Ufisadi wa CHADEMA Moshi: Ofisi zote Halmashauri ilikuwa zifungwe kwa wiki nzima!!!

Reading between the lines kilichokusukuma ni UMBEA zaidi ya uzalendo.

Wingi wa Madiwani wa CHADEMA haukuwazuia madiwani wa vyama vingine kugomea mpango huo. Nani ajuaye pengine hata wazo hilo lilitoka kwa madiwani wa CCM. Na ikiwa bajeti ya halmashauri yao inaruhusu na wao wakaona ni jambo la manufaa kwa halmashauri yao shida iko wapi?

Hata hivyo, ilikuwa safari ya kipuuzi. Lilikuwa ni suala la kumpeleka Afisa Mazingira na mwingine anayehusika ambaye ktk kurudi kwake angetoa elimu aliyoipata huko kwa madiwani na wadau wengine
Mkuu unless una makengeza, soma gazeti Niashe, leo 14/9/2012, ukurasa wa 4 ili ujiridhishe kuwa UMBEA HUU NI WA KWELI.

Soma UMBEA mwingine wa gazeti hilo hilo la Nipashe, Meya huyo wa Moshi akijitetea kutohusika na mauaji ya kijana mtaani kwake.(Uk.8)
Achana na tabia ya kupuuza ukweli unaokugusa kwa kuuita ni umbea, ni ukosefu wa uwajibikaji na kupuuzia nafasi nzuri ya kujisahihisha.
 
Ukishakuwa CCM, akili na umakini vinapotea kabisa...
Dkt. Lawrence Gama (RIP) ana utofauti sana na Leonidas Gama. Kwa kuwa ulikuwa unaleta umbea, basi hata mambo ya msingi kama hayo yamekushinda. Nikushauri tu wewe na wenzako wote, Ndesa na timu yake na wananchi woooote waume kwa wake watawatesa sana kwa nguvu kubwa wanayoipa CHADEMA..

Mlikujaga na stori ya Diwani kutokumpa lifti mgonja, mpaka akafa. Sijui imeishia wapi? Narudia, mtasubiria sana mkono udondoke, lakini hautadondoka kamwe..
Huu ni unyasi, boti linakwenda mrama hilo, mwenye masikio na asikie.
 
Mnduoeye ndiyo maana nikahisi kuwa mtoa mada anaweza akawa amekoleza chumvi. siamini watu makini wanaweza kukanyaga kinyesi kirahisi kivile! asante kwa ufafanuzi naamini mwenye kujua sakata hilo kwa uhakika bila kujali kama kweli umeukalia ama la atatujuza sisi wenye msimamo wa kati.
Ni ukosefu wa kitu ile wazungu wanaita intergrity kwa mtu kuzuia nafasi moyoni mwake kukubali kukosolewa wakati mambo yako dhahiri.
Kwa vile wewe ni Tomaso tena ile aina mbaya, soma gazeti la Nipashe la leo(Uk.4)
 
Mkuu unless una makengeza, soma gazeti Niashe, leo 14/9/2012, ukurasa wa 4 ili ujiridhishe kuwa UMBEA HUU NI WA KWELI.

Soma UMBEA mwingine wa gazeti hilo hilo la Nipashe, Meya huyo wa Moshi akijitetea kutohusika na mauaji ya kijana mtaani kwake.(Uk.8)
Achana na tabia ya kupuuza ukweli unaokugusa kwa kuuita ni umbea, ni ukosefu wa uwajibikaji na kupuuzia nafasi nzuri ya kujisahihisha.

Mimi sijapinga mada, nimepinga namna yako ya uwasilishaji. Inaonekana jambo hili halikukusikitisha badala yake imekuwa faraja kwako kwamba limefanyika ili tu upate cha kuongea.

