mkuu, hii ni kwa wale walio committed tu, kwa less committed sijajua biashara wanayoweza kufanya kilelemama n a ukapata pesa!..hii ni kutokana na uzoefu wangu, ukiwaachia wafanyakazi kufanya kila kitu utakuta wameuza madawa na nguruwe wote wanakufa, hii ni ngumu kwa vijana wa sasa hamuwezi kupiga mswaki nguruwe!
 
Tegu (Tapeworm) ni aina mojawapo ya minyoo inayosababisha ugonjwa unaojulikana kitaamu kama Cysticercosis na hii inatokana na kuwepo kwa viuvimbe vingi ndani ya viungo vya mwili vilivyojaa majimaji. Aina ya tapeworm

inayosababisha ugonjwa huu inajulikana kwa jina la kisayansi kama Taenia solium. Hatua ya lava iitwayo cysticercus ndiyo yenye madhara na ndo kiini cha jina la ugonjwa huu. Tegu wakubwa ambao mara nyingi wana urefu zaidi ya mita

moja hukaa kwenye utumbo mwembamba lakini ni mara chache sana wanaweza wakasababisha ugonjwa. Madhara yaletwayo na ugonjwa huu ni makubwa ikiwemo ya kiuchumi kwa vile nyama ya nguruwe mwenye ugonjwa hutupwa yote, lakini pia ugonjwa huleta mdhara makubwa umpatapo mwanadamu. Ugonjwa huu upo sehemu mbalimbali za

Tanzania na madhara yake yamekuwa ni makubwa situ kwa wafugaji bali hata kwa walaji wa nyama ya nguruwe. Tafiti nyingi sana zimefanywa na wataalamu kutoka SUA katika kitivo cha tiba ya mifugo na kubaini uwepo wa ugonjwa huu hasa maeneo ya Mbulu, Mbeya, Iringa, Morogoro na mengine mengi tu. Ugonjwa huu uko karibu maeneo yote duniani isipokuwa haujawi kuripotiwa katika maeneo ya Pasifiki pekee.


UENEAJI WA UGONJWA HUU
Ugonjwa huu unasababishwa na tegu (Taenia solium) wakiwa katika hatua ya lava, na nguruwe anaupata ugonjwa huu anapokula chakula kilichochanganyikana na kinyesi cha binadamu chenye mayai ya tegu. Wakati mwanadamu

anaupata ugonjwa huu anapokula nyama ya nguruwe yenye ugonjwa huu ambayo haikupikwa vizuri au kwa bahati mbaya akimezaa mayai ya tegu kutoka katika vyakula vilivyochanganyikana na uchafu wenye mayai ya tegu. Mzunguko mzima wa maisha ya tegu ni kama inavyoonekana kwenye kielelezo hapa chini.







Kulingana na kielelezo hapo juu utabaini kuwa kwa asilimia kubwa kinachofanya ugonjwa huu unendelee kushamili katika maeneo ambapo ugonjwa huu upon i kutokana na nguruwe kula kinyesi cha binadamu. Hivyo ufugaji huria wa nguruwe (kuwaacha wajitautie wenyewe chakula) pamoja na watu kujisaidia hovyo bila kutmia choo ni michango dhahili ya ugonjwa huu nan i maeneo ambayo yanapaswa kurekebishwa ili kuzuia mwendelezo wa ugonjwa huu.


DALILI ZA UGONJWA

a) Dalili kwa nguruwe


Kwa bahati mbaya ugonjwa huu una dalili chache sana kwa nguruwe na mara nyingi si rahisi kuziona nguruwe akiwa hai, hivyo huonekana wakati amechinjwa. Uumuhimu wake ni kule kumpata hasa mwanadamu na kupelekea kukataliwa

hata nyama ya nguruwe na hivyo kuwa hasara kwa mfugaji. Dalili za ugonjwa huu hasa ugonjwa ukiwa kwa nguruwe wengi ni kama zifuatazo;
-Mfumo wa fahamu na misuli huwa huvurugika
-Kuwepo kwa malengelenge katika maeneo kutolea haja kubwa na chini ya ulimi
-Afya hudhoofika
-Mapigo ya moyo hushindwa kufanya kazi
Lava wakiwa chini ya ulimi wa nguruwe
Ukimchinja nguruwe
Ukimchinja nguruwe unaweza kuona uvimbe uliojaa maji yenye malengelenge wenye ukubwa wa milimita 5-8 kwa milimita 3-5. Maji yake huwa na rangi ya kahawia au waridi na wakati mwingine kichwa cha lava huonekana kama nukta nyeupe. Na viuvimbe hivyo vinaweza kuonekana maeneo yafuatayo;
-Kwenye moyo
-Ulimi
-Misuli ya mashavuni, mabegani, koromeo, kiwambo kinachotenganisha mapafu na tumbo na misuli ya mbavuni na shingoni.
-Mara chache viuvimbe vinaweza kuonekana kwenye ini, bandama, ubongo na tezi.
Nyama ya nguruwe ikiwa imejaa vijiuvimbe maeneo mbalimbali
Moyo wenye vijiuvimbe vingi vyenye majimaji ndani
b) Dalili za ugonjwa kwa binadamu

