Mkuu uchafu huo uliotaja hapo juu Mimi sifanyi na wala mimi sijadai kuwa ni Msafi au bora kuliko wengine.
Bali ninachofanya ni Kutahadharisha Umma na madhara ya Huyu mnyama.
Kiafya hafai na Ki imani HAFAI.
Thats all.
Mkuu mm nataka kuanza kufaga ni 4,000,000/= natak nianze na 40 nipo moshi ila nitafugia kibosho je garam zao zitazd huo mtaji niliona mpk kufikia hatua ya kuwauza.
Ng'ombe anaweza kuwa analipa kwenye maziwa,kwa vile utamkamua muda mrefu na faida nyingine ni kukuletea ndama,lakini kasoro yake hadi kufikia hatua hizo inachukua muda mrefu sana.Ivi ufugaji wa nguruwe na ng'ombe upi wenye faida nzuri. Msaada apo ktk ufugaji
Mwenye uzoefu wa kufuga nguruwe tunaomba changamoto zakee maana nimejitosaa kufuga hawa jamaa
Mkuu nimependa sana hilo banda, ila niulize huwa hakifanyiwi usafi kwa kuosha na maji sababu umesema hapo kati zinawekwa pumba au nyasi...Wakati nnafikiria namna nafuu ya kufuga nguruwe wengi kwa wakati mmoja nikakutana na mfumo unaitwa Pig Innovation Production System (PIGS).
Mfumo huu bunifu unatumiwa sana philipines kwa kuwa mnamuwezesha nguruwe kufanya vitu anavyopenda kufanya naturally ambavyo ni rooting,wallowing na socialization.Ili nguruwe akue haraka na kuwa productive lazima apate chakula na mazingira muafaka
PIGS ina manufaa yafuatayo
1.Ni nafuu sana ujenzi wake
2.Humpa nguruwe mazingira natural kuweza kukua vema
3.Huwezesha wananyama wengi kukaa sehemu moja
4.Ni rahisi kufanya usafi na mabanda hayana harufu
Shambani kwangu hutumia mfumo huu kuzalisha market pigs i.e nguruwe nnao wakuza na kuwauza kwa nyama.
Katika mfumo huu nguruwe mmoja huhitaji mita za mraba 1-1.5,Hivyo banda la 5mx5m lilaweza kulea nguruwe 15-20.
Hivi ndivyo linavyojengwa(angalia picha ya kwanza)
1.msingi wa tofali au mawe na miti/mabanzi.
2.upande mmoja kwa upana wa 30cm na partition za 25-30cm ni vya kulishia chakula ili kila mnyama apate nafasi
3.upande wa pili ni bwawa la kuogea la upana wa 0.7-1m ili nguruwe akitaka kujipooza anafanya hivyo
4.katikati panachimbwa 60cm-100m na kujazwa mapumba/malamba au nyasi Kwa ajili ya wanyama ku root au kupumzika
Mfumo huu ni very cost effective,banda la namna hiyo hujengwa kwa around 1.5m shambani kwangu.Ni matumaini yangu itawasaidia wanaopata shida ku design banda ufugaji nguruwe kwa ajili ya mauzo
Upendo kwanza,
Ahsante kwa input nzuri.nadhani wadau watakuwa wamekupata.
Bwana ngamba,
Nguruwe wa kawaida hadi miezi 6 anahitaji 1.5square metre ya eneo.kwa mfano 2mx3m wanaweza kukaa nguruwe 4.overall ukimpa nafasi zaidi,anakua vizuri zaidi.wenye mimba wanahitaji nafasi zaidi .nakushauri tembelea wafugaji kupata design nzuri.kuna namna nyingi za kujenga banda.pia google search,kuna document nyingi kuhusu hilo
Mashamba gharama huku.wanauza 400,000/eka
Mashamba gharama huku.wanauza 400,000/eka
Nguruwe wangu mdogo miguu ya mbele haina nguvu hawezi kusimama atakua amepata ugonjwa gani au shida nini mkuu..Kama utawalisha inavyotakiwa,hiyo ni pesa ya kutunza nguruwe 20 kwa muda wa mwaka mmoja na nusu toka wazaliwe na wao kuanza kuzaa