misorgenes
JF-Expert Member
- Oct 7, 2010
- 206
- 50
Anayejua elimu/ujuzi wa ufugaji wa Nyuki, Mizinga bora,ulinaji asali na soko la asali atupe elimu. Natamani kufanya biashara hii.
===========
===========
Ericus Kimasha
..1. Naomba ufafanuzi nasikia kuna asali nzito na nyepesi, pia asali ya nyuki wadogo na asali ya nyuki wakubwa. Kuna Asali ya aina gani na ipi?
Ni kweli ziko asali nzito na nyepesi, amber, nyeupe na nyeusi. Uzito au rangi za asali kwa kiwango kikubwa huchangiwa na aina ya maua ambayo nyuki huchukua mchozo wa kutengenezea asali. Mfano asali ya maeneo mengi ya Tabora ni nyeusi wakati ile ya Singida maeneo ya Sanjaranda na Itigi ni amber ilhali ile ya Dodoma ni nyeupe na ina machicha kama barafu.
Aina ya nyuki wanaofungwa zaidi katika maeneo ya Kitropiki na Tanzania ikiwemo ni Apis Mellifera mbao tuliowengi tunawafahamu kama nyuki wakubwa. Hawa nyuki ni wakali na wana mwiba unaotumika kujihami. Tofauti na nyuki wadogo ambao ni wapole na asali yake inatumika zaidi kama dawa
Ufugaji wa Nyuki ni kazi ya kudumu lakini uvunaji wa mazao ya nyuki hufanyika kwa misimu. Iko mikoa nchini mwetu ambayo huwa na misimu miwili kwa mwaka; Msimu mdogo na msimu mkubwa. Maranyingi asali inayopatikana katika msimu mdogo huwa ni ya masega ambayo hayajakomaa. Ninaweza kukushauri kwenye hili pale utakapo kuwa umeisha amua wapi utaweka mizinga. La muhimu ni kujua msimu wa maua unaanza lini. Hii itakusaidia kupata nyuki-wakaaji hii itakuhakikishia masega kujenjwa katika muda mfupi...2. Je, ufugaji wa nyuki una msimu? Miezi ipi basi ni mizuri kwa Ufugaji wa Nyuki?
Watanzania wengi wanapenda asali ya amber. Ili kisayansi asali ya Dark-Blue ina virutubisho vingi zaidi. Mkoa wa Kigoma unaibuka kama chanzo cha asali nzuri na bora. Ninaposema bora namaanisha ulinaji unaozingatia kanuni bora, ukamuaji unaojali usafi na upakiaji katika vifaa safi na bila kuongeza kitu chochote (adulteration)..3. Asali nzuri inayopendwa sana ni ya mkoa gani?
Iko mizinga ya aina mbalimbali na hivyo bei tofauti tofauti. Kwa maelezo ya kina nitumie email ekimasha@jamiiforums.com..4. Utengenezaji wa mizinga unakuwaje, ukubwa wa mizinga au dimensions ipi ni kikomo au ipi ni safi? gharama za kutengeneza mzinga ni ipi?
Aina ya mzinga inaushawishi katika ubora na kiwango cha asali inayopatikana. Majibu zaidi ya swali hili nitayaandaa au nitakupatia vitabu vyenye vipimo ambavyo vitakupanua uelewa kwenye suala hili...5. Utoaji wa asali unakuwaje lita ngapi kwa dimension ipi ya mzinga?
Miti na maua yanayotoa mchozo ni muhimu sana. Lakini pia chanzo cha maji lazima kipatikane katika eneo la mzingo usiozidi ekari tano..6. Mahitaji muhimu kwa ufugaji wa nyuki / kinachovuta nyuki ni kipi?
Sikumbuki vizuri. Nitauliza..7. Asali inaiva inakomaa baada ya muda gani?
Soko la Jumla litakulipa lakini si vizuri sana kama kupaki kwenye chupa na kusambaza katika Min and Supermarkets. Pia unaweza kufanya direct home delivery. Soko la Jumla liko kwa wapakiaji wa Dar (Honey Packers) ambao wengine hufuata moja kwa moja kutoka huko mikoani...8. Soko la Asali kwa bei ya jumla lipo wapi hapa dar?
Mimi ni muumini wa soko la ndani. Hii inatokana na ugumu na vikwazo vingi vilivyoko katika soko la nje na mwisho wa siku profit-margin ni ndogo sana. Soko la ndani ni kubwa mno ndo maana bado supermarkets zetu zimejazwa na asali kutoka Brazil, india na China...9. Je soko la nje la asali lipo wapi sana? Usafirishaji wa Asali nje ya nchi unakuwaje?