Mwanadamu aliyepata tegu wakubwa mwilini mwake ataanza kutoa mayai kwenye kinyesi kuanzia wiki ya 8 hadi 12. Na tegu wakubwa huweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wakitoa mayai na vipingiri vilivyopevuka kupitia kinyesi kwa muda wa miaka 30. Hii ni hatari sana kwa usambazaji wa ugonjwa. Dalili za ugonjwa huanza kujitokeza kuanzia wiki

moja au miaka kumi na kuendelea tangu awapate hao tegu na mara nyingi lava wakiwa wanakufa.
Mwanadamu awapo na tegu wakubwa mwilini mwake huwa si rahisi sana kutambua, shida huanza anapokuwa na lava.

Mara chache tegu akiwa tumboni mwa binadamu dalili zisizo maalumu kama kuwa mkali bila sababu (anawaka), kupoteza hamu ya kula, kupunua uzito na maumivu ya tumbo, kuharisha na kufunga choo zaweza kujitokeza.
Dalili za ugonjwa huu kwa mwanadamu zaweza kuwa kali kutegemea eneo ambalo lava (vijiuvimbe) wapo ndani ya mwili. Na ni mara chache vijiuvimbe vinaweza kufika sentimita 1-2 hasa kwenye ubongo wa mwanadamu.

-Misuli: Vijiuvimbe kwenye misuli katika maeneo mbalimbali ya mwili kwa kawaida havionyeshi dalili zozote, isipokuwa mabonge ya uvimbe waweza kuyatambua kwa kubonyeza ngozi.
-Macho: Vijiuvimbe vinaweza kuwa vinaelea kwenye macho na kusababisha macho kutokuona vizuri na hata kutenganisha mboni ya jicho.

-Ubongo na uti wa mgongo: Vijiuvimbe hivi vya ugonjwa vikiwepo kwenye ubongo na uti wa mgongo huwa na dalili kama kuuma kichwa, kizunguzungu, kuchanganyikiwa, kuyumbayumba (kukosa urari) na kasha kufa. Kwa muda mrefu

maeneo mengi hapa nchini na kwingineko barani Afrika wamehusianisha ugojnwa huu na ushirikina hasa mgonjwa unapoenda kichwani na kupelekea kwenye ugonjwa wa kifafa. Hapa ndipo hatari kubwa ya ugonjwa huu, kifafa na kifo kwa mwanadamu.

Kifafa
-Ni kawaida ya lava kwenda kwenye mfumo wa fahamu wa binadamu na hasa maeneo ya ubongo. Larva hukaa kwenye ubongo kwa muda mrefu sana kwani hulindwa na kizuizi damu-ubongo. Lakini kwasababu ya lava kufa na kuleta madhara kwenye ubongo dalili za kifafa huanza kuonekana
Uvimbe chini ya ulimi wa mwanadamu mwenye ugonjwa
Jinsi ya kuutambua ugonjwa
-Dalili zilizotajwa hapo juu zitasaidia kuutambua ugonjwa huu zikiunganishwa na za kimaabara.
-Kwenye maabara uchunguzi wa kinyesi cha mwanadamu kuangalia uwepo wa mayai ya tegu kwa kutumia darubini hufanyika.
-Larva wakiwa kwenye ubongo wa binadamu njia za kitaalamu zaidi hutumika kama MRI au CT brain scan. MRI ndicho kipimo chenye uhakika kwani kinauwezo wa kuonyesha hatua ya uvimbe, mahali ulipo na mabadiliko yake. Lakini gharama kubwa za kipimo hiki na gharama za kununua mashine yenyewe imefanya matumizi yake kuwa kwa nchi chache tu ambazo tena ugonjwa huu kwao si tatizo.

Matibabu ya ugonjwa huu

Matibabu ya ugonjwa huu yanalenga hasa tegu wakubwa, kwa wadogo wakiwa ndani ya viuvimbe vyenye ngozi isiyorushu dawa kupita huwa ngumu.

