Ufisadi Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,351
Zaidi ya Shilingi Bilioni 35.7 zikiwemo fedha za matumizi ya ofisi shilingi bilioni 5.7 na maendeleo Bilioni 30 zimetolewa hazina na kuingizwa kwenye tume hewa ya ushirika kwa kutumia voti namba 24 katika kipindi cha mwaka 2010/2011 kupitia wizara Ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Source: ITV Tanzania.
 
tumepiga kelele za ufisadi! CCM na magamba yake wameweka pamba masikioni.2015 tujitahidi kuondoa uvundo.
 
Zaidi ya Shilingi Bilioni
35.7 zikiwemo fedha za matumizi ya ofisi shilingi bilioni 5.7 na
maendeleo Bilioni 30 zimetolewa hazina na kuingizwa kwenye tume hewa ya
ushirika kwa kutumia voti namba 24 katika kipindi cha mwaka 2010/2011
kupitia wizara Ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Source: ITV Tanzania.
Unashangaa njoo IDARA YA MAHAKAMA,uone jinsi pesa zinavyotafunwa,chief accountant ana mtandao wa kufiilisi mahakama,anahonga HAZINA asihamishwe
 
Mi nashindwa kuelewa nchi hii inakwenda wapi? Ma afisa ushirika huko wilayani wanafanya kazi ktk mazingira magumu sana hata usafiri wakwenda kutekelea majukumu yao halmashari zinadai hakuna fungu na hii imechangia vyama vya ushirika vingi vife , hivi leo tunaposikia kuna fungu lilipitishwa kupitia hiyo vote,nashindwa kupata jibu kama kweli hawa viongozi wetu wana nia njema na wananchi wake
 
Nimechoka kushanagaa!..sasa hivi imeshakuwa ni jambo la kawaida tu watu kuhujumu pesa za walipakodi, na hakuna anayejali kwani kila kukicha utasikia mara kuna mabilioni uswiss, mara rada yetu mpya imeharibika, mara utasikia kodi zetu zinampeleka mwenyenyumba kubembea jamaica, wakati mwingine kaenda kula tende. Haya yote yanaanza kuzoeleka masikioni mwetu.
Mytake: Tuongeze elimu ya uraia kwa wananchi wetu ili tuhakikishe 2015 wapigakura wanajitokeza na kupiga kura makini.
Mungu ibariki Tanzania
 
ndio nchi yetu hii, watanzania tumefika mahali pabaya yaani kuona ufisadi na wizi wa pesa ya umma kama sehemu ya maisha yetu?? Maskini Tanzania where are you heading to??
 
Back
Top Bottom