Ukiwa na akili angalau kidogo ungeona chini ya hiyo hiyo post unayoijibu nimeconclude pale, acha nikuwekee tena uone maoni yangu ni nini.
Hata hivyo, ilikuwa safari ya kipuuzi. Lilikuwa ni suala la kumpeleka Afisa Mazingira na mwingine anayehusika ambaye ktk kurudi kwake angetoa elimu aliyoipata huko kwa madiwani na wadau wengine

Mimi sio mnafiki mwenzio. Wewe ulifarijika kuwa hata CDM nao wanakosea, lkn mimi mtizamo wangu ni kwamba hata maoni ya Leonidas Gama nayo ni ya hovyo. Kwenda kwa awamu si suluhisho, suluhisho ni aende anayehusika na yeye atawafunza wenzake.

Soma na comment yangu ya chini ya hiyo uliyojibu utanielewa vizuri.
 
Katika kile ambacho kingeushangaza umma wa kiTanzania, uongozi WOTE wa Halmashauri ya mji wa Moshi ilijipangia safari ya kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya matembezi ya kusafisha macho na kuona usafi wa Jiji la Kigali.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Lawrence Gama, ameuwekea kauzibe mpango huo baada ya kuona gharama kubwa na ukosefu wa uwajibikaji kwa maana ya kusudio la kufunga Ofisi karibu zote za Halmashauri ya Moshi kwa wiki nzima au zaidi wakati wa matembezi hayo.

Haya wana CDM changamoto kwenu na utawala bora, matumizi sahihi ya fedha za mlipa kodi, somo la ufisadi bado kitendawili hata kwa wateule wenu.

Habari nzima uliyoiweka hapa imechafuliwa na uongo huo hapo juu kwenye blue,
Huyo mheshimiwa uliyemtaja hapo hayupo tena ... Au kuna mwingine mwenye jina kama hilo ??
Sasa habari nzima ni uongo mtupu ??? Au ni habari ya mwaka 2008 !!!
Hebu rekebisha hapo juu kwanza ndio uje tena na 'habari' hii.
Hii kama ingekuwa ni habari, basi magazeti yote ya CCM yangeiweka front page.
 
Mkuu usijipe faraja kuu kwenye kitu iliyo dhahiri, kweli nimekosea Ni Leonidas na siyo Lawrence, lakini wote si wa kule kule na chama kile kile?
Mantiki na maudhui ya habari hii iko intact.
 
Mimi sijapinga mada, nimepinga namna yako ya uwasilishaji. Inaonekana jambo hili halikukusikitisha badala yake imekuwa faraja kwako kwamba limefanyika ili tu upate cha kuongea.

Ukiwa na akili angalau kidogo ungeona chini ya hiyo hiyo post unayoijibu nimeconclude pale, acha nikuwekee tena uone maoni yangu ni nini.

Mimi sio mnafiki mwenzio. Wewe ulifarijika kuwa hata CDM nao wanakosea, lkn mimi mtizamo wangu ni kwamba hata maoni ya Leonidas Gama nayo ni ya hovyo. Kwenda kwa awamu si suluhisho, suluhisho ni aende anayehusika na yeye atawafunza wenzake.

Soma na comment yangu ya chini ya hiyo uliyojibu utanielewa vizuri.

Mkuu hili sakata limetuonyesha tu kuwa wanafiki tupo wengi na ndio maana nasema CDM=CCM ngoma droo!
Wezi na mafisadi ni wale wale, watu wanitaka nchi kuitawala ili wale kodi za wananchi.
Kuhusu ujumbe wako you will only live and achieve to your own expectation! Ride on!!!
 
Katika kile ambacho kingeushangaza umma wa kiTanzania, uongozi WOTE wa Halmashauri ya mji wa Moshi ilijipangia safari ya kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya matembezi ya kusafisha macho na kuona usafi wa Jiji la Kigali.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Lawrence Gama, ameuwekea kauzibe mpango huo baada ya kuona gharama kubwa na ukosefu wa uwajibikaji kwa maana ya kusudio la kufunga Ofisi karibu zote za Halmashauri ya Moshi kwa wiki nzima au zaidi wakati wa matembezi hayo.

Safari hii ambayo ya ujumbe wa Halmashauri ya Moshi, ina mentality ya kishule shule kwa maana ya excursions, na ingewahusu Madiwani wote pamoja na Meya, wakuu wa Idara wote(pamoja nafikiri na Mkurugenzi), viongozi waandamizi wote kwenye halmashauri.

Jumla ya watu waliojipangia kwenda safari hiyo ni 57( Du! wanaiga wapi hii!!)
Na wote wangelipwa posho nono ya kufikia Tshs milioni 200 kwa hii wiki moja tu!!

Hii Halmashauri inaongoza na Meya Jafari Michael na ina uwingi wa maDiwani wa CHADEMA pengine kuliko halmashauri yoyote nchini.

Meya Jafari Michael(CHADEMA) amesikika Radio One asubuhi hii akilalama kuhusu kuingiliwa na Mkuu wa Mkoa kuhusu safari hiyo.
Ati alikuwa waende "kujifunza usafi" kutoka Kigali-sawa na kumfundisha ng'ombe kutengeneza maziwa!

Haya wana CDM changamoto kwenu na utawala bora, matumizi sahihi ya fedha za mlipa kodi, somo la ufisadi bado kitendawili hata kwa wateule wenu.

Umeileta kishabiki sana michango yetu ipo very limited. Issue ni madiwani wengi kuwa CDM?
 
Umeileta kishabiki sana michango yetu ipo very limited. Issue ni madiwani wengi kuwa CDM?
Ha ha ha !
Nimelileta kwa unazi mkubwa , boli liko kona yenu.
Si mnajigamba kuwa CDM chama makini?
Umakini unaishia majukwaani tu au kwa vitendo?
Ufisadi ni dhambi isiyo na kabila, chama wala rangi, sasa tumedhihirishiwa.
 
Ingekuwa vyema hii habari, tungeipata pia kutoka upande wa pili , yaani wahusika wenyewe madiwani wa moshi, vinginevyo panaweza kuwa na upotoshaji hapa, maana mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa chama fulani, halmashauri inaongozwa na chama kingine, usitegemee hawa watu wafanye kazi pamoja bila kukwazana maana kila mmoja anatetea upande wake!
 
Mkuu usijipe faraja kuu kwenye kitu iliyo dhahiri, kweli nimekosea Ni Leonidas na siyo Lawrence, lakini wote si wa kule kule na chama kile kile? Mantiki na maudhui ya habari hii iko intact.
Kwa maana hiyo mtu akisema kuwa Julius Kambarage Nyerere ni mbunge wa Tanzania katika Bunge la Arika mashariki atakuwa yupo sahihi kwa sababu Makongoro Nyerere na Julius Nyerere ni wa kule kule na wapo ktk chama kimoja japokuwa Jukius Nyerere amefariki?. Kubali umekosea sio kuleta utetezi wa kitoto
 
Mkuu usijipe faraja kuu kwenye kitu iliyo dhahiri, kweli nimekosea Ni Leonidas na siyo Lawrence, lakini wote si wa kule kule na chama kile kile?
Mantiki na maudhui ya habari hii iko intact.

Kwa maana hiyo mtu akisema kuwa Julius Kambarage Nyerere ni mbunge wa Tanzania katika Bunge la Arika mashariki atakuwa yupo sahihi kwa sababu Makongoro Nyerere na Julius Nyerere ni wa kule kule na wapo ktk chama kimoja japokuwa Jukius Nyerere amefariki?. Kubali umekosea sio kuleta utetezi wa kitoto
Mkuu unless huelewi hata ulicho ki-quote, jibu la critique yako ya awali ni dhahiri hapo juu , sasa nashindwa kuelewa kinachokushinda kuelewa.
Mambo ya akina Nyerere wewe wayafahamu vizuri zaidi, jiridhishe na analogy yako.
 
sitaki kuona mshabiki yeyote wa chadema analeta unazi wake hapa. Hongera sana mkuu wa mkoa bwana gama kwa kuzuia uhuni huu, moshi ndio watu wanapaswa kwenda kujifunza usafi na si wao kwenda kujifunza usafi kwingine.

