Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

Nashukuru sana mkuu. hapo napafahamu vizuri nitakwenda kuwaona mkuu mara nyingi huwa nafika Arusha. Asante!
 
Wadau ningeomba kuwasilisha kwenu ili muweze kunishauri.

Nilikuwa napenda sana ufugaji wa nyuki baada ya kuvutiwa sana na faida ya asali.

Nilikuwa naomba ushauri,mawazo na utaalam wenu wadau juu ya ufugaji wa nyuki ili niweze kuvuna asali nying,nzuri na ya uhakika.
Ningependa kufaham mazingira ambayo nyuki watazalisha asali nyingi


Je, katika ufugaji wa nyuki hali ya hewa huwa ina depend?

Jekuna aina ya nyuki? Na aina ipi ni nzuri kwa ufugaji na huwa inatoa mavuno(asali) mengi?

Ningependa kufaham hayo kwanza au kama kuna mu2 ana kitabu au website yoyote yenye kuweza kunisaidia hata kama atataka nimchangie haina shida nipo tayali.

Msada wenu plz.
 
Salama mkuu kuna kitabu kinaitwa beekeeping in tanzania nadhani kitakupa ufafanuzi wa kutosha hebu kacheki hapo wizarani ofisi za idara ya nyuki wanaweza kukupa ushirikiano wa kutosha
Wadau ningeomba kuwasilisha kwenu ili muweze kunishauri.

Nilikuwa napenda sana ufugaji wa nyuki baada ya kuvutiwa sana na faida ya asali.
Nilikuwa naomba ushauri,mawazo na utaalam wenu wadau juu ya ufugaji wa nyuki ili niweze kuvuna asali nying,nzuri na ya uhakika.
Ningependa kufaham mazingira ambayo nyuki watazalisha asali nying,
je katika ufugaji wa nyuki hali ya hewa huwa ina depend?
Je kuna aina ya nyuki? Na aina ipi ni nzuri kwa ufugaji na huwa inatoa mavuno(asali) mengi?
Ningependa kufaham hayo kwanza au kama kuna mu2 ana kitabu au website yoyote yenye kuweza kunisaidia hata kama atataka nimchangie haina shida nipo tayali.

Msada wenu plz.
 
Mada zinazostahili pongezi siwezi kupita bila kutoa pongezi!!!! Zis iz JF we had and ze JF we want!!! BEE KEEPING,FISH FARMING,POULTRY na nyingine nyingi twazihitaji ili tuendeleze jamii yetu kwa manufaa
 
yes, ukizingatia ubunifu wa packaging nzuri utauza sana, hii ni kuweza kuwa na packs zenye quantities nyingi tofauti, e.g. 125 mls, 250 mls, 350 mls, 500mls, 1 liter, 5 liters, hii itawezwesha kila.mtu kumudu kununua bidhaa yako
 
Hicho kitabu cha Bee keeping in Tanzania wanagawa bure pale wizarani. Kinaonyesha na idadi ya colonies nchi nzima,na maeneo ambayo bado virgin. Ushauri wangu ni huu, fuga nyuki ktk maeneo yasiyo chafuliwa na shughuli za kilimo ili upate asali daraja la kwanza.
 
Malila, mimi nimeanza kuogopa kuwekeza TZ, tusije tukaweka pesa kwenye ufugaji wa nyuki -- Asali ikamiminika toka misitu ya Congo ikawa kama biashara ya mayai.
 
Malila, mimi nimeanza kuogopa kuwekeza TZ, tusije tukaweka pesa kwenye ufugaji wa nyuki -- Asali ikamiminika toka misitu ya Congo ikawa kama biashara ya mayai.

Mkuu usiogope,
Kuna nyuki wa jamii nyingi, wewe fuga nyuki wadogo ambao wanapatikana kwa wingi maeneo ya Chunya, Nkinga na misitu ya Uvinza, pili ukiweza kupata asali yenyewe toka ktk mizinga yako, soko liko pale pale.

Wakati watu wanahangaika kuuza kuku, kuna mzee mmoja pale Msufini/mbezi ametupanga foleni ya kununua kuku kwake, hata mimi niko ktk foleni hiyo mwezi wa pili sasa, kisa yy anauza kitu kilicho bora kabisa.Kwa hiyo na ww fuga nyuki ktk mazingira bora kabisa.
 
LEGE, Mimi si Mtaalamu wa kusomea mambo ya Nyuki lakini nitakushirikisha kile nilichojifunza na kufanyia kazi toka kwa magwiji wa sekta hii kwa takribani miaka isiyopungua mitano.
.. Ningependa kufaham mazingira ambayo nyuki watazalisha asali nyingi. .
Nyuki anategemea maua yenye mchozo na maji yanayopatikana katika mazingira yake ili aweze kutengeneza asali na bidhaa zingine. Mali ghafi hizi lazima zipatikane ndani ya mzingo wa kilometa tatu. Hivyo sua la hali ya hewa na mazingira lina ushawishi katika uzalishaji wa asali. Na nyongeza ya hapo, aina ya maua yanayopatikana katika eneo husika hushawishi rangi na radha ya asali. Mfano asali ipatikanayo Singida toka Itigi Thicket ni amber wakati ile ya Tabora ni black!
Je kuna aina ya nyuki? Na aina ipi ni nzuri kwa ufugaji na huwa inatoa mavuno(asali) mengi?
Nijuavyo kuna makabila mengi ya nyuki. Lakini Tanzania inafuga ukoo wa Apis Mellifera (Nyuki Wakali) na Nyuki wadogo. Apis Mellifera kwa mtazamo na uelewa wangu ndiyo koo linalofugwa zaidi katika nchi zetu za Tropiki. Suala la mavuno mengi rejea jibu langu hapo juu.
Ningependa kufaham hayo kwanza au kama kuna mu2 ana kitabu au website yoyote yenye kuweza kunisaidia hata kama atataka nimchangie haina shida nipo tayali.
Unaweza kuwasiliana na hawa kwa elimu zaidi: Balaza la Asali Tanzania (Tanzania Honey Council)- Unaweza kupata mawasiliano yao hapa Tanzani Honey Expo - 2009 Wizara ya Maliasili, Idara ya Misitu na Nyuki Traceability-T Ltd - Traceability - T Ltd :: Welcome to our website
 
SHUGHULI za ufugaji nyuki wilayani Manyoni Mkoa wa Singida ambao kwa sasa unashika kasi na kuuacha nyuma Mkoa wa Tabora, zilianza kutambulika rasmi mwanzoni mwa miaka ya 1980.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Fortunata Malya, anasema ufugaji huo ni moja kati ya shughuli za kijadi wilayani humo kwa baadhi ya watu.

Malya anaeleza hayo hivi karibuni kwa timu ya waandishi wa habari waliofanya ziara wilayani kwake iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kwa lengo la kujifunza kuhusu shughuli za ufugaji nyuki.
Anasema kasi ya juhudi hizo ilitokana na Mradi wa Uendelezaji Ufugaji Nyuki uliokuwa ukifadhiliwa na Serikali ya Tanzania na Norway kuanzia mwaka 2000 hadi 2006.

“Pamoja na ufadhili kufikia kikomo, misingi iliyoachwa na mradi bado inafanya kazi na shughuli zote zilizokuwa zinafanyika wakati huo bado zinaendelea aidha Shirika la Friedkin Conservation Fund(FCF), SIDO, DADPS na TASAF wamewezesha kuendeleza shughuli kwa kufadhili 22 kuanzia mwaka 2009 hadi 2011,” anasema Malya.

Anataja fursa zilizopo wilayani humo katika kuongeza wingi na ubora wa mazao ya nyuki (Asali na Nta) kuwepo kwa hifadhi ya nyuki ya taifa ya Aghondi yenye ukubwa wa hekta 3,000, hifadhi ya nyuki katika vijiji 59 eneo ambalo lina ukubwa wa hekta 128,187, vichaka pekee vya Itigi (Itigi Thickets) ambavyo havipatikani mahali pengine Afrika na misitu ya miombo (Miombo Woodlands.

Fursa nyingine ni kuwa na Manzuki ya mfano 10 kwenye vijiji 10 vya mfano, vikundi 52 vya ufugaji nyuki katika vijiji 52 vyenye wanachama 733 na mizinga 39,346, kuwa na wataalamu wa jadi wa ufugaji nyuki walio tayari kubadilika endapo wataendelea kupata elimu stahiki, kuwepo kwa wataalamu tisa waliobobea.

Kwa mujibu wa Malya, fursa nyingine ni kuwapo sera, sheria na programu ya taifa ya ufugaji nyuki, viongozi na wataalamu wa ngazi zote wilayani kuhamasika katika kufuga nyuki na kuhimiza ufugaji huo na viongozi wa mkoa na taifa kuhamasika na kuelekeza misaada stahiki kwenye juhudi za maendeleo ya ufugaji nyuki Wilayani kwake.

Hali ya ufugaji nyuki


Anasema mwaka 2005 asali iliyozalishwa ilikuwa kilo 520,115 na nta kilo 9,500; mwaka 2006 kilo 205,160 na nta kilo 11,716 na mwaka 2007 walizalisha kilo 3,700 za asali wakati hawakuzalisha nta hata kilo moja.

Mwaka 2008 uzalishaji wa asali ulipanda na kufikia kilo 1,313,910 na nta kilo 314,875, mwaka 2009 walizalisga kilo 650,500 na nta kilo 85,000, mwaka 2010 kilo 850,000 na nta kilo 85,000 wakati uzalishaji kwa mwaka jana (2011) ulikuwa kilo 985,000 na nta kilo 60,000.
Anasema kwa mwaka jana uzalishaji ulishuka ikilinganishwa na mwaka 2008 ambapo walipata asali nyingi kutokana na kuwepo kwa ukame.

Kwa mujibu wa Malya nyuki hutegemea chakula chake kutoka kwenye maua mwaka jana hali ilikuwa tofauti kutokana na ukame uliokuwepo hali iliyosababisha nyuki kukosa chakula cha kutosha hivyo uzalishaji asali kutokuwa mzuri.

“Uzalishaji hutegemea hali ya hewa itakavyokuwa ikiwa mbaya unashuka,” anasema Malya.
Kwa upande wa nyuki wasiouma(nyuki wadogo) mwaka 2006 walizalisha lita 42, mwaka 2007 lita 69, mwaka 2008 lita 102 mwaka 2009 lita

350, mwaka 2010 lita 445 wakati mwaka jana (2011) uzalishaji ulipanda na kufikia lita 800.
Anasema bei ya asali ya nyuki wakubwa (wanauoma) ni sh 8,000 wakati wasiouma (nyuki) wadogo ni sh 18,000 kwa lita. Bei hiyo hutofautiana kwa kuwa asali ya nyuki wadogo ina faida kubwa ikiwamo kutibu magonjwa mbalimbali kama kikohozi kinachobana kuliko ya wakubwa.

Mizinga ya kiasili, kisasa


Anasema mwaka 2005 walikuwa na mizinga ya kiasili 228,000 na mizinga 917 ya kisasa, mwaka 2006 walikuwa na mizinga ya kiasili 298,000 na ya kisasa 947 huku mwaka 2007 walikuwa na mizinga ya kiasili 300,000 na ya kisasa 1,050.
“Mwaka 2008 kulikuwa na mizinga ya kiasili 350,000 na ya kisasa 1,400, mwaka 2010 ilikuwa 360,020 na ya kisasa 2,108 na mwaka jana

tulikuwa na mizinga ya kiasili 480,000 na ya kisasa 2,208,” anasema Malya.
Kwa upande wa wafugaji nyuki anasema mwaka 2005 walikuwa 12,500, mwaka 2006 walikuwa 14,000, mwaka 2007 walikuwa 17,000, mwaka 2008 idadi yao ilikuwa 22,000, mwaka 2009 na 2010 walikuwa 35,000 wakati mwaka jana (2011) idadi yao iliongzeka na kufikia 48,000.

Anavitaja vikundi vya ufugaji nyuki kuanzia mwaka 2005 hadi 2011 ambavyo idadi yao iko kwenye mabano kuwa ni mwaka 2005 (13), 2006 (35), 2007 (40), 2008 (42), 2009 (45), 2010 (50) na mwaka 2011 vikundi vilikuwa 52.
Sambamba na hilo anasema mwaka 2005 wafugaji/wadau waliopatiwa mafunzo ya mbinu na teknolojia sahihi za ufugaji nyuki ilikuwa 120,

mwaka 2006 walikuwa 250, mwaka 2007 walikuwa 373, mwaka 2008-600, mwaka 2009 walikuwa 780, mwaka 2010 walikuwa 860 na mwaka jana walikuwa 920.
Anasema wilaya hiyo pia imekuwa ikishiriki katika maonyesho mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ya ubora wa asali tangu mwaka 2000 na

kufanikiwa kutunukiwa ushindi wa kwanza mara tatu.
Anaeleza pia sampuli za asali ya Manyoni ziliwahi kutumwa kwenye maabara za kimataifa Ulaya mara tatu na kuthibitishwa kuwa na ubora unaokubalika.

Changamoto


Malya anazitaja changamoto zilizopo kuwa ni kukithiri kwa uharibifu wa mazingira unaochangiwa na kilimo duni, uchomaji, mkaa, upasuaji mbao, wahamiaji na wingi wa mifugo.

Nyingine ni kuwepo dalili za makundi ya nyuki kuvamiwa na kupe wa nyuki, ongezeko la maadui wa nyuki wakiwemo wadudu kama nyegere, buibui, mijusi na nondo wala nta, baadhi ya jamii kuwa wazito katika kuhifadhi mazingira, uwezo mdogo wa wafugaji nyuki katika kutumia sayansi na teknolojia bora ya wafugaji nyuki.

“Uwezo mdogo wa kusambaza huduma za ugani vijijini katika kulikabili suala la msingi la mapinduzi ya ufugaji nyuki hususanisuala la mapinduzi ya viwanda vinaavyojikita kwenye ufugaji nyuki,” anasema Malya.

Changamoto nyingine ni ukosefu wa usafirishaji kwa ajili ya huduma za ugani, wafuga nyuki wengi na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki kutozingatia udhibiti wa ukaguzi thabiti wa ubora wa mazao ya nyuki, wanawake wengi kutofuga nyuki kwa sababu za imani kuwa ufugaji ni kazi

ya wanaume peke yao (kutokana na mazingira magumu ya msituni, umbaki kutoka vijijini na kazi ya kupanda miti wakati wa kutundika mizinga na kurina asali.

Nyingine ni wananchi wengi kutofuga nyuki kwa kuhofia wezi ambao huiba mizinga na asali, wafugaji nyuki kutokuwa na chombo chao (ushirika) cha kusimamia uzalishaji, uhifadhi, uchakataji na soko la mazao ya nyuki wakati changamoto nyingine ni mabadiliko ya tabia nchi.
Anasema changamoto hizo zinasababisha kupungua kwa kizazi cha nyuki, ubora na wingi wa mazao ya nyuki na uchangiaji mdogo kwenye uchumi wa wafugaji nyuki na wananchi wa Manyoni kwa ujumla.

Malengo ya halmashauri


Malya anayataja malengo ya halmashauri kuwa ni kuendeleza a rasilimali ya nyuki kwa misingi endelevu na kuongeza mchango wa wafugaji nyuki katika kukuza pato la mwananchi na viashiria ni kuwepo vikundi vya mfano 20 (wafugaji nyuki 600) wanaotekeleza ufugaji nyuki kwa

misingi endelevu ifikapo mwaka 2015, kutokuwepo kwa nyuki wanaouawa wakati wa kurina asali ifikapo mwaka 2015.
Viashiria vingine ni kuongezeka kwa uzalishaji na ubora wa asali kutoka kilo 15 za asali hadi kilo 60 kwenye kila mzinga wa kisasa ifikapo

mwaka 2015, kuwepo kwa hifadhi za nyuki 20 katika vijiji vya mfano 20, kuwepo kwa misingi endelevu ya Hifadhi ya Nyuki ya Taifa Aghondi na kuongezeka kwa idadi ya wahamasihaji.

Malengo mahsusi ni kukamilika kwa matumizi ya mbinu na teknolojia sahihi za ufugaji nyuki ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya mavazi ya kinga ya nyuki, mizinga ya kisasa ili kuwavutia wafugaji wa nyuki wengi zaidi wakati huo kuendeleza ufugaji nyuki kwa misingi endelevu.

Anasema viashiria vyake ni mbinu za teknolojia sahihi za ufugaji nyuki zitazoendelezwa katika vijiji 20 ifikapo mwaka 2013 pia wafugaji nyuki 600 wanaume, wanawake na vijana watakuwa wamepatiwa mafunzo na kushiriki katika shughuli za ufugaji nyuki kwa kutumia mbinu na teknolojia sahihi ifikapo mwaka 2013.

Lengo jingine ni kuimarishwa kwa huduma za ugani (utoaji ushauri wa kitaalamu kwa misingi endelevu) na viashiria vyake ni kwamba vikundi 20 vitakuwa na vifaa vya mfano vya kinga ya nyuki, mizinga ya kisasa, vifaa vya kuvunia, kuhifadhia na kufungashia asali ifikapo Juni 2013, kutokuwepo kwa matukio ya moto msituni ifikapo mwaka 2015, ongezeko la uzalishaji wa asali bora kufikia kilo 60 kwa mzinga ifikapo mwaka 2015.

Viashiria vingine ni ongezeko la wafugaji nyuki kutoka 60 hadi 1,200 kupitia TOTs katika vijiji 20 ifikapo mwaka 2015, kutokuwepo kwa vifo vya nyuki wakati wa urinaji ifikapo mwaka 2015 na kuwapo kwa ushirika wa wafugaji nyuki wilaya (APEX) ifikapo mwaka 2015.
Lengo jingine ni kuimarishwa kituo cha kukusanyia na kuuzia mazao ya nyuki cha ushirika wa wafugajii nyuki na viashiria ni kuongezeka kwa

biashara ya maao ya nyuki ifikapo mwaka 2015, kuboreka kwa mazao ya nyuki kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyo sasa na kuwapo kwa mfumo wa ukusanyaji takwimu muhimu za ufugaji nyuki ifikapo mwaka 2015.
Anayataja masharti yatakayofanikisha malengo kuwa ni kupatikana kwa rasilimali za kutosha (fedha, vitendea kazi, rasilimali watu) kwa wakati mwafaka.

Mengine ni kuwepo sheria ndogo za ufugaji nyuki za Halmashauri ya wilaya ya Manyoni na kuzitekeleza kwa dhati, wahusika wengine kukubali kuiga na kushiriki shughuli za kuimarisha ufugaji bora wa nyuki, wataalamu wa nyuki, kushikamana na kushirikiana kwa dhati pamoja na kuwezeshwa ipasavyo kufanya kazi za ugani kwa uadilifu mkubwa.

Masharti mengine ni viongozi wa ngazi zote kuunga mkono juhudi za wataalamu na wafugaji nyuki, watakaopatiwa mafunzo kupangiwa maeneo na kuwajibika kusambaza utaalamu na wataalamu wa fani nyingine.

Naye Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Ufugaji Nyuki nchini kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba anasema lengo la ziara hiyo ni kuwawezesha waandishi wa habari kujifunza kuhusu shughuli za ufugaji nyuki na kuzitangaza kwa umma.
Anasema kwa sasa Manyoni imekuwa mstari wa mbele katika uzalishaji asali hivyo serikali imeona ni vema kuendeleza shughuli za ufugaji nyuki.

“Hivi sasa tunataka kuendeleza shughuli za ufugaji nyuki kwa kasi kwani naamini itaondoa umaskini kwa watu wetu, Wilaya ya Manyoni ni mfano wa kuigwa kwa sasa katika uzalishaji asali nchini,” anasema.

Anasema serikali imedhamiria kuwasaidia wafugaji nyuki kwa kuwapatia nyenzo na vitendea kazi vingine ikiwamo mizinga kwa ajili ya kufanikisha shughuli zao.
Mkamba anasema tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa Mkoa wa Singida kuona namna watakavyowapatia mizinga 500 ya kisasa ili kuwanufaisha wafugaji.
Anatoa rai kwa wananchi kujikita zaidi katika shughuli hizo zitakazowasaidia kuwaletea maendeleo.
Ufugaji nyuki wawanufaisha Manyoni
 
thanx mganga wa kienyeji.. nilikuwa natafuta sana taarifa hizi za ufugaji wa nyuki kutoka kwa mfugaji. Nimepata pakuanzia
 
sitaki kufuga kienyeji, huoni avatar?
Nakuona mkuu wewe ni CCM Damu Hongera na CCM yako ila CCM imeshakuwa Nzee CCM aliyoiacha Baba waTaifa Mwalim Nyerere na CCM hii iliyopo madarakani ni tofauti kabisa CCM imepitwa na wakati samahani kama nitakuudhi asante mkuu.
 
Nakuona mkuu wewe ni CCM Damu Hongera na CCM yako ila CCM imeshakuwa Nzee CCM aliyoiacha Baba waTaifa Mwalim Nyerere na CCM hii iliyopo madarakani ni tofauti kabisa CCM imepitwa na wakati samahani kama nitakuudhi asante mkuu.

MziziMkavu

mbona umeingiza siasa tena huku kwenye ujasiriamali ..... ha haa haaaa
 
This is an area of interest...tukipata mashamba ya kufugia definetely that is the easiest thing to do. Hakuna kuchimbua visiki wala kupalilia. Ni kufuga nyuki na wezi wakiwasogelea wanachukua kubwa kwahiyo biashara inakuwa safe.
 
This is an area of interest...tukipata mashamba ya kufugia definetely that is the easiest thing to do. Hakuna kuchimbua visiki wala kupalilia. Ni kufuga nyuki na wezi wakiwasogelea wanachukua kubwa kwahiyo biashara inakuwa safe.

Njoo tuanzishe shamba letu mkuu.
 
Kwa JF wote,
Fikiria vijana wetu wanamaliza shule au vyuo hawana kazi.Tafiti niliyo fanya kwa undani kuna kazi moja ukifanya una uhakika kufanikiwa bila wasiwasi.Fikiria kiwanda unachoanzisha hakiitaji mtaji mkubwa , malighafi bure , wafanyakzai bure, huna haja ya umeme. Kiwanda cha namna hii kinawezekana Tanzania pia kwa kuhusisha watu wengi. Wajua ni nini? Ebu nikujuze kuanzia sasa jishughulishe na ufugaji wa nyuki ukaone maajabu siyo kupoteza muda unasubiri kazi ingia kwenye nyuki akutengenezee pesa.Ukifuga nyuki unakuwa na uhakika wa kupata asali na pesa
.

Watanzania tusilale kumbuka wenzetu usukumani walichezea dhahabu sasa wanalia wawekezaji wamekuja hawana bao, angali kanda ya ziwa sangara wanalia mnasubiri nini kuanzisha ufugaji wa nyuki kibiashara. Kama hatuwezi subiri Wachina waje wakianza kufuga nyuki waswahili tutaanza kulalama.

Ebu tuamuke , tufuge nyuki asali ni mali asali ni dawa kama hujui ingia tu kwenye mtandao uliza bee au honey au beekeeping ukaone maajabu ya nyuki.
Asali na dhahabu hakuna tofauti. Wenzetu wanaita asali liquid gold.
Watanzania tuhamuke tufuge nyuki achana na biashara ya pikipiki na bajaj ingia misituni , mashambani weka mizinga utakuwa tajiri mara moja ujumbe ndio huu msipo fanya wachina wako mlangoni watafanya.
Changamka wakati ni huu wana JF kula ASALI KWA AFYA usingoje kwenda kwa BABU
 
wadau ni kwa namna gani unaweza wekeza kwny mradi wa ufugaji nyuki kisha upate milioni kumi 10 kwa mwaka?soko kubwa la asali ni wapi ndani na nje ya nchi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom