Ufisadi wanyemelea misaada ya waathirika wa milipuko ya mabomu Dar

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,900
21,990
Ufisadi wanyemelea misaada ya waathirika wa milipuko ya mabomu Dar
broken-heart.jpg
Na Jackson Odoyo

Maafa yaliyosababishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea kwenye kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), kambi ya Mbagala sasa yanatumiwa kama mradi wa kujiingizia fedha kutokana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo pamoja viongozi wa serikali za mitaa kubuni njia za kujinufaisha na fidia inayotarajiwa kutolewa na serikali kwa walioathirika.

Serikali imeshatangaza kuwa itawafidia wote walioathirika na milipuko ya mabomu hayo yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye ghala la silaha la kambi hiyo na kulipuka Jumatano iliyopita likichukua maisha ya wanajeshi na wakazi wanaoishi kwenye makazi yanayozunguka kambi hiyo.

Tayari manispaa ya Temeke inagawa misaada ya dharura ya vyakula, vyandarua, sabuni, maji na mahema kwa watu ambao makazi yao yalipobomolewa na mabomu hayo, lakini ugumu wa zoezi hilo unaonekana kuzidishwa na ujanja wa watu wachache wanaotaka kujinufaisha na misaada hiyo huku baadhi wakisingizia kuharibiwa nyumba zao ili waingizwe kwenye orodha ya watakaolipwa fidia.

“Tumeanza kupata kesi mbalimbali ambazo zinahusishwa na milipuko ya mabomu, lakini tukifanya uchunguzi wa kina tunabaini kuwa ni ujanja ujanja tu wa baadhi ya watu ili waunganishwe katika orodha ya watu wanaotarajia kulipwa fidia,” alisema mkuu wa wilaya ya Temeke, Said Mkumbo alipoongea na Mwananchi jana.

"Wameanza kubuni njama mbalimbali za kunufaika na misaada hiyo wakati wao si walengwa.

“Moja ya kesi hizo ni tukio la watu wawili tofauti waliokwenda katika Hospitali ya Manispaa ya Temeke wakidai kuwa vifo vya ndugu zao vilitokana na tukio la mabomu.

"Watu hao walidai kuwa baada ya jamaa zao kuumia wakati wa mlipuko wa mabomu, walipelekwa hospitali ya Temeke kwa matibabu na baadaye wakahamishiwa (Hospitali ya Taifa ya) Muhimbili kwa kwa matibabu zaidi lakini wakafa huko," aliongeza Mkumbo na kuendelea:

“Baada ya ofisi yangu kupata taarifa hiyo nilimwagiza mganga mkuu wa wilaya kufuatilia suala hilo ikiwa pamoja na kuwataka watu hao wapeleke taarifa kamili kutoka Muhimbili lakini, walipoondoka hawakurudi tena.”

Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke, Sylvia Mamkwe alikiri kupata taarifa kama hiyo, lakini akasema maelezo yao ya ndugu wa marehemu hao yalipishana na maelezo ya mganga wa wa zamu aliyempokea mgonjwa mmoja kati yao.

Tukio jingine, kwa mujibu wa mkuu huyo, ni la kijana mmoja Julius Avelini, 30, anadaiwa kwenda ofisi za Kata ya Mbagala Kuu na kumweleza DC kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na baada ya kutibiwa Muhimbili, alipata nafuu lakini tangu tukio la mabomu litokee hali yake imekuwa mbaya.

DC Avelini alisema kijana huyo alidai hata dawa alizokuwa akitumia, sasa hazimsaidii na kuomba serikali imsaidie.

Hata hivyo Mkumbo alisema aliamua kumpigia mganga mkuu wa Hospitali ya Temeke, Aisha Mahita kumtaka ampokee mgonjwa huyo kwa matibabu zaidi.

“Mganga wa zamu anasema kuwa tatizo la mgonjwa halikutokana na tukio la mlipuko wa mabomu ingawa alifikishwa hapo siku ya tukio," alisema mganga mkuu wa Temeke, Mamkwe.

"Tumeamua kurudisha suala hili Muhimbili kwa ajili uchunguzi wa kina kabla ya taarifa hizo kukabidhiwa kwa ngudu zao.”

Katika hatua nyingine mmoja wa maafisa wanaoendesha zoezi la uhakiki wa waathirika wa mabomu, alisema jana kuwa zoezi hilo ni gumu kwa sababu baadhi ya watu wameanza kushirikiana na viongozi wa serikali za mtaa kutoa taarifa za uongo.

“Wengine wanaandikisha majina kuwa nyumba zao zimeathirika na wanahitaji misaada, lakini tukifika katika nyumba hizo hatuoni mahali palipoharibiwa na bomu badala yake tunachobaini ni uharibu wa makusudi na wengine wanatuonyesha mpasuko wa siku nyingi,” alisema afisa huyo kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini.

Naye John Bwana, ofisa maendeleo ya jamii na mwenyekiti wa kamati inayosimamia ugawaji misaada, alisema suala la unganyifu katika zoezi hilo ni kubwa hasa katika upande wa misaada ya vyakula na mahema.

“Baadhi ya watu wanatoa taarifa za uongo ili wapate misaada lakini ukifuatilia unakuta wanaohitaji misaada hiyo ni wachache kuliko idadi ya watu wanohitaji misaada," alisema.

"Hata hivyo baada ya uongo huo kubainika tumeamua kuandaa utarabu upya utakowawezesha waathirika halisi kupata misaada hiyo.”

Bwana alisema baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa pia sio waaminifu kwa sababu wanatuwapelekea idadi kubwa ya watu wanaohitaji misaada kuliko idadi ya watu walioathirika.

Unganyifu mwingine uliobainika katika zoezi hilo ni baadhi ya waathirika kuandika majina wawili ama matatu ili wapate misaada mingi ya vyakula na wengine wanaandikisha watu zaidi ya wawili kwenye nyumba moja.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanalalamikia utaratibu wa kufanya tathimini na ugawaji wa misaada mbalimbali.

“Huu utaratibu wa kugawa misaada unavyofanywa na hii tume hii, haturidhiki nao. Mimi nadhani hili zoezi lingeendeshwa na askari wenyewe au watu wa msalaba mwekundu kila mtu angepata haki yake bila matatizo yeyote,” alisema Rashidi Ali, 35, ambaye ni fundi ujenzi.

Pia wakazi hao walilalamikia utaratibu mbovu wa tathimini ya athari kwenye nyumba zao, utaratibu ambao walisema huwalazimu kushinda nyumbani siku nzima wakisubiri maafisa wanaofanya zoezi hilo bila mafanikio, hali ambayo walisema inahatarisha vibarua vyao. Milipuko hiyo ilitokea Aprili 29 mwaka huu kwenye kambi hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania, kikosi cha 671 na kusababisha vifo vya watu 24 kati yao raia 19, na watu 306 kujeruhiwa huku kaya 907 zikibaki bila makazi.
 
huyo kijana ana pointi ya kimsingi kabisa na inabidi asikilizwe na kusaidiwa kwa hali na mali na serikali!!!
 
Kila kitu sasa ufisadi,hata milipuko ya mabomu hayo ni ufisadi,Mkuu wa JWTZ na Waziri wa Ulinzi hadi sasa wanasubiri nini wasijiuzulu kwa kuteketea kwa Raia wengi kiasi hicho na ambapo hata idadi kamili imefichwa.
 
Back
Top Bottom