By the way jamani hivi usafi nao unafundishwa au ni kuagiza vifaa vya kufanyia usafi? Huu ni uhuni na kamwe haukubaliki.

hawawezi kukosa, wapo wengi ni aidha chadema addicted, zitto addicted, mbowe addicted, slaa addicted, yaani hata kama wahusika wataharibu, wao kuwadefend tu. Utadhani akina ritz1, rejao na ccm yao?
 
Mkuu usijipe faraja kuu kwenye kitu iliyo dhahiri, kweli nimekosea Ni Leonidas na siyo Lawrence, lakini wote si wa kule kule na chama kile kile?
Mantiki na maudhui ya habari hii iko intact.

Thead heading iko kishabiki zaidi.
Neno Ufisadi limetumika visivyo. Ufisadi ni "criminal offense". Mhusika wa ufisadi akigundulika tu anaburuzwa mahakamani. Kama ingekuwa ufisadi, madiwani wote walioshiriki wangeburuzwa mahakamani mara moja.
Hapa mkuu wa mkoa alikataa kwa sababu nyingine tu, na wala sio ufisadi.
Angalia vizuri article kwenye Nipashe. Moja wapo ya sehemu inasema hivi ...

Gama alisema kabla ya kumshauri Waziri, aliomba kujua baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na idadi ya watu watakaokwenda, muda, gharama na fedha hizo zitatokana na vyanzo gani vya mapato.

Alisema alijulishwa kuwa safari hiyo ingetumia Sh. milioni 123.2, ambapo kila mshiriki angelipwa Dola 420 (Sh. 6,61500), washiriki ni wakuu wa idara 14, watendaji wa halmashauri 14 na madiwani 29, hivyo kuwa na jumla ya watu 57. Ziara hiyo ilipangwa kuanza Septemba 15 hadi 20, mwaka huu huku wakieleza kuwa vyanzo vya mapato ni ruzuku ya
malipo ya safari za nje ya nchi na vyanzo vya ndani.

"Nimewauliza bajeti yenu ya mwaka ya kujengeana uwezo na amfunzo ni kiasi gani, wamenieleza ni Sh. milioni 130, wataalamu wangu wamepiga mahesabu na kuonyesha kuwa fedha waliyopanga kutumia ni ndogo sana kwani ziara hiyo inaweza kugharimu kati ya Sh. milioni 150 hadi 200…busara ya kawaida kabisa inakataa matumizi ya fedha yote kwenye ziara moja," alisema.
 
Hivi kweli study tour inaweza kusomba kila anayehusika au wataenda wachache waje kutoa mrejesho huyo Jaffari Meya wa Moshi sijui kama anajielewa
 
Manispaal ya Moshi mwaka huu imeingiza faida sana kuchota faida kidogo kwenda kupata mafunzo kwa wenzetu sio mbaya maana wakirudi watatoa mafunzo kwa madiwani wengine je? wakiomba kwenda Germany au Canada mtasemaje? acheni hizo wapeni nafasi wakajifunze
 
Hizi ni propaganda chafu sana, yaani mleta mada kachukua ukweli mdogo halafu kajaza uwongo mwingi sana hivyo kupotosha kila kitu.

UKWELI ULIOPO
1/Ilikuwa ni ziara ya kimafunzo katika mji wa Kigali kuhusiana na mambo mbalimbali ya uendeshaji wa miji.
(Sio kwenda kujifunza usafi, kumbuka mji wa moshi umefanikiwa sana kwenye usafi Tanzania)

2/Ingewahusu baadhi ya watendaji na madiwani wa manispaa ya mji wa moshi
(Sio madiwani tu, tena wa Chadema, wala sikweli kwamba watendaji wote wa manispaa wangesafiri na ofisi ikose watendaji)

3/Gharama za Safari nzima kwa ujumla ni Milioni 123 kwa ujumbe wote.
(Sio million 200 kwa kila mjumbe wa safari)

4/Suala nzima la safari hiyo lililuwa ni pendekezo la wazi la baraza la madiwani kwenda serikalini.
(Sio mpango wa kificho/hila kufanya Safari hiyo kwa madiwani wa Chadema)

