Ufisadi Wizara ya Ardhi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Maofisa Wizara ya Ardhi wajizolea viwanja kibao
Shadrack Sagati
Daily News; Wednesday,February 18, 2009 @19:23

Wakati idadi kubwa ya wananchi Dar es Salaam walikosa viwanja vilivyogawiwa na serikali katika mradi wa viwanja 20,000, imegundulika kuwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wamejimilikisha viwanja vingi katika mpango huo.

Gazeti hili limebaini kuwa watumishi hao wanamiliki viwanja kati ya 10 na 13, ambavyo walijimegea wakati wa kutekeleza mradi huo ambao umetekelezwa katika manispaa tatu za Mkoa wa Dar es Salaam.

HabariLeo imebaini kuwapo idadi kubwa ya watumishi ambao wanamiliki viwanja kati ya viwili hadi 10 katika maeneo ya mradi; hivyo kuwafanya watumishi wa wizara hiyo kuwa wamiliki wa viwanja vingi vilivyopimwa kuliko wananchi wengine.

Gazeti hili lina baadhi ya majina ya watumishi ambao wamejilimbikizia viwanja hivyo bila kuviendeleza katika maeneo mbalimbali. Viwanja vilivyopimwa wilaya ya Temeke viko katika maeneo ya Tuangoma, Kisota, Mtoni Kijichi, Mwongozo na Gezaulole na Kibada.

Viwanja vilivyopimwa wilaya ya Kinondoni katika mradi huo ni Mivumoni, Mbweni kuelekea Mto Mpiji, Mbweni JKT na Bunju, wakati wilaya ya Ilala ni katika maeneo ya Buyuni na Mwanagati. Idara ya Kodi ya wizara hiyo imeyaweka wazi majina ya watumishi wanaotakiwa kulipia viwanja hivyo walivyovinunua katika mpango wa mradi wa kupima viwanja.

Orodha hiyo inaonyesha majina ya watumishi na viwanja wanavyomiliki katika maeneo mbalimbali ya mradi. Mpango wa kupima viwanja 20,000 katika Jiji la Dar es Salaam ulibuniwa na Serikali katika mwaka wa fedha 2002/2003. Mradi huo ulikuwa unatekelezwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na halmashauri zake.

Wakati wa kugawiwa viwanja hivyo, wananchi wengi ambao walihitaji viwanja hivyo walivikosa, hali iliyozusha malalamiko ya kuwapo uwezekano wa kutumika kwa ‘mchezo mchafu’ wakati wa utekelezaji wa kugawa.

Kujilimbikizia viwanja hivyo ambako kumegundulika ndani ya Wizara ya Ardhi, kunadhihirisha malalamiko ya wananchi wengi kuwa ndani ya wizara hiyo kuna ufisadi mkubwa unaofanywa na watumishi hao wa umma.

Waziri wa Wizara hiyo, John Chiligati, alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema: “Hata mimi nilishangaa kukuta watumishi wanamiliki idadi kubwa ya viwanja namna hiyo … niliulizia na kufuatilia suala hilo, wakaniambia kuwa viwanja hivyo vilikuwa vinanunuliwa na watu wote wenye uwezo.

“Wameniambia vilikuwa vinauzwa kama nguo dukani, hivyo mwenye uwezo alikuwa na haki ya kununua kiasi chochote cha viwanja anavyotaka … ndivyo nilivyoelezwa,” alisema Chiligati. Alipoulizwa hatua ambazo wizara inaweza kuchukua, Waziri alisema: “Kila jambo lina wakati wake, kwani wakati viwanja hivyo vinagawiwa mimi sikuwa waziri katika wizara hii; hivyo ni vigumu kwangu kwa sasa kuanza kuwahukumu watumishi hawa kwa namna walivyovipata.”

Chiligati alikabidhiwa wizara hiyo mwaka mmoja uliopita na kumrithi John Magufuli aliyeongoza wizara hiyo mwaka 2006, mara baada ya uchaguzi mkuu ulioiweka madarakani Serikali ya Awamu ya Nne. Hata hivyo, Waziri alisema matarajio ya serikali ni kwa watu ambao wamenunua viwanja hivyo kuhakikisha wanaviendeleza na akaonya kuwa mtumishi ambaye amenunua kiwanja kwa nia ya kukilangua, atakiona cha moto.

“Kama kuna mwananchi yeyote ambaye anamfahamu mtumishi wa wizara hii ambaye amenunua viwanja hivyo; lakini akaviuza tena kwa bei ya kulangua, ni vyema aniletee jina lake nami naahidi kushughulika naye,” alisema Chiligati. Alisema kitendo cha kulangua viwanja hivyo ni sawa na mtumishi kutumia vibaya madaraka yake. “Huyo ametumia cheo chake kupata kiwanja na kumuuzia mwananchi kwa bei ya juu, hilo halikubaliki.”

Serikali ilitekeleza mradi huo mkubwa wa Kupima Viwanja 20,000 na uligharimu Sh bilioni 8.9. Serikali ilitarajia kukusanya Sh bilioni 26 kutokana na mauzo ya viwanja 30,655 vilivyopimwa katika maeneo hayo. Fedha hizo ambazo ni mkopo wa shughuli zote za mradi zilitumika kwa uthamini, ulipaji wa fidia ya mali za wananchi ndani ya maeneo ya mradi, fidia ya thamani ya ardhi, uandaaji wa michoro na mipango miji, upimaji wa viwanja na uwekaji wa miundombinu, kwa mfano, barabara.

Wizara hiyo ni lazima irejeshe fedha hizo kwa utaratibu wa kuchangia gharama kwa wale ambao walipewa viwanja hivyo. Viwango vilivyokuwa vikitozwa kwa viwanja vilivyopimwa chini ya mradi huu gharama ya chini ilikuwa Sh 500,000. Serikali ilitangaza kuwa azma kubwa ya kupima viwanja hivyo ilikuwa kumaliza uhaba wa makazi. Ili kutekeleza azma hiyo, viwanja vilivyopimwa viligawiwa kwa watu wenye uwezo na sifa zinazotakiwa ili waweze kujenga. Malengo mengine ya mradi huo, yalikuwa ni kupunguza matatizo yanayotokana na ujenzi holela na hasa katika maeneo hatari kama vile mabondeni. Serikali inaamini kuwa viwanja hivyo vikiendelezwa, vitapunguza msongamano wa watu katikati ya Jiji, kwa kuwa huduma zote zimeelekezwa kwenye maeneo ya mradi na ujenzi holela katika maeneo yasiyopimwa utapungua.
 
Tanzania ni kubwa inafaa mtu apewe kiwanja size ya nusu ya uwanja wa Mpira. ili ajiwezeshe kulimalima mboga.
Ila iwepo na sheria ya kujenga ndani ya miezi sita nyumba iwe imeshaelekea na ndani ya mwaka mmoja na nusu iwe imeshamalizwa ,kama hakuna kilichofanyika panataifishwa na kupewa mtu mwengine ,halafu tuone huo ujemedari wa kujikusanyia viwanja kumi.
 
Hawa ni mboko tu...tena mbele ya wake zao!!

sasa DC Bukoba yuko wapi?

Sheria gani..wakati no responsibility?

Wapelekwe mahakamani ila baada ya mboko kwanza...iwe funzo wengine wasirudie!
 
Hivi hali kama hii itakwisha lini? Nakumbuka kuna thread moja huku ilikuwa inazungumzia bei za properties hapa nchini ni absurd. Hawa ndio wanasababisha bei za viwanja zinakuwa kubwa. Just imagine wanafanya monoply kubwa kiasi hicho, then wanaanza kuuza kwa bei wanayotaka wao. Ni mbaya sana kwa sisi wenye kipato cha chini.
 
Tanzania ni kubwa inafaa mtu apewe kiwanja size ya nusu ya uwanja wa Mpira. ili ajiwezeshe kulimalima mboga.
Ila iwepo na sheria ya kujenga ndani ya miezi sita nyumba iwe imeshaelekea na ndani ya mwaka mmoja na nusu iwe imeshamalizwa ,kama hakuna kilichofanyika panataifishwa na kupewa mtu mwengine ,halafu tuone huo ujemedari wa kujikusanyia viwanja kumi.

Mkuu wazo lako ni zuri lakini linaweza lisileate 'equity' katika jamii (sorry nimekosa neno lakiswahili la 'equity'). Huo muda unaweza kuwa ni mdogo sana kwa mtandaznia wakawaida kuwa amemaliza ujenzi hasa ujenzi wa kisasa. Na kigezo hicho kinaweza sababisha wajanja na wenyenazo wakanunua viwanja vingi tena kwa bei ndogo na kujenga majengo/nyumba za kupangisha au biashara nyingine na kuibua ukabaila ''land monopoly''

Hata hivyo kitendo cha watumishi kujimegea viwanja vingi sii jambo zuri wangeruhusiwa kumiliki mpaka viwanja 2 tu.
 
Waungwana heshima mbele!mimi naomba nitoe ushuhuda wangu kuhusu hawa jamaa wa Ardhi.Nilikuwa nahitaji sana kiwanja kilichopimwa,nikatwanga mguu hadi ardhi nikakutana na waheshimiwa pale wakadai viwanja vya mradi kwa sasa vimeisha ila kuna watu walinunua mwanzoni sasa wanataka kuuza.Jamaa wakanichukua hadi eneo la Kibada kigamboni,kufika lol sikuweza kuamini macho yangu manake ni mapori tu jamaa wana bonge la ramani wanakuonyeshea,ukipenda ndio mnaingia kwenye Price.Kwa kweli nilipenda viwanja viwili kuulizia bei lol kasheshe,jamaa wanataka milion 9 kila kimoja.

Vile viwanja vya Kibada wala havijaisha wala nini ila ni njia ya jamaa wa ardhi ya kujipatia fedha,ukitaka kiwanja wanazunguka wanakinunua kwa shs 500,000 wanakubamiza kwa milion 9.Kweli bongo balaa!!!!
 
Back
Top Bottom