Kwa nguruwe
: Nguruwe watibiwe kwa kutumia dawa ya minyoo ( Oxfendazole ndiyo dawa inayopendekezwa kutumika kuua tegu na lava-ushauri wa mtaalamu ni muhimu)

Kwa binadamu
: Ukiwa nje ya mfumo wa fahamu si wa kutisha na hivyo hauhitaji matibabu maalumu. Dawa za minyoo zinatumika hata kwa wenye lava walio kwenye mfumo wa fahamu japo uponyaji wake si wa uhakika. Lava wakiwa kwenye mfumo wa fahamu upasuaji ili kuondoa uvimbe hushauriwa ufanyike. Lakini matibabu mengine hufanyika yatakayosaidia kushusha dalili za kifafa kabla ya upasuaji kufanyika.

Njia za kuzuia ugonjwa huu


Nguruwe
: Nguruwe wafugiwe ndani ya mabanda na wasiruhusiwe kutembea nje ya banda
-Wapatiwe dawa za magonjwa ya minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu
-Nguruwe wakaguliwe na wataalamu wakati wa kuwachinja na wale wote watakaopatikana na ugonjwa waharibiwe.​
-Chakula na maji wanayopewa nguruwe yawe ni masafi​

Mwanadamu
: Hakikisha nyama ya nguruwe inapikwa kwa ukamilifu, epuka kula nyama isiyopikwa vizuri. Kuwa makini na kiti moto ambacho sasa ni maarufu sana hapa nchini. Lava wanaweza kufa kwa kuweka nyama kwenye friza nyuzi -10 kwa siku 4 au kupika katika nyuzi 45 hadi 50 kwa dakika 15 hadi 20.

-Mboga za majani zioshwe na kupikwa vizuri hasa maeneo ambako wanatumia mbolea ya

nguruwe au nguruwe wanazurula ovyo​
-Hakikisha unanawa mikono kwa maji safi na sabuni mara utokapo chooni na kabla ya kuandaa chakula(Usafi kwa ujumla)​
-Hakikisha vyombo unavyotumia ni safi kwa ajili ya kitimoto na hata matumizi ya kawaida nyumbani​
-Hakikisha matuzi ya choo nyumbani yanafanyika ipasavyo na epukuka kujisaidia sehemu isiyo na choo.​
-Hakikisha unapima choo chako angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu ili kujua hali yako kwa magonjwa ya minyoo​
-Tumia dawa za minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu ili kutibu magonjwa ya minyoo ambayo hayajaanza kuonyesha dalili. Kama eneo lina watu wengi wenye minyoo hii utibuji wa pamoja utasaidia kuzuia mzuko wa maisha ya tegu (Praziquantel na Albendazole zimependekezwa zitumiwe-ushauri wa daktari muhimu).​

Kumbuka
: Mwanadamu ndiye mwenye mchango mkubwa wa kuhakikisha ugonjwa huu unazulikika hivyo elimu ya kutosha kupambana na huu ugonjwa inahitajika kwa kiasi kikubwa sana. Maeneo kama ya Mbeya na Mbuyu

yameonyesha kuwa ufugaji huria/holela wa nguruwe umechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa ugonjwa huu kushamili maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutotumia choo.​

Kwa maeneo yenye minyoo aina ya tegu, kutibu binadamu na nguruwe kwa wakati mmoja ndiyo njia pekee ya kuondokana na huu ugonjwa.


HAYA TENA KWA WALAJI WA KITOMOTO KAZI KWENU MCHANGA WA PWANI HUO MIMI SIMOOOOO
 
Magonjwa yanayoathiri nguruwe

Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija.

Ugonjwa wa miguu na midomo

Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.

Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja. Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.

Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.

Homa ya Nguruwe (Swine fever)

Virusi vinavyosababisha ugonjwa wahoma ya nguruwe huenea kwa harakasana miongoni mwa makundi yanguruwe, na huua kwa haraka sana,lakini hauna madhara kwa binadamuna hauambukizwi kwa binadamu.Nguruwe walioambukizwa waanshikwana vindonda ama mapunyekwenye ngozi. Pia masikio na ngozihuwa mekundu.

Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.

Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.

Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)

Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.

Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.

Kimeta (Anthrax)

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi.

Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.

Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.

NA MARADHI HAYA PIA NI RAHISI KUMPATA BINADAMU ANAYEKULA NYAMA YA NGURUWE.
 
Mchanganuo umekaa vizuri lakini hatujaona effect ya swin flu na mengine

Ni kweli mkuu, lakini unakumbuka hii post ni ya mwaka gani? wapwa zangu wenye hasira walishafuatilia kitambo kaka.
 
Mpwa nimekusikia!Nina vinguruwe vyangu vi3 nime vihasi vyote ila ebu nijaribu kuwa serious coz umenipa mwanga flani.naomba kujua hao vijakazi una walipaje?...
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom