Elections 2010 Ufisadi wa kutisha ikulu - Kikwete atumia bilion 29 kukarabati ikulu

Kuna gharama sana kuweka maintainance ya mambo kama haya!

DSC09816.JPG

Mkuu huyu ni nani?
 
kwa mujibu wa CAG (kupitia kwa mbunge wa moshi mjini Ndesamburo), serikali ya Kikwete imetumia bilioni 29 (nimesema bilioni yenye B) kukarabati ikulu.

Kumbuka kuwa ikulu ilikarabatiwa kwa bilioni 4+ miaka ya mwisho ya utawala wa Mwinyi, Mkapa alitumia karibu bilioni 10 kuikarabati.

Kikwete katumia bilioni 29 kwenye miaka yake mitano ya kwanza. Hizi bilioni 29 zilinunua nini?
.

Kiasi cha fedha hicho sio cha kutisha kukarabati makazi namba moja ya Taifa (Ikulu), CAG alitakiwa kueleza aina ya matumizi ndio hoja hii ingeweza kujadiliwa kwa marefu na mapana, hivi ilivyo ni kama inaelea hewani. Tangu, awamu ya Rais Mwinyi na Rais Mkapa ni miaka kadhaa imepita sio rahisi kulinganisha na hasa tukichulia kwamba kwa sasa mfumuko wa bei (inflation rate) uko juu na hata nguvu ya dola dhidi ya shilingi ni tofauti hivyo gharama zitakuwa juu. Kwa mfano, kama tunakumbuka Nyumba aliyokuwa anaishi Mkapa iliungua hivyo ilihitaji ukarabati au ujenzi mpya, yote haya hatujui kama yamo katika gharama hizo za CAG au la.
 
NAOMBA FAHAMISHWA...KUNA BINTI/MAMA ANATOKEA KWENYE PICHA NYINGI NI NANI HUYU......WOZOZA POST NAMBA 13 PIA KAMUWEKA nataka jua ili niijuvye akili yangu
 
Tusubiri ccm wakanushe kwani kwa kutumia akili ya kawaida tu.................kipindi cha mkapa zilitumika tsh.9bilion kukarabati ilkulu kwa hiyo ilitakiwa japo isubiriwe miaka mingine kama kumi hivi ili kukarabati tena.......ajabu haka kabwana mdogo kanatumia 29bilion....kukarabati nini tena????????
Kweli kuna kiongozi wa nchi hapo????
Kikwete anaombea tu achaguliwe atimize kiu ya kislamu ya kuwaanzishia mahakama ya kadhi ambayo italeta vita.....

Naona unachanganya madawa, Mahakama ya kadhi inaingiaje kwenye mada hii????? madai ya Makahakama ya kadhi haikuanza wakati wa awamu ya nne, madai haya yalikuwepo enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Kikwete ameyakuta anaendelea kuyafanyia kazi kuanzia pale walipoacha wenzake. Hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba Rais wa awamu ya nne atakuwa mwislamu. Kugongana kwa mahakama ya kadhi na Rais mwislamu wa awamu ya nne isiwe kesi ya kuzua kwamba Kikwete ndiye aliyeleta madai hayo.
 
hahaaa hiyo niliyo bold ndo imenichekesha sana.....keli na umenena ukweli mtupu

Tuache ushabiki tujenge hoja zitakazowasaidia watoa maamuzi kufikia hitimisho litakalosaidia kuanzisha au kutoanzisha mahakama ya kadhi bila kuleta vita ya kidini.
 
Tusubiri ccm wakanushe kwani kwa kutumia akili ya kawaida tu.................kipindi cha mkapa zilitumika tsh.9bilion kukarabati ilkulu kwa hiyo ilitakiwa japo isubiriwe miaka mingine kama kumi hivi ili kukarabati tena.......ajabu haka kabwana mdogo kanatumia 29bilion....kukarabati nini tena????????
Kweli kuna kiongozi wa nchi hapo????
Kikwete anaombea tu achaguliwe atimize kiu ya kislamu ya kuwaanzishia mahakama ya kadhi ambayo italeta vita.....[/QUOTE]

Duhi, hiyo itakuwa tamu na itamweka mrithi wake kutoka Sisiemuuuuu kwenye hali mbaya zaidi kisiasa, kwani inasemekana agenda ya kuanzisha hiyo mahakama imenyofolewa kinamna kutoka kwenye ilani ya uchaguzi ya 2010. Hapo ndo watu watakapotaka kujua huo uanzishwaji umetoka wapi?

Sidhani kama agenda ya mahakama ya kadhi imenyofolewa kinamna. Nilisikia, kama sio Pius Msekwa basi ni Yusuf Makamba akisema ilani ilisema CCM italitafutia ufumbuzi suala la mahakama ya kadhi sio kwa maana ya kuianzisha kisiasa bali kuzungumza na jumuia ya Waslamu namna ya kulitatua jambo hilo. Na sio waislamu tu bali na watanzania wengine kwa sababu suala hilo linagusa mambo mawili, imani na katiba. kwa upande wa imani ni la Waislamu na upande wa katiba ni ya watanzania wote. Huko uswazini tunasema suala hili linazungumzika tena kwa amani endapo kila mmoja wetu ataepusha jazba.
 
Hizo BILIONI 29 ni pamoja na yale matumizi ya shughuli za kifamilia tulizokuwa tunazifanyia WAITI-HAUSI na kumbuka familia yote iko WAITI -HAUSI unategemea nn hapo mkuu :mad2::mad2: halafu bado watu watapanga foleni kuipigia kura CCM

Haya ni majungu na hayatatufikisha hitimisho sahihi ya mada yetu. Kama haijaelezwa fedha hiyo imetumikaje basi ni vigumu kujadili mada inayokosa viambatisho muhimu vinavyoweza kutusadia kujua kama matumizi hayo ni sahihi au la. kwa kuangalia tarakimu 29 bilioni tu hatutakuwa tofauti na wasemavyo, "bila utafiti hauna haki ya kuzungumza" kwa kuwa unaweza kuipotosha jamii.

Mathalan, chukulia kwamba wote hapa tuna nyumba, mwingine anaweza kuwa amejenga kwa sh. milioni 20, milioni 30, milioni 50, milioni 80 na kuendelea. Kupata ukweli ni kwa nini nyumba hizo zimejengwa kwa gharama tofauti lakini zote ni nyumba inahitaji maelezo ya ziada.
 
Haya ni majungu na hayatatufikisha hitimisho sahihi ya mada yetu. Kama haijaelezwa fedha hiyo imetumikaje basi ni vigumu kujadili mada inayokosa viambatisho muhimu vinavyoweza kutusadia kujua kama matumizi hayo ni sahihi au la. kwa kuangalia tarakimu 29 bilioni tu hatutakuwa tofauti na wasemavyo, bila utafiti hauna haki ya kuzungumza kwa kuwa unaweza kuipotosha jamii.

Mathalan, chukulia kwamba wote hapa tuna nyumba, mwingine anaweza kuwa amejenga kwa sh. milioni 20, milioni 30, milioni 50, milioni 80 na kuendelea. Kupata ukweli ni kwa nini nyumba hizo zimejengwa kwa gharama tofauti lakini zote ni nyumba inahitaji maelezo ya ziada.

Umeanza ligi? how long are you staying?
 
Endelea kufumba macho ili usiuone ukweli!

Hatuwezi kuuona ukweli wakati mada imeletwa hapa kisiasa badala ya ki-Hasibu. Kwa Wahasibu au wakaguzi wa mahesabu huwezi kumkamata mtu mwizi bila vielelezo na ndio maana tunasema tarakimu pekee haitoshi kusema fedha iliyotumika ni nyingi au ndogo. Nani kasema wote hapa JF ni wanasiasa kila mtu na fani yake.
 
Back
Top Bottom