5/Pendekezo hilo limekataliwa na Serikali kupitia mkurugenzi wa halmashauri ya Moshi Bi. Benedicta Kinabo kwa sababu serikali haina pesa za kutoa kwa mkupuo mmoja.
(Sio kwa sababu gharama za safari zina utata au safari ni ya kizushi au kwamba serikali hauna hela)

MZOZO ULIOPO SASA
*Kitendo cha Mkuu wa mkoa Mh. Gamma kwenda kulisema kwa waandishi wa habari iwe kama kashfa kwa madiwani wa Chadema
(Ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa halmashauri na mabaraza yake na kwa nafasi aliyokuwa nayo kufanya hivyo)

*Kitendo cha mkurugenzi wa halmashauri kushindwa kutoa sababu za msingi za kueleweka kwa madiwani za kukataa safari hiyo na wakati huo huo kutumia vyombo vya habari kulieneza Vibaya kabla hajalileta kwenye baraza la madiwani(Nalo linadaiwa ni kinyume cha kanumi na utaratibu)

MY TAKE
Mimi ni mpingaji mkubwa sana wa safari za namna hii(eg. Warsha,Kongamano,Ziara,Semina nk) kwa Viongozi/watumishi wa umma kwani zinagharama kubwa sana na zinaishia kuwa za kimatembezi tu na pia zinaweza kuzaa mambo ya ajabu kama hili.
Nawashauri CHADEMA kama wanampango wa kuongoza nchi huu utamaduni waanze kuufuta sasa.
 
Hao ndio wamepewa udiwani tu, ukiwapa nchi? kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Katika kile ambacho kingeushangaza umma wa kiTanzania, uongozi WOTE wa Halmashauri ya mji wa Moshi ilijipangia safari ya kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya matembezi ya kusafisha macho na kuona usafi wa Jiji la Kigali.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Lawrence Gama, ameuwekea kauzibe mpango huo baada ya kuona gharama kubwa na ukosefu wa uwajibikaji kwa maana ya kusudio la kufunga Ofisi karibu zote za Halmashauri ya Moshi kwa wiki nzima au zaidi wakati wa matembezi hayo.

Safari hii ambayo ya ujumbe wa Halmashauri ya Moshi, ina mentality ya kishule shule kwa maana ya excursions, na ingewahusu Madiwani wote pamoja na Meya, wakuu wa Idara wote(pamoja nafikiri na Mkurugenzi), viongozi waandamizi wote kwenye halmashauri.

Jumla ya watu waliojipangia kwenda safari hiyo ni 57( Du! wanaiga wapi hii!!)
Na wote wangelipwa posho nono ya kufikia Tshs milioni 200 kwa hii wiki moja tu!!

Hii Halmashauri inaongoza na Meya Jafari Michael na ina uwingi wa maDiwani wa CHADEMA pengine kuliko halmashauri yoyote nchini.

Meya Jafari Michael(CHADEMA) amesikika Radio One asubuhi hii akilalama kuhusu kuingiliwa na Mkuu wa Mkoa kuhusu safari hiyo.
Ati alikuwa waende "kujifunza usafi" kutoka Kigali-sawa na kumfundisha ng'ombe kutengeneza maziwa!

Haya wana CDM changamoto kwenu na utawala bora, matumizi sahihi ya fedha za mlipa kodi, somo la ufisadi bado kitendawili hata kwa wateule wenu.

Umeandika mwenyewe Kawrence Gama, halafu unatuuliza kwenye post nyingine kwamba Lawrence Gama si ameshafariki!,??.
Strange!,

Anyway, kama ni kweli, basi sio madiwani tu, mpaka mkurugenzi, wote hawafai. Hii tabia ya kutumia fedha za walipa kodi kwenda kujifunza the obvious sijui imetoka wapi.

Hat mkulu juzi kaenda kujifunza kulima mamananasi Ghana, na ameahidi atapeleka watu wakajifunze kilimo cha mananasi. . . . . SUA wanafanya nini? . . . .afterall tunajua yeye ndo mkulima wa mananasi . . .comflict of interest tayari.
 
Back
Top Bottom