Ufisadi shule za msingi waibuliwa na dr slaa

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
519
Dr slaa ameibua ufisadi ktk shule za msingi akihutubia katika mkutano wake mkoani Ruvuma jana alidai kuwa michango ya madawati inachangishwa kila mwaka kwa wanafunzi je ni lini madawati yatatosha wanafunzi wasichangishwe tena maana madarasa ni yale yale na madawati yanachangishwa kila mwaka ina maana madarasa hayo hayajai madawati kwa miaka yote hiyo! Nakubaliana naye kabisa kuna ufisadi shule za msingi ambao haujamulikwa kabisa na unawaumiza sana wanyonge wanaopeleka watoto wao.Pili kila baada ya miezi mitatu kila shule hupewa fungu la fedha za capitation ambazo hutakiwa kununulia vitabu,vifaa na matengenezo sasa tembelea shule ngapi zina library ya vitabu tangu zimeanzishwa zinapokea fedha hizo na wanadai vitabu vimenunuliwa Je kwa shule yenye miaka 10 iweje isiwe na library sasa kichekesho hata vitabu ukiuliza viko vichache na hata wanafunzi hawajui kama kuna vitabu vipo shuleni waazime wasome wizara inafanya kazi gani kuhakikisha vitabu vinanunuliwa mashuleni!!au ndo mkondo wa kuchakachua hela za vitabu!!!
 
Dah hapo kuna hoja ngumu sana,michango kila mwaka alaf madarasa hayajai na hayaongezeki. Serikali inanunua vitabu ila shule zina kabati moja umo umo vitabu,chaki,fimbo na majarida ndo utunzwa kwa pamoja,aya ni maajabu!
 
hahahaha....jamaa anawafumbua macho taratibu! Mwisho wa siku mpende msipende, CCM LAZIMA ITOKE! Tumechoka kuburuzwa na wajinga na wezi!
 
Yaani vituko vya ccm haviishi nchi hiii!
Yaani fedha za serikali zinachakachuliwa kuanzia juu hadi shuleni serikali za vijiji. Halimashauri zote huozo mtupu, ndio maana wanangangania umeya. Hili la shule na michango ya madawati wazazi wote walivalie njuga, hesabu zipigwe tujue kuna fedha kiasi gani madawati mangapi yamenunuliwa, kila shule ifanye hivyo. Dr Slaa azid kuelimisha watu watoke usingizini, fedha nyingi za watu zinaliwa ovyo na mafisadi uchwala!!!!!!!!!! Ahsante Dr kwa kufumbua watu macho!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom