Ufisadi wa Rada usijadiliwe ni upuuzi mtupu.

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Watanzania wamechoka kusikia habari za rushwa iliyotolewa katika ununuzi wa rada ya nchi. Suala hili limejadiliwa Bungeni zaidi ya miaka 4 sasa bila kuona wahusika wanachukuliwa hatua badala yake Serikali imekuwa ikipoza machungu ya rushwa hiyo kwa kuipachika majina ya kupotezea kama "chenji ya rada" wengine wameibatiza na kuiita "ni vijisenti" .

Wabunge wamekuwa wakitumia pesa za nchi kulijadili suala hili pasipo ukomo miaka yote.

OMBI:Kama wahusika wa ufisadi huu imeshindikana kuwachukulia hatua basi wabunge fungeni midomo yenu tumechoka kusikia makelele yanayodhihaki wananchi huku mafisadi wanaendelea kutamba mitaani. Pangeni ziara muende kutembea nje ya nchi na starehe zote za dunia, tukutane majimboni uchaguzi ujao 2012.
 
Ndugu utaumia bure, wanaotakiwa kushitakiwa ndio hao hao walio na madaraka sasa na hata bungeni wamo zaidi ya 85% ya watuhumiwa, na nchi hii hatuna sera hiyo itakuwa ni kama kuvunja katiba kuwashitaki kwa vile walishazoe kula bila kuulizwa. I submit, thanks.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom