Ufisadi umeanzia kwenye familia mpaka ngazi ya taifa

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,273
3,750
Ndugu wanajamvi neno hili la ufisadi limekuwa likiongelewa sana kwenye midomo ya watanzania kwa kuwashutumu au kuwalaumu viongozi kwa kufanya ufisadi. Tumejaribu kujadili matokea kuliko kujadili chanzo cha hili neno ufisadi binafsi katika hili ufisadi unaanzia kwenye familia zetu hadi ngazi ya taifa. Mfano baba anamuachia mama nyumbani 10,000 mama anaamua kumega 2,000 na kuweka pembeni na mwambia mme wake pesa imeisha, mtoto anatumwa kitu dukani asipoulizwa chenji anaibania. Ili tuweze kupigana na hili zimwi ufisadi tuanzie kwenye famila zetu ili tujenge kizazi kilicho bora
 
Back
Top Bottom