Ufisadi sio tatizo, tatizo ni uzalishaji!!

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Leo imenibidi niandike kitu hii kutokana na hali halisi ya Tanzania na pengine kuwatatiza wengi kuelewa kwa sababu ya kichwa cha mada hii. Nimetafakari sana hali halisi ya Tanzania na kusema kweli imenishinda hata kumeza kwa sababu nilipokuwa Bongo nilikutana na wafanyabiashara wengi ambao wamekubali matokeo ya hali halisi hivyo kuendesha biashara zao ktk misingi ya kuwa Ufisadi sio tatizo bali uzalishaji ndio tatizo!..

Kwa wenye Mashule, Hospital, Daladala, Bodaboda, maduka, Mahotel, viwanda, mashirka ya kutoa huduma wote hawa wanaelewa wazi kwamba mali zao zinaibiwa na wafanyakazi. Wanaendesha biashara zao wakijua kuna asilimia fulani ya kuibiwa na wafanyakazi walowaajili, hivyo kinachotakiwa ni kuongeza uzalishaji zaidi ili kufidia kiasi kile unachoibiwa na waajiriwa.. Na kibaya zaidi ni kwamba kama huwezi kuvumilia kuibiwa basi huwezi kufanya biashara Tanzania. Hii ndio hali halisi na imekubaliwa na wafanyabiashara wote. Wizi ni utamaduni unaokubalika na hakuna uwajibikaji kutokana na wizi wa ndani..

Kuna rafiki yangu ana Restaurant yeye huibiwa nyama toka ktk friji yake, hivyo hununua kilo 60 akijua kati ya hizo kilo 5 zitaibiwana wafanyakazi, mwingine ana Bar anajua wafanyakazi huingiza pombe zao wakaziuza kabla ya mauzo yake lakini maadam mwisho wa siku wanaleta millioni 1 ya mauzo inatosha. Daladala vile vile dereva hupumzisha gari na akasema leo mauzo mabaya kwa sababu alikamatwa na traffic Polisi wakati haikutokea hivyo.Hii ndio Tanzania yangu..

Kitaifa sasa tunawakuta viongozi wakiiba mabillioni ya fedha pasi kuwajibika kwa sababu mfumo wa utendaji kazi ni ule ule wenye shida la kutoharamisha wizi. Kwa hali yoyote ile serikali itaibiwa kwa sababu wananchi wenyewe wameupitisha wizi kuwa ni ujanja wa kuishi mjini. Ni utamaduni unaokubalika maadam hukamatwi kwa sababu inatakiwa ushahidi wa kumkamata mwizi na nyama mkononi ndio unaweza kumtuhumu mtu na hata kumfikisha mahakamani lakini sii swala la kuhesabu zimeibiwa kilo ngapi kuwa ushahidi wa kuibiwa. Wenyewe wanasema ulomkamata na ngozi ndiye aliyeiba ng'ombe!

Kwa hiyo, katika mazingira haya ya kutatatisha watu wengi sana waanaamini Tatizo la nchi yetu sio UFISADI, huwezi kukomesha wizi wala kuwajibisha watu kama suluhisho isipokuwa ni kuongeza Uzalishaji kufidia kiwango cha wizi ili faida unayokusudia ipatikane ktk ujenzi wa Taifa letu. Tumeibiwa sana toka ubinafsishaji wa viwanfda na mashirika, uuzaji wa nyumba za serikali, mikataba ya uwekezaji toka IPTL, Rada, Madini na kadhalika. Wahusika wa wizi na ufisadi huu hawaonekani kuwa na makosa kutokana na utamaduni wetu wa kutojali mwizi ambaye hana ngozi .. Sasa kilichobakia ni Ardhi maana tumesha ibiwa kote na hali ya uchumi wetu unazidi kudumaa na kuwa sugu - Wanasema ati ili tuendelee nguvu na juhudi kubwa zaidi inatakiwa kulijaza pakacha linalovuja!

Je, kuna ukweli kwamba uchumi wetu umedumaa kwa sababu - Ufisadi sio tatizo bali tatizo ni Uzalishaji mdogo?
 
its complicated.......ufisadi unaweza kuua kabisa uzalishaji....

kuna aina za ufisadi....ufisadi wa Asia...barabara zinajengwa,nchi zinaendelea lakini kuna ufisadi still
South Korea wamewafunga marais wawili kwa ufisadi but still wanapiga hatua....
but tazama Nigeria....mafuta yoote waliyouza Nigeria toka uhuru ni sawa na GDP ya South Africa.....
but yako wapi hayo maendeleo????
ufisadi wa Tanzania unafanana na wa Nigeria..tazama mfano Rais wa Brazil amekuja hapa na kusema waziwazi
wanaweza kusaidia 'kumaliza tatizo la umeme kwa mda mfupi kwa kujenga the cheapest hydropower plant mto Rufiji....
hakuna alietaka hata kufuatilia hiyo habari na vyombo vya habari utasemwa vilihongwa na wabunge wote kimya..
 
Yote ni tatizo ...ila kwangu swala ni tatizo gani lishugulikiwe kwanza kisha lipi lifute..!!

ufisadi usipo shughulikiwa kwanza hata tuzalishe vp pesa hazina zinafisadiwa ,je itatufaidi nini?
I suggest kind of parallel processiing ktk swala hili ,,,tukihubiri ubaya wa ufisadi iwepo na awareness ya bidii ya kazi ktk kujenga nchi.
 
Mkuu matatizo yetu ni makubwa mno.., ni kweli kuna wengine kutokana na maisha magumu basi wanakula kwa urefu wa kamba zao, Bongo kila mtu mwizi asipokula basi hawezi kusukuma siku (ingawa mazoea hujenga tabia na watu wameshazoea..)

Ila mkuu kulingana na tatizo la sasa tusiongelee hii petty thieves (ambalo ni tatizo kweli) ila tatizo kubwa zaidi ambalo linatokea sasa ni la viongozi kuuza nchi which means hawatuibii sisi peke yetu bali wanauza na mtaji wa wajuu zetu...

Hii inanikumbusha story ya "The Golden Goose" yaani baada ya mkulima kupata bata anayetaga mayai ya dhahabu kwa tamaa yake akamchinja ili atoe mayai yote tumboni kuliko kusubiri yai kila siku...., utaona kwamba hawa viongozi kwa kiasi kidogo tu cha 10% wanauza nchi kwa bei nafuu sana wakati wangeweza kufanya mambo kwa manufaa ya wengi...

Wengi ni mafisadi mkuu hata Gaddaffi alikuwa anachota pesa lakini yeye afadhali alifanya machache tofauti huku hakuna wanachokifanya kabisa

By the Way Ufisadi nao ni Tatizo ambalo lipo kwenye culture yetu sasa hivi na ni vigumu kuisha ila kuzalisha zaidi kutasaidia wale wanaoiba sababu ya njaa wapunguze... kwahiyo nakubaliana na wewe in the sense kwamba huwezi kumwambia mtu aache kuiba wakati ana njaa mpe chakula ashibe ili akiiba umwonyeshe option nyingine ambayo angechukua.
 
naona umeeleza vyema.

tatizo la ufisadi ni tatizo la kijamii zaidi hivyo pamoja na kuilaumu serikali ni vyema pia kuieleza jamii ukweli kama ulivyoliweka hapa bwana Mkandara. sasa hivi huko mtaani ukiwa mwizi (na una pesa zako) unasifika zaidi.
kuna rafiki yangu alidondosha pesa noti kama za laki tatu hivi na zikasambaa katika eneo lenye watu wengi, huwezi amini watu walizishambulia na kutokomea nazo naye akabahatika kuokota elf 40 tu. wale watu hawakujali kurudisha pesa zile. hivyo hata suala la fisadi ni nafasi tu (mtu akipata nafasi anakomba)

naunga mkono hoja na ningeomba hata wanaharakati wasiishambulie serikali tu, wachukue na jukumu la kuielimisha jamii ibadilike. wahimize uzalishaji mali (nashukuru nilimsikia Mh Mdee akisisitiza kwamba watu waache kulalama kila kukicha bali wafanye kazi kwa juhudi na maarifa)
 
Nimewasoma wakuu zangu, na nitajariubu kjila hali kuiendeleza mada hii kwa sababu maamuzi ya kifira ni leo na sii kesho. Ukumbi wa siasa hapa JF umejaa habari za watu kusemana, matusi ya UCCM na Uchadema sijui Magamba vs Magwanda ili hali hakuna mawazo ya kutatua matatizo isipokuwa kunyoosheana vidole nani nyani na kima nani..

Lakini tumeshindwa kutazama matatizo yetu, tumeshindwa kuzitazama sura zetu wenyewe ktk kioo na kujua how ugly we look!..Na nijuavyo mimi uwekzekano wa ufumbuzi wa matatizo yetu upo kati ya vitu hivi viwili.. Tanzania inaongoza kwa Ufisadi maanake toka kiti kikubwa hadi kijakazi ni Ufisadi kwa kwenda mbele hali tukikazana kupiga makelele ya kuhimiza kuongeza uzalishaji..

Kama alivyosema Voiceof Reasoning - MAZOEA HUJENGA TABIA. haya ni maneno mazito sana na yanatisha haswa ukifikiria kwamba Ufisadi umekuwa mazoea ya wananchi wote na hivyo umejenga TABIA ambayo leo sii kikwazo cha maendeleo. Lakini ukweli umesimama wapi?.. Binadamu kwa hulka yake akiweza kupata msaada wa kuzalisha akaweza kuiba ama kupata kitu hicho bure pasipo kutumia nguvu ama akili, hawezi kuacha kuchukua urahisi huo dhidi ya kutumia nguvu zake..

Nikiwa na maana ya kwamba kelele zote tunazopiga kuhusu kuongeza uzal;ishaji haziwezi kuwa na mafanikio ikiwa ktk kuongeza nguvu hizo tutakuwa na watu wanaosubiri kunyakua matunda..Hata mkulima wa shamba la mahindi kama atalima na nyani kila siku wanakuja vuna huwezi tegemea kuongeza mavuno bila kufikiria kwamba hata idadi ya nyani nayo itaongezeka kwa sababu ya urahisi wa kupata chakula. Kwa hiyo, hizi mbiu za kuongeza uzalshaji zinakuja na gharama kubwa sana kwa ni kwa kila uwekezaji kuna mafisadi wanaopiga mahesabu na kualikana.. Hesabu yao inaongezeka kila mwaka kiasi kwamba hatutakuwa na mwananchi mzalishaji isipokuwa kila mmoja tasubiri nafasi ya kufisadi..

Bado naamini sana kwamba UFISADI ni tatizo kubwa sana, vita yake inatakiwa ifanyike haraka iwezekanavyo laa sivyo Tanzania yetu itakuwa haitawaliki tena. Tulipofika leo ni njia panda! maamuzi magumu yanatakiwa kufanyika na serikali na kama serikali haiwezi basi wananchi wenyewe wachukue jukumu hilo kwa sababu Ufisadi una mnyororo mrefu sana. Toka mkulima hadi anauza mazao yake, mfugaji, mvuvi, mashirika ya huduma kote kuna watu wanasubiri deal la kufisadi aidha mwenye mali ama mzalsiahji.. Hizi hesabu za kufiidia Ufisadi ulokubalika ktk jamii nadhani unatugharimu zaidi ya uwezo wetu ktk kuzalisha..
 
Salaam,

Nimekua nikifuatilia mazungumzo mengi ya hapa na huko mtaani kuhusu siasa na mustakabali wa nchi yetu tukielekea uchaguzi wa 2015 na nimeona tuna jambo moja la muhimu tunalolidharau, hatulifahamu vizuri au tuko kwenye hali mbaya kiuongozi kiasi kwamba tunasahau misingi ya uongozi mzuri katika demokrasia yeyote ile.

Katika nchi yeyote kuna itikadi inayoongoza nchi kisiasa, kijamii na kiuchumi na katika itikadi hii ndiyo viongozi wanatengeneza dira za kimaendeleo za taifa, miiko na maadili ya uongozi. Ndani ya itikadi tawala unazaliwa mfumo tawala ambao unaifanyia kazi itikadi kutekeleza azma yake katika kuendesha taifa. Naam, sasa hapa nafikiri tumeona jinsi mfumo tawala ulivyokua muhimu katika kutimiza azma zetu kimaendeleo. Bila ya mfumo si itikadi, dira, katiba, taasisi nk vinavyoweza kufanya kazi kikamilifu.

Tatizo la kimsingi la Tanzania yetu siyo itikadi, (itikadi ya kiliberali ipo), siyo dira, (kuna dira 2025), siyo mipango, (wataalamu wanapanga kila siku mafaili yanajaa tu wizarani na katika idara zingine za serikali). tatizo la msingi ni uongozi usiokua wa kizalendo unaoletwa na mfumo tawala wa kifisadi ambao unatoa faida binafsi za kisiasa na kiuchumi kwa wajanja wachache kwa gharama ya walio wengi na hapa ndipo tunapoona matatizo yote haya katika nchi iliyobarikiwa kwa mengi.

Tukiwa tunaelekea uchaguzi muhimu kwa mstakabali wa nchi hii wa 2015 naona shauku imekua ni kuchambua uzuri wa chama au ubaya wake na wafuasi wamekua wakishindana kwamba CDM itafanya na itasimamia hiki au CCM ikimuweka huyu au yule itakua hivi huku mada tawala katika vyama vyote viwili imekua ni ufisadi, dowans, mafisadi, ufisadi tena. Haya yote ni mzozano usiokua na tija kwetu labda kwa wachache makada wa juu wa vyama husika, sisi tunahitaji kujua mikakati itayokuepo kupambana na huu mfumo fisadi kwani hili ndiyo tatizo/kikwazo kikuu cha kuneemesha jamii yetu ya kitanzania. Kwa mfano katiba mpya ni wazo zuri, lakini haitotosha kuupunguza nguvu au kuondoa mfumo wa kinyonyaji wa kifisadi, (siyo assertions ni fikra tu naomba kukosolewa).

Atakuja huyu au yule, kitakuja chama hiki au kile lakini bila ya kuuondoa huu mfumo wa kifisadi watawala hawa wajao ili kujizatiti kisiasa itabidi angalau nyuma ya pazia kushirikiana kwa kiasi fulani na wahimili wa mfumo wa kifisadi na hii itakua ni muendelezo wa mfumo huu. Kwa hili hapa ndugu zangu tutakua tunacheza muziki ule ule sema tu ma DJ tofauti.

Naomba tuchangie

Shukhran
 
Jibu kwa title ya mada yako kabla sijaspoma ndani nasema ni yote 2 .Sasa naenda kusoma nitaibuka baadaye .
 
.............shida yetu kubwa ni udogo wa mawazo unaletekezwa na uvivu wa kufikiri nieleweke hivyo kwa kuanzia, pili kuwa fisadi ni sawa na ugonjwa ambao chanzo chake ni mfumo wa kifisadi, Nitakupeni mfano, wana CCM pamoja na watanzania wengine mathalani wanaaminishwa na wanaotutawala kwamba Lowasa, Chenge na Rostamu ndio mafisadi wa nchi hii na kwa tafsiri yao ni kwamba wakiondoka kwenye vikao vya maamuzi, narudia wakiondoka kwenye vikao vya maamuzi watakuwa wameushinda ufisadi, Inahitajika akili ya kiwendawazimu kuamini haya. Hivyo tunakataa chanzo na/au ugonjwa wenyewe ambao ni CCM na ufisadi wenyewe respectively
 
Basically ni wote mfumo wa kifisadi na mafisadi wenyewe..uwezi tengenisha ufisadi na mafisadi...maana kwanza mfumo wetu ulionekana kuwa ni bora kabisa,lakini walipopata upenyo hao mafisadi wakaubadilisha ukawa wa ufisadi...unaweza ukajitahidi kuwa na mfumo mzuri kabisa wa kuendesha mambo,lakini unapoingiliwa na kirusi cha ufisadi kinasambaa kwa kasi na kuaharibu kila kitu....kwa dhana hii tunapaswa kupigana kuwaondoa mafisadi kwenye mamlaka na kutafuta mfumo mpya wa uongozi utakaozuia kirusi hiki kuingia kiurahisi....hata kipindi cha mwalimu ufisadi ulikuwepo isipokuwa walikuwa wakali kama Mwalimu mwenyewe alivyowai kusema....
 
Tatizo letu ni moja tu. UJINGA, Na ndo maana mpaka leo from 1961 tuko nyuma kwa sababu ya ujinga. wakati wenzetu kenya, uganda etc wakiinvest kwenye elimu za vyuo vikuu sisi tunahangaika eti kufuta ujinga wa kusoma na kuandika.
 
Ugonjwa wetu una herufi tatu tu yaani: CCM. Hiki ndicho chanzo cha ufisadi na mafisadi wa nchi hii.
 
elimu muhimu lakini iendane na katiba mpya. Katiba mpya ilenge kwenye utawala na taasisi za kiutawala. Bunge liwe na nguvu zaidi kuikosoa serikali, mahakama huru ziwafunge mafisadi pindi wakihukumiwa, tume huru ya uchaguzi ili serikali ziwe na maadili na nidhamu ili kuepuka kupigiwa kura za hapana na wananchi. hii nafikiri itasaidia zaidi.

