UFISADI WA $121m WAMUONDOA WAZIRI CHINA

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
source: BBC News - Sacked Chinese railways minister in corruption inquiry
Waziri wa Reli wa China amefukuzwa kazi wakati anafanyiwa uchunguzi wa kupokea rushwa ya zaidi ya $121m, kwa ajili ya kutoa mikataba ya treni ziendazo kwa kasi.
Serikali ya ki-communist ya China isiyopenda kuonyesha udhaifu wa viongozi wake, ililazimika kuchukua hatua hiyo ngumu ili kutopoeza imani ya wananchi dhidi ya serikali yao, kwani hasira kubwa sana za raia wa china ni dhidi ya ufisadi.
 
hiyo ndiyo serikali , wachina hawana mchezo hata siku moja
wanasema hakuna kitu kinaitwa bahati mbaya, kama ukikosea basi sheria inachukua mkondo wake mara moja
Natamani kama tungekuwa na uwezo wa kukopa hao viongozi waje kwetu walau hata kwa miaka 5 tu ,tungakuwa na mabadiriko makubwa sana
 
Hapa kwetu Bongo kwa dau kubwa la $ 121M, Waziri huyo angeinunua ikulu, kamati kuu ya CCM akiwamo Mkuchika na Tambew Hiza, wabunge wote wa CCM pamoja na spika wao, mahakama, Hosea na Takukuru na familia yote ya katibu mkuu wa CCM wamtetee na kumsafisha ili achaguliwe rais wa awamu ya 5. Ni nchi kama Tanzania tu ufisadi unalipa sana... The land of impunity!
 
Back
Top Bottom