Siyo kila nchi za kidemokrasia zina elimu ya juu kwa elimu katika kutatua hili tatizo la msingi kama ufisadi siyo ya msingi sana, nakuliana na katiba kwanza, elimu itatengemaa tu kukiwa na ufanisi wa kazi. mbona Nigeria wana elimu nafikiri ya kiwango cha juu au Kenya lakini ufisadi ni mkubwa bado?
 
Bw Mkandara kwa heshima zote nakubaliana na wewe kuhusu uzalishaji, lakini kmbuka uzalishaji unaletwa na mfumo unaotoa tija, aei, na uzalendo katika kuzalisha huko. huu mfumo unawanyima watu wengi nafasi ya kuzalisha wanabaki kubaki kwenye informal sectors hizi zisizochangia kwenye pato la taifa ambalo lingesaidia kipato na kua chachu ya wengine kuzalisha pia na hii process ingeendelea. wengine wenye vipaji wanakimbia nje ya nchi kwa kukosa nafasi hapa kwao, ukianzisha ka biashara kadogo TRA wanakuja haraka haraka kukudai wakati mabwana wakubwa wengine wanapeta, huu umeme unafikiri hauathairi wazalishaji na uzalishaji wao? na umeletwa na nini?

kwa kifupi huu mfumo hauleti tija ya uzalishaji katika taifa. Siyo mfumo unaongeza ufanisi katika uchumi na uzalishaji. namaliza kwa kusema uzalishaji unaendana na mfumo madhubuti wenye ufanisi na usiyoruhusu upotevu wa kipato na kodi zetu.
 
Bw Mkandara kwa heshima zote nakubaliana na wewe kuhusu uzalishaji, lakini kmbuka uzalishaji unaletwa na mfumo unaotoa tija, aei, na uzalendo katika kuzalisha huko. huu mfumo unawanyima watu wengi nafasi ya kuzalisha wanabaki kubaki kwenye informal sectors hizi zisizochangia kwenye pato la taifa ambalo lingesaidia kipato na kua chachu ya wengine kuzalisha pia na hii process ingeendelea. wengine wenye vipaji wanakimbia nje ya nchi kwa kukosa nafasi hapa kwao, ukianzisha ka biashara kadogo TRA wanakuja haraka haraka kukudai wakati mabwana wakubwa wengine wanapeta, huu umeme unafikiri hauathairi wazalishaji na uzalishaji wao? na umeletwa na nini?

kwa kifupi huu mfumo hauleti tija ya uzalishaji katika taifa. Siyo mfumo unaongeza ufanisi katika uchumi na uzalishaji. namaliza kwa kusema uzalishaji unaendana na mfumo madhubuti wenye ufanisi na usiyoruhusu upotevu wa kipato na kodi zetu.
Na ndio maana nimeandika kichwa cha mada kinyume ili nipate hoja zenu.. yanibidi nikubali kwamba UJINGA unaweza kuwa sababu kubwa sana ya matokeo yote haya hivyo niseme Uzalishaji na hata Ufisadi yaweza kuwa matunda ya Ujinga, maanake huwezi kupata viongozi bora kati ya wajinga!
 
Na ndio maana nimeandika kichwa cha mada kinyume ili nipate hoja zenu.. yanibidi nikubali kwamba UJINGA unaweza kuwa sababu kubwa sana ya matokeo yote haya hivyo niseme Uzalishaji na hata Ufisadi yaweza kuwa matunda ya Ujinga, maanake huwezi kupata viongozi bora kati ya wajinga!

Nakubali Kenya wanajitahidi na Zambia wanafanya kweli, Tanzania hatujawafikia hawa kwa kiwango cha elimu kiujumla, Bw Mkandara hata madai yetu ya katiba wasomi na wapinzani wameanzisha kwa nia safi lakini gurudumu limekwama kwa wananchi walio wengi, (nakubaliana na wewe hapa kwa sababu ya upeo finyu nisingependa kuwaita wenzangu wajinga) bila public pressure ya kutosha nafikiri hatupati katiba mpya na mfumo fisadi utaendelea. ahsante kwa mchango
 
Back
